CHADEMA hakitapokea wanachama wapya wa vyama vingine

​ukilala unota CHADEMA,ukiamka unamuona Dr. Slaa pole sana(ni vita rahisi kupambana na Lowasa kuliko kupambana na Dr. Slaa hamlali Lumumba)
 
hakuna ukweli kwa hili kwa jinsi ulivyoandika. wanachama wapya ni LAZIMA ila inategemea ni wanachama wa aina gani
 
Katika habari za saa za kituo cha ITV mwenyekiti wa CHADEMA ametangaza uamuzi huo.
kwa mapendekezo yangu hii ni hatua nzuri itasidia sana kuepuka na hizi habari za masalia na mamluki wengine ndani ya chama.
......huu si utaratibu mzuri wa kutoa maelekezo yanayopingana na katiba ya chama.....katiba ipo na inaeleza sifa za kuwa mwanachama....kama haikidhi haja irekebishwe.....ifuatwe katiba ili kupunguza migongano isiyo na faida...........
 
Upande mmoja ndio: cdm kupitia m4c wako mbioni kupata wanachama wengi vijana/wenye muono na wengi ambao si wanachama wa vyama vingine. zaidi ya tzns 12m ambao si wanachama ccm wanatosha kuingiza cdm ikulu.

upande mwingine, mlango wa wanaccm kwa vigezo maalum uwe wazi: mfano, kuwa mwanachama cdm bila mdaraka kwa mda furani- zaidi baada ya uchaguzi.

cdm imalisheni dafutari lenu la wana cdm pure kueleke 2015.
Kuwakwepa wanachama wapya wa CCM ni kutokubaliana na ukweli wa mambo.
Zaidi ya 95% ya wananchama wa CHADEMA wametoka CCM
Ambaye anabisha aeleze wote Dr Slaa, Mbowe na wengine wametoka wapi.
Wengine hata kadi bado wanazo kama souvenirs!!!
 
MWENYEKITI AMEKURUPUKA KATIKA HILI..
  • Je katiba ya chama inazungumzia nin kuhusu kujiunga chadema?
  • kwanini chama kilikuja na mchakato wa VUA GAMBA VAA GWANDA, tena uliotumia pesa nyingi tu kunadi sela za chama nchi nzima ili kuwakomboa wana CCM kutoka ufisadini?
  • Je ana uhakika gani kuwa kila mtu atakayeamia ni mamluki,mbona kuna watu walihamia kutoka CCM na sasa ndo central figure za CHADEMA i.e. Dr slaa
  • Je kama chadema ipo kwa ajili ya ukombozi wa watanzania wote, hao wana CCM sio watanzania??
  • JE chama kimeshindwa kuweka misingi imara ya uongozi na wanachama kiasi cha kuyumbishwa na mamluki?anataka kusema katiba na irani za chadema ni dhaifu kiasi icho?
  • Je ni lazima kila atayehamia awe katika uongozi?au kuingia katika vikao vya juu vya chama kiasi cha kuvuluga utaratibu.
Nikiwa kama mwanachama mtiifu wa chadema naomba majibu...kwani wapiganaji wengi tu wa chadema wametoka CCM akiwemo Kamanda mawazo,Dr slaa, na wengine wengi tuu...KAMA MWENYEKITI HAJAKURUPUKA THEN ATOE SABABU ZAIDI YA KUOGOPA MAMRUKI......PEEEEEOPLESSSSSSSSS

Subiri kusikia kwa viongozi wa chama wenyewe au mtu aliye nukuu vema. Watu wengine wanasikia habari mwishoni wanarusha hapa.

Tutapata updates za hakika kuhusu hili
 
Mtoa uzi unatakiwa kuelewa kabla hujaandika! Ni wanachama wanaotaka kuingia CHADEMA wapate kugombea maana ukurasa huo tutaufunga mapema! Wanachama wa kawaida tunawapokea hata ucku ukituamsha!
 
Gazeti la jamboleo la leo heading yake iko hivi "Chadema yabadili mbinu za kuingia Ikulu 2015" Yawapiga 'stop' Watakaotimuliwa CCM

Mleta uzi nadhani habari umesikia vibaya ITV.
 
Mbona mnajichanganya kuna uzi humu CHADEMA yakomba wanachama wapya 1000.

Wapya si ndo hao hao fresh mkuu Ritz? Wanamaanisha hapa hawataki tena wanachama design ya kina Shonza Juliana kama mlivyowapokea!! Wanataka kitu na moto wake si mamluki!! Si mnajua hii ndiyo njia yenu!! Baada ya kujifunza kwa Shibuda si unaona wale ambao wamekuja nyuma yake not heard kabisa!! Pambanua!!
 
Chadema achana kabisa na wanaCCM.Chukua the youngs,energetic,the (Mnyika,Silinde,Zitto,Lema,Sugu,Halima Mdee etc)likes.Nchi tunataka ichukuliwe na vijana wakiongozwa Dr Slaa-2015 siyo mbali.Vijana wa CCM wamelewa utajiri wa kifisadi wa wazazi wao.Achana nao kabisa.
 
Back
Top Bottom