CHADEMA kutowavumilia wanachama mafisadi

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
na Danson Kaijage, Dodoma



CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa kamwe hakitawavumilia wanachama ambao wanasaka uongozi ndani ya chama hicho kwa lengo la kufanya ufisadi badala ya kuwatumikia wananchi na umma kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Viti Maalumu, Regia Mtema (CHADEMA), wakati akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu katika kongamano la wanavyuo ambao ni wanachama wa chama hicho.
Mbunge huyo alisema CHADEMA inasimamia misingi ya uaminifu pamoja na kuwatumikia wanachi wote ili kuweza kuleta maendeleo kwa jamii ya Watanzania wote.

Akizungumzia mchakato wa uchaguzi wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (CHAVITA), kugombea nafasi mbalimbali, aliwataka vijana ambao wana lengo la kugombea nafasi hizo kwa malengo ya kufanya ufisadi ni bora wakajiengua mapema ili kuachia nafasi kwa wale ambao wapo tayari kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.

Mbunge huyo alidai kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kinapingana na sera ya kukumbatia na kulea watu ambao wanamalengo ya kujilimbikizia mali badala ya kuwasaidia wananchi ili kuweza kujikwamua katika umasikini uliokithiri. Mbali na hilo, Regia aliwataka vijana wa CHADEMA kuhakikisha wanajipanga kufungua matawi kuanzia ngazi ya vitongozi hadi kata ili kuweza kujipanga kuingia katika ushindani wa uchaguzi wa mwaka 2014 ikiwa ni pamoja na maandalizi ya uchaguzi mkuu mwaka 2015.
 
Back
Top Bottom