IsayaMwita
JF-Expert Member
- Mar 9, 2008
- 1,127
- 140
Ndugu zangu,
"Kuishi kwingi kuona mengi" huenda haya ninayoyasema sasa ni asilimia ndogo sana walikuwa na ufahamu na wanakumbuka. Kipindi cha muongo wa kwanza wa siasa za vyama vingi kambi ya upinzani ilitawaliwa na Augustine Mrema na vyama vyake kwanza akiwa NCCR-Mageuzi na baadaye TLP.
Mrema akiwa na kauli yake ya "kulipua mabomu" bungeni na nje ya Bunge alisababisha mawaziri kadha wa kadha kung'atuka na hatimaye kuondoka katika siasa.Sera ya "kulipua mabomu" ilisababisha Mrema kuletewa zengwe na kutimuliwa kwenye nyumba ya serikali ambamo aliishi kama mpangaji.
Baada ya watu kusikia kuwa Mrema anaondolowa kwenye nyumba aliyopanga walikusanyika eneo la Manzese Argentina na kutangaza kununua nyumba mara moja na kumpa hati milki ili aendelee "kulipua mabomu".Nyumba ikapatikana Sinza mbapo Mrema na mkewe Rose walihamia na kuishi bila bugdha.
Tabia ya watanzania kusaidia ipo pale pale lakini haimaanishi kuwa watakuchagua uwe Rais wao.Nakumbuka pamoja na wananchi kumnunulia nyumba ilipofika mwaka 2000 kuelekea uchaguzi mkuu Mrema alikataa gari lake kusukumwa baada ya kugundua kuwa linapokuja suala la kura hawampi.
Tutaendelea kuwapa historia vijana wetu na kuwakumbusha waliosahau.
Sent using Jamii Forums mobile app