CHADEMA iwe makini na Mbatia pamoja na Zitto

Joblube

JF-Expert Member
Mar 4, 2011
369
151
Wana JF napenda kutoa angalizo kwa CDM kuwa makini na hawa jamaa wawili kwa hawa wanakazi muhimu kwao ya kuibomoa CDM kwani ni maagenti wa usalama wa taifa.

Huyu Mbatia kwa wale tuliokuwa naye pale chuo kukuu mwaka wa 1990 mtakumbuka mambo aliyotufanyia tulipoanzisha ule mgomo. Mwenzetu tulikuwa tunapanga na yeye kwenye mkutano wetu kumbe usiku wake anapelekeka taarifa ya kile tunachopanga tunawahiwa na tulimgundua na kutenga.

Mtakumbumbuka pia alisababisha Rais wa Campas ya muhimbili ndugu Kimaro kufukuzwa chuo na hakurudi tena baada ya kugundua kuwa msaliti alikuwa katikati yetu. Huyu jammaa anajifanya mpinzani hamna lolote ni sawa na Zitto nionavyomienendo yake.

Kama hamuamini subiri sikuzinakuja mtagundua hayo nisemayo.

Hawa jamaa hupandikizwa kwa staili ya hali ya juu sana kiasi cha nyie kutotambua cha msingi ni kuwa makini na hawa jamaa wasije wakachelewesha ukombozi wa Watanzania.
 
ni hoja yako; lakini jihadhali sana kuzua migawanyiko ndani ya CDM-mkombozi wetu kama utakuwa umetumwa!!. Km mbatia ongelea, lakini zitto ni jemedari wetu wa CDM-muache kumugusa na usimuhusishe na mbatia!!
 
zitto ni jembe ila huwa anateleza kama wanadamu wengine,na huu ni muda wa Zitto kurudisha imani kwetu sie Walalahoi.
 
Dhambi za ubaguzi ni mbaya sana. Mfukuzeni basi muone yale ya Kafulila.

Chadema wachawi wenu wanajulikana ni wale share holders wa kampuni ya Chadema. waondoeni hao kwanza kisha hivyo vidagaa.
 
Mkuu naona umeamua kujiunga kwa style ya ku-attack..., Ijumaa hadi leo J3.., ngoja tuvute subra tutaendelea kufahamu mwelekeo wako!
 
Nitasema kuhusu Mbatia. Ya Zitto nitakuachia mwenyewe - mi simjui kivile.

Stori yako ya 1990 si sahihi.... I know all what happened (who did what when where).
Na kusema Mbatia ni usalama wa taifa nalo si sahihi..... Namfahamu sana Mbatia fyi.

Lakini nakiri kuwa siasa zimem-transform sana Mbatia. Sifa ya upiganaji aliyokuwa nayo pale UDSM na wakati anajiunga NCCR sasa imemtoka kabisa...amekuwa opportunist na mtu wa kupenda misifa.

Haambiliki hata akishauriwa ....so, si mtu wa kumwamini tena na amekosa sifa kama mpambanaji kuelekea ukombozi tunaoutamani kwenye taifa hili.
 
Taarifa yako ina mvuto kusoma, kwa maana ya kichwa habari na maneno yaliyomo lakini imekaa kama tetesi kuliko ukweli.
 
Ni alama na ishara zipi zinathibitisha kuwa wanatumiwa na vyombo vya kijasusi, japo mfano mmoja au miwili ingeipa uzito taarifa yako.
 
Ukweli ni kuwa zito tumempoteza, na sio tena tegemeo letu kama kamanda wa kuleta mabadiliko. TIME WILL TELL. Unafahamu walivomkata maini huyo zito? mafisadi wamempa 400Milioni na kumfunglia kampuni ya ujenzi mheshimiwa Zito. Unafahamu walichofanya baada ya hapo? tenda zote za ujenzi wa madaraja mkoani Kigoma kapewa yeye zito na kampuni yake. This is true, not longolongo za mitaani. Asanteni
 
shughuli ya UVSISIEMU? hapa tumekwenda mbali sana mkuu, huwa nina hofu na zitto kimsimamo lkn kwa haya mkuu utakuwa umetumwa

Join Date : 3rd February 2011
Posts : 2
Thanks
0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power : 0
 
Nitasema kuhusu Mbatia. Ya Zitto nitakuachia mwenyewe - mi simjui kivile.

