CHADEMA Kumshitaki RPC Kagera

Kamende

JF-Expert Member
Mar 1, 2008
416
45
Baada ya kutoa taarifa za uongo kuhusu CHADEMA kumiliki silaha mbali mbali zikiwepo Magobore, mapanga, visu na tindikali mbele ya vyombo vya habari sasa RPC wa mkoa wa Kagera Salewi anakabiliwa na wakati mgumu baada ya CHADEMA kuamua kumfikisha mahakamani kwa tuhuma ya kukichafua na kuudanganya umma.

Kamanda wa uchaguzi wa CHADEMA mjini hapa alisema kuwa kama Salewi angekuwa mstaarabu angetokeza mbele ya jamii tena kuomba radhi baada ya jeshi lake kufanya upekuzi na kukuta kuwa gari letu halina kitu chochote cha hatari.

"Kutokufanya hivyo kunatudhihirishia sisi na umma mzima wa watanzania kuwa hatua ya kukichafua chama ilikuwa ni kutekeleza agizo la CCM" Tunamfikisha mahakamani ili aijue thamani ya dhamana aliyopewa na nchi yetu". Alisema John Mrema ambaye ndiye kamanda wa uchaguzi Biharamulo kwa CHADEMA.
 
Japo hiyo kesi itaishia kupigwa dana dana, ila itasaidia kufikisha ujumbe kwa uma kwamba kuna hila za namna hiyo zinazo fanywa makusudi kuharibu sifa ya chama mbadala!

Kamende, asante kwa kutupa yanayo jiri B'mlo.
 
hata kama itaisha kwa danadana ni heri kama usemavyo iingie kwenye kumbukumbu ili siku ikifika ya kuchukua serikali tunaanza na keso viporo ili kuwawajibisha watu wote wanaojiweka juu ya sheria na kuvunja katiba ya nchi kwa kutumia vibaya vyeo walivyopewa kama dhamana.
 
Baadhi ya watendaji wa umma, wanayafanya hayo wayafanyao sio kwa kutumwa na CCM, bali kujikomba kwa CCM kuendeleza ulaji, Mahita aliukwaa uIGP baada ya kumvurumishia Mrema mabomu.
 
Ndo maana itakuwa vyema kesi hiyo ifunguliwe, hata kama itafanyiwa mazingaombwe lakini itatoa fundisho kwa wengine wenye mipango hiyo ya ama kuwa wametumwa ama kujipendekeza wenyewe kwa mafisadi!
 
Baadhi ya watendaji wa umma, wanayafanya hayo wayafanyao sio kwa kutumwa na CCM, bali kujikomba kwa CCM kuendeleza ulaji, Mahita aliukwaa uIGP baada ya kumvurumishia Mrema mabomu.

na mara nyingi huwa ni watendaji wenyewe kudhani wanamfurahisha ''boss''.

nasubiri siku ambayo chaguzi za Tanzania utapambwa zaidi na habari za sera na mipango kuliko mbwembwe na vituko!
 
Tanzania hakuna sera, CCM hawana sera, kuna ahadi tu. Je ahadi ni sera?. Labda hii tuitafutie thread yake.
Nasema hakuna sera kwani wanasema tutajenga barabara, tutajenga mashule nk - lengo ni kuondoa umaskini nk. Wanadai wameyafanya yote waliyoahidi kwenye ilani yao, lakini bado takwimu zinaonyesha kuwa maskini wameongezeka, akina mama wajawazito wanaokufa wameongezeka, watoto chini ya miaka 5 wanaokufa wameongezeka nk. Sasa kama umetekeleza ahadi na bado lengo halikufikiwa, si hizo ni ahadi tu na siyo sera?.Au wakubali kuwa hawajatekeleza.
 
Back
Top Bottom