CHADEMA Kilimanjaro yateua mgombea Jimbo la Siha huku wakisubiri baraka za Kamati Kuu

CHADEMA haitafanikiwa kamwe kwa kubadilikabadilika kama kinyonga Mara kususia Mara kushiriki jinga kabisa
 
Maandalizi yatakuwaje kupambana na CCM na madalali wake wenye nguvu wafuatao:
-Serikali kupitia mkuu wa Mkoa na wilaya pamoja na yule aliyevishwa koti la msimamizi mkuu yaani DED?
-Polisi ambalo ni wakala mkuu wa CCM mwenye bunduki na magari washawasha?
- Usalama wa taifa wakala muhimu wa watu wasiojulikana ambao hata sasa wamejipanga kumteka huyo mgombea au hata mkewe?
- Wala green guard wanaopewa silaha za moto na polisi?
- Wakala mkuu wa CCM ni tume ya uchaguzi ambaya imeapishwa kutokutangaza wapinzani.

Rejea chaguzi za madiwani zilizopita juzi
 
Mimi ni CHADEMA DAMU na najisikia fahari kwa hilo ila huu ni ujinga unafiki ushenzi na upumbavu ambao Mbowe na kamati kuu mmeufanya sasa tukishindwa mtasema tena tumeibiwa kura???

Singida kaskazini walijitoa.... Songea mjini walijitoa.... Alafu haya majimbo mawili ndio tunaweka mgombea ilihali tunajua kabisa kuwa TUME ni ile ile na sheria za uchaguzi ni zile zile

Kwa hili CHADEMA mmeboronga sana na amini nawaambia hamtoshinda jimbo hata moja maana CCM hawawezi kukubali kuingia hasara ya kununua majimbo afu yarudi upinzani.... Never.... Na ole wenu tusikie mnaanza kulia lia baada ya uchaguzi eti mmeibiwa kura!!!!

Kwa hapa tulipofikia hatutakiwi kulegeza kamba kiasi hiki mtamfanya magufuli azidi kutudharau...... Ingawa Dk slaa alisaliti mabadiliko ila sidhani kama angekubali upuuzi huu mnaoufanya!!!

Mniradhi kama nimetumia maneno makali though......
kwani maamuzi ya kushiriki yalishatoka? hivi bado hujapona ugonjwa wako? Slaa na mbowe nani alisaliti mabadiliko? hivi mnaamini lowasa atawapa mabadililko?
 
Sasa uko Siha hakuna gharama?
Ipo lkn aliyeisababisha ni Godwin wala sio huyo muombea wa CDM. Kimsingi Godwin anapaswa kujibu swali hili, hivi CCM pakimboa kabla ya 2020 aakihamia chama kingine je atagombea tena? Hao ni vibaya kuliingiza taifa kwenye gharama kubwa namna hii kisa mihemko yake tuu?
 
Ni upuuzi kumsimamisha mgombea Siha huku uliacha kumsimamisha mgombea Longido
Hamtaweza kushinda na itakuwa aibu kubwa zaidi,
Kama mmesusa,suseni kweli kweli
Ukiwa wa moto kuwa wa moto na sio kuwa vuguvugu
Upuuzi tu kama democracy haipo ni haipo tu walikuwa hawana sabb ya kunagua majimbo nchi ni moja na vyombo vya ulinzi na usalama ni vile vile
Kwahiyo mnataka fisi aendelee kususiwa bucha?
 
Inawezekana tatizo likawa ni fedha (ruzuku). Pengine chaguzi ndogo zilizopita zilifanyika kwenye kipindi ambacho ruzuku ilikuwa haijatoka Hazina, na sasa pengine ruzuku imetoka. Najaribu kufikiria tu nje ya boksi, na pengine huenda ninachokifikiria kikawa hakina ukweli wowote.
 
kwani maamuzi ya kushiriki yalishatoka? hivi bado hujapona ugonjwa wako? Slaa na mbowe nani alisaliti mabadiliko? hivi mnaamini lowasa atawapa mabadililko?
Embu na wwe usintibue mchana wote huu kama huna la kuchangia pita pembeni.... Huyo Dr slaa amesaliti mabadiliko ndio!! Maana muda tuliomuhitaji akaona mke ni muhim kuliko maslahi ya watanzania million 50....... Mbowe kasaliti makubaliano gani??? Slaa mbona aliafiki lowasaa agombee CHADEMA ila mke akagoma the rest is history...... Kuhusu lowassa hakuna aliyesema mtu mmoja ataleta mabadiliko ila timu nzima ya CHADEMA nina imani nayo kwamba ingeleta mabadiliko maana tumeona tokea bungeni wakipigania maslahi ya sisi wananchi wadogo ingawa walikuwa wachache
 
HAYA WENZAKO WASHACHUKUA FOMU, NENDA KAJINYONGE.
 
HAYA WENZAKO WASHACHUKUA FOMU, NENDA KAJINYONGE.
Unazungumziaje wanachama wenzako waCCM wapya hata mwezi hawajafikisha wala hawajajenga chama alafu wamefika tu wiki moja wanapewa kugombea ubunge?? Nipe maoni yako maana nakumbuka kwa lowassa mlitoka povu kweli

Unafki at it's best!!!
 
Back
Top Bottom