Stori yako ya 1990 si sahihi.... I know all what happened (who did what when where).
Na kusema Mbatia ni usalama wa taifa nalo si sahihi..... Namfahamu sana Mbatia fyi.

Lakini nakiri kuwa siasa zimem-transform sana Mbatia. Sifa ya upiganaji aliyokuwa nayo pale UDSM na wakati anajiunga NCCR sasa imemtoka kabisa...amekuwa opportunist na mtu wa kupenda misifa.

Haambiliki hata akishauriwa ....so, si mtu wa kumwamini tena na amekosa sifa kama mpambanaji kuelekea ukombozi tunaoutamani kwenye taifa hili.

Napata shida kidogo kama kweli una elimu ya chuo kikuu halafu unakosa upeo wa kuelewa kwamba idara za ujasusi dunia mzima lazima ziwe na informers wao, basi hiyo elimu yako ina walakini, elewa kwamba kwamba idara ya ujasusi inakuwa na waajiliwa wake na mwakala wake wake ambao wanalipwa pesa kwa kazi maalum na muda maalum, huu unakuwa ni mkataba wa muda. Zitto kuwa na ukaribu na Deputy Director wa usalama wa Taifa ni lazima kuna some information anazipata kutoka kwa Zitto, na ni taarifa hizo hizo za kiitelijensia ndio wamemdanganya Mkwere kwamba CHADEMA sasa wanapanga kumpinduwa.
Ukitaka kujuwa vizuri kazi za mainformer angalia Israel huwa inapewa na nani taarifa za Magaidi wa kiparestina? Angalia movie moja inaitwa Delta Force one ndio utajifunza vizuri kuhusu hawa mainformer, ila tofauti ya mainformer wa kwetu ni kwamba njaa zimewazidi ndio maana wanatambulika kirahisi, lakini kwa kawaida ni ngumu sana kumjuwa informer.
 
Ukweli ni kuwa zito tumempoteza, na sio tena tegemeo letu kama kamanda wa kuleta mabadiliko. TIME WILL TELL. Unafahamu walivomkata maini huyo zito? mafisadi wamempa 400Milioni na kumfunglia kampuni ya ujenzi mheshimiwa Zito. Unafahamu walichofanya baada ya hapo? tenda zote za ujenzi wa madaraja mkoani Kigoma kapewa yeye zito na kampuni yake. This is true, not longolongo za mitaani. Asanteni

Mwananyati tutaamini vipi kama siyo longologo ikiwa hakuna hata moja ya ushahidi wa udhibitisho japo kutaja jina la kampuni anayomiliki ili nasisi tuifuatilie
 
Ile miaka ya kuogopa hujuma ishapita kwani wananchi washajua ni nani ana uzalendo wa kweli na chi yake.

Ila nawahurumia siku kiongozi wa wananchi akichukua hii nchi kuna watu wengi sana watakwenda kuishi uhamishoni kwa hali inavyokwenda.

PEOPLES POWER.
 
Tatizo Zitto hatokei Kilimanjaro au Arusha. Ukabila wa chadema

cdm inakubalika tz nzima sio mikoa ulotaja, acha hizo, kwani wale prof k.kahigi kule bukombe ni arusha au klm, nyerere musoma mjini sugu mby, silinde mbz, wenje nyamgn, na kwingineko ni arushana klm?
 
Mi mwenyewe nshashtuka mapema, na si hawa tu tumwongeze na Shibuda ndan ya red blackets. Hawa ni vichomi wa CDM. Asante kaka! Lakn vp huna mawasiliano ya mbatia ya direct il uweze kumpa habar kuwa tushamshtukia?
 
Nadhani CHADEMA ni zaidi ya hizi propaganda Chafu,hebu tujaribu kujitenga na haya majungu.Tuko juu ya hizi ajenda chafu...yeyote anayemchafua mtu kwa malengo ya kisiasa hata kama yupo CHADEMA mimi nampuuza
 
Swala la kuwa makini ni la muhimu sana hasa juu ya Zitto mbatia simjui, Zito Zuberi Kabwe nina uhakika 100% ila sidhanai kama kuwa Informer wa TISS kunamnyima mtu kutetea Nchni yake maana hata wao kunawakati utakuta kuna mambo hawayapendi sana, kuna weakness moja ya Zitto inayomlazimu akubali kuwa kibaraka wa hao jamaa hana ujanja hapo ingawa yawezekana hakupenda ila baadae itam-cost sana.
 
Back
Top Bottom