CHADEMA liangalieni hili linawashushia imani kwa wananchi

GeniusBrain

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
4,315
306
Jana yalifanyika maadhimisho ya miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo viongozi mbali mbali wa vyama vyote vya siasa walihudhuria isipokuwa CDM peke yao. Hii ni ishara mbaya kwa chama cha siasa kinacho tafuta ridhaa ya watanzania ya kuongoza nchi kujitenga na sherehe za kitaifa. Ikumbukwe kuwa sherehe hizi za Kitaifa hazipo Tanzania tu, zipo duniani kote na huwa ni za wananchi wote bila kutizama itikadi za vyama vyao. Kwani hata CDM wakipata ridhaa ya watanzania hizi sherehe watazifanya tu. CDM pevukeni kifikra na kimawazo mnajishusha hadhi yenu kwa vitu km hivi na ndipo watu wanakuja na hoja ya kuwa mna ajenda za kuvuruga nchi pindi mtakapo pewa madaraka
 
Wewe akili yako kama nyengo, inaangalia upande mmoja tu! Hawa virus wa magamba wanasumbua sana akili za waungwana. Jana hukusikiliza mahojiano ya Dr Slaa na star tv? Acha upuuzi wako.
 
Hahahahahaaa!!!!
Akili kama nyengo!!
Hii nimeipenda, yani akili kama ya Rebosome
 
Full of ****!kila siku zinavyozidi imani ya wananchi wanaokua na imani na cdm inazidi kuongezeka kwa kasi,ushaidi tosha ni jinsi wana c.c.m wanavyokimbia kwa wingi na kujiunga c.d.m,kuanzia madiwani,wenyeviti wa vijiji na wanachama wa kawaida,na hata chaguzi za vijiji zinatoa majawabu,sasa wewe unaongelea imani gani ya wananchi wanayoipoteza kwa c.d.m!si kila sherehe ina tija kwa taifa,mtasherekeaje kitu chenye kasoro ambapo pande zote zinalalama?labda ni fair kwa watu *******
 
Imani inashuka kwa wananchi wa wapi? Mwananchi gani wa Tanganyika au Zanzibar mwenye shida na huo muungano wako kama siyo viongozi wa magamba tu?
 
Full of ****!kila siku zinavyozidi imani ya wananchi wanaokua na imani na cdm inazidi kuongezeka kwa kasi,ushaidi tosha ni jinsi wana c.c.m wanavyokimbia kwa wingi na kujiunga c.d.m,kuanzia madiwani,wenyeviti wa vijiji na wanachama wa kawaida,na hata chaguzi za vijiji zinatoa majawabu,sasa wewe unaongelea imani gani ya wananchi wanayoipoteza kwa c.d.m!si kila sherehe ina tija kwa taifa,mtasherekeaje kitu chenye kasoro ambapo pande zote zinalalama?labda ni fair kwa watu *******

Viongozi wote walikuwa kwenye kesi zao mahakamani.
 
Jana yalifanyika maadhimisho ya miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo viongozi mbali mbali wa vyama vyote vya siasa walihudhuria isipokuwa CDM peke yao. Hii ni ishara mbaya kwa chama cha siasa kinacho tafuta ridhaa ya watanzania ya kuongoza nchi kujitenga na sherehe za kitaifa. Ikumbukwe kuwa sherehe hizi za Kitaifa hazipo Tanzania tu, zipo duniani kote na huwa ni za wananchi wote bila kutizama itikadi za vyama vyao. Kwani hata CDM wakipata ridhaa ya watanzania hizi sherehe watazifanya tu. CDM pevukeni kifikra na kimawazo mnajishusha hadhi yenu kwa vitu km hivi na ndipo watu wanakuja na hoja ya kuwa mna ajenda za kuvuruga nchi pindi mtakapo pewa madaraka

Uhalali wa muungano unaujua?uliwahi kuuliulizia hili?Hebu fikiri zaidi ya hapo ulipo kwa kuangalia tu kuwa Chadema hawakuhudhuria Sherehe za muungano.
 
Hawa magamba wanakosa hoja kabisa yaani embu fikiria wanawaza kwa njia gani sasa? Manake wanashindwa kupost thread ambayo ina mantiki na ukweli ambao mtu hawezi kupinga.
 
Jana yalifanyika maadhimisho ya miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo viongozi mbali mbali wa vyama vyote vya siasa walihudhuria isipokuwa CDM peke yao. Hii ni ishara mbaya kwa chama cha siasa kinacho tafuta ridhaa ya watanzania ya kuongoza nchi kujitenga na sherehe za kitaifa. Ikumbukwe kuwa sherehe hizi za Kitaifa hazipo Tanzania tu, zipo duniani kote na huwa ni za wananchi wote bila kutizama itikadi za vyama vyao. Kwani hata CDM wakipata ridhaa ya watanzania hizi sherehe watazifanya tu. CDM pevukeni kifikra na kimawazo mnajishusha hadhi yenu kwa vitu km hivi na ndipo watu wanakuja na hoja ya kuwa mna ajenda za kuvuruga nchi pindi mtakapo pewa madaraka

Hapo kwenye red,
Wewe unataka kumaanisha kuwa mtu yoyote aliyehudhuria sherehe za muungano hana ajenda ya kuvuruga nchi.
Hebu angalia yafuatayo:-
Mawaziri wote walihudhuria sherehe hizo, na mawaziri hao hao ndio watuhumiwa wakubwa kwenye ripoti za CAG, na ripoti za kamati za bunge kwa ufujaji na ubadhilifu wa fedha za umma. Sasa hao hawavurugi nchi ??
Mafisadi wote walihudhuria shsrehe za muungano, vipi hao nao kwa ufisadi wao hawavurugi nchi ??
Waliosaini mikataba mibovu ya madini pia walihudhuria shsrehe za muungano. Hapo vipi??

Pole sana mwana-JF wewe.
 
hv mm huwa najiuliza huu muungano unakitu gani mpka mkuu wa kaya apige marufuku mijadala yake kuna umuhimu gani kuwa nao kma wananchi haturuhusiwi kuujadili namna bora ya kuuboresha kwan kuna nn kilichojificha humo ndani?
 
Mleta mada! Ulishaona wapi unahuzuria harusi ambayo haina hata cheti cha ndoa?
 
Kweli kabisa Ndallo hata Kamanda Silaa anasema hivyo. Na kwa kuongezea, wananchi wana matatizo mengi ya kimaendeleo eg. ukosefu wa maji safi, matibabu nk. Sasa sherehe za Muungano zinasaidiaje kutatua matatizo ya wananchi?
 
Hapo kwenye red,
Wewe unataka kumaanisha kuwa mtu yoyote aliyehudhuria sherehe za muungano hana ajenda ya kuvuruga nchi.
Hebu angalia yafuatayo:-
Mawaziri wote walihudhuria sherehe hizo, na mawaziri hao hao ndio watuhumiwa wakubwa kwenye ripoti za CAG, na ripoti za kamati za bunge kwa ufujaji na ubadhilifu wa fedha za umma. Sasa hao hawavurugi nchi ??
Mafisadi wote walihudhuria shsrehe za muungano, vipi hao nao kwa ufisadi wao hawavurugi nchi ??
Waliosaini mikataba mibovu ya madini pia walihudhuria shsrehe za muungano. Hapo vipi??

Pole sana mwana-JF wewe.

Nimeipenda gharama zote zilizotumika si zingenunua madawa au madawati na vitu vinginevyo vya muhimu
 
Back
Top Bottom