CHADEMA haina mtu mwenye uwezo kushindana na Rais Samia katika sanduku la kura uchaguzi ujao

Nchi ina Rais Imara, shupavu ,jasiri na madhubuti madarakani ndio maana unaona uchumi wetu ukiendelea kufanya vizuri sana,maisha ya watanzania yakiendelea kuwa bora na yenye kuleta matumaini,huduma za kijamii zikiendelea kupelekwa karibu zaidi ya wananchi. Miradi ya maendeleo ikiendelea kujengwa kila mahali inayochochea maendeleo na fursa za ajira kwa maelfu ya vijana.
hupewi hata ubaloz wa ten house boss
 
CCM haijawahi kushinda uchaguzi wowote kwenye Sandusky la kura.The voice of the son of Abeid Karume.
 
Kama hizo ndio sifa za kua Raisi mbona bibi yenu hana hizo sifa hata kidogo 🤔au kwa vile aliingia dirisha dogo 🤔 yule bibi akishindanishwa hata na Heche alafu uchaguzi ukiwa huru na haki atachakazwa mapema Sana
 
Kwenye swala la chadema kukosa mtu mwenye sifa tajwa katika andiko lako naweza kukubaliana na wewe kwa aslimia 85% .

Lakini kwenye izo sifa tajwa za upande wa pili kidogo na mashaka na lengo lako kama ni kusifia bila kupima au unafurahisha nafsi, mimi binafsi naamini kiongozi mwenye maono anayeona miaka mingi mbele anaweka mipango ya muda mrefu na muda mfupi iliyo wazi na wananchi wa taifa lake wasome na watoe hoja zao kama wanachi mipango hiyo wanaionaje na si kubabaisha.

Kama Rais wetu ana sifa hiyo angeeweka bayana kama raisi anaona nini na anataka twende wapi kwa miaka yake mitatu aliyo rithi kiti lakini hawezi kufanya na hakuna raisi katika Taifa hili amewahi kufanya hivoo wala Chama cha siasa kilichowahi kufanya hivo ni ahadi tu zisizo na forecasting plan, HANA SIFA YA MAONO AONI CHOCHOTE HILO NAKATAA.

Hili la kuungwa mikono na mamiloni ya watanzania umeandika kwa hisia tu huna data kama una data leta tuzione.

Hili la kurudisha mikutano ya kisasa halina maana kama wananchi hawawezi kuchagua wanachotaka katika chaguzi zao kama anaamanisha anajali awape wanachi tume huru ya uchaguzi kuanzia mwakani kwenye chaguzi za serikali za mitaa hapa kweli atakuwa amemaanisha kujali uhuru wa watu wake.

Kitu pekee ambacho anacho ni icho angalau ana kifua.#bereal
 
Kama hizo ndio sifa za kua Raisi mbona bibi yenu hana hizo sifa hata kidogo 🤔au kwa vile aliingia dirisha dogo 🤔 yule bibi akishindanishwa hata na Heche alafu uchaguzi ukiwa huru na haki atachakazwa mapema Sana
That's true
 
Kwenye swala la chadema kukosa mtu mwenye sifa tajwa katika andiko lako naweza kukubaliana na wewe kwa aslimia 85% . Lakini kwenye izo sifa tajwa za upande ...
Kinachowanyima ushindi upinzani katika sanduku la kura siyo Tume tu bali ni ubovu wa sera zao,udhaifu wa wagombea wao,kukosa sera na ajenda zinazogusa maisha ya watu, kukosa misimamo wa kauli zao na ajenda zao na katika hili rejea kilichotokea 2015 juu ya kile walichokuwa wanahubiri majukwaani na kile walichokuja kufanya. Kukosa safu ya uongozi yenye kuleta matumaini pamoja na kutumia lugha za matusi,ubaguzi kwa misingi ya ukabila, ukanda, jinsia na Udini.

Ukija kwa CCM chini ya Rais samia unaona ni Rais mwenye maono ya mbali na anayetazama miaka mia mbele, ndio maana unaona akitoa Elimu bure na bora ili mwisho wa siku tupate wasomi wa kada zote na kutuondolea adha ya kufauta huduma au utaalamu nje ya nchi kwa kukosa wataalamu ndani ya nchi anataka Taifa la watu walio na Elimu bora ili waje watumie na kuziibua fursa mbalimbali zilizopo maeneo mbalimbali nchini.

Ndio maana unaona akitoa nakubadili muelekeo wa kilimo ili kiwe ni kilimo cha biashara kitakachomnufaisha mkulima na kumuondolea umasikini wa kipato,lakini pia kitakachotoa ajira kwa watu wengi huwa nchi ikiwa na chakula cha kutosha na kulisha Bara zima la Afrika.
 
Rasilimali zetu ni salama katika mikono salama ya Rais samia.Pia napenda kuendelea kusema ya kuwa hakuna mwenye uwezo wala ubavu wa kushindana na Rais samia katika sanduku la kura. Hayupo mtu huyo .kama yupo niambie ni nani ili nikupe uchambuzi wangu.
Hata kuandika majina ya watu kwa kuanza na capital letter 'S' hujui, halafu na wewe unatazamia kupata teuzi kwa uchawa wa majitaka.

You are a total disgrace to manhood.
 
Kama hizo ndio sifa za kua Raisi mbona bibi yenu hana hizo sifa hata kidogo 🤔au kwa vile aliingia dirisha dogo 🤔 yule bibi akishindanishwa hata na Heche alafu uchaguzi ukiwa huru na haki atachakazwa mapema Sana
Rais samia amekidhi sifa hizo ndio maana Anaendelea kupeta na kuiteka mioyo ya watanzania,kwa kuwa amekidhi matarajio ya wananchi na kuwapatia kile walichokuwa wanakihitaji kwa muda mrefu.sasa wamempata.Huyo Heche hata uenyekiti wakanda ndani ya CHADEMA alishindwa na kuishia kupewa tu kwa huruma za mwenye kigoda.
 
Luca ukishashiba balagha huishiwi kucheua/kubehua vituko.
Mimi naongea ukweli hata kama ni mchungu kwa baadhi ya watu.huwezi ukaacha kumpa mgonjwa dawa unayojuwa itamponya eti kwa kuogopa uchungu wake na sauti ya kulia kwake na kukunja sura kwa mgonjwa. Lazima anywe tu .hivyo CHADEMA lazima wapewe dawa yao.
 
Mimi naongea ukweli hata kama ni mchungu kwa baadhi ya watu.huwezi ukaacha kumpa mgonjwa dawa unayojuwa itamponya eti kwa kuogopa uchungu wake na sauti ya kulia kwake na kukunja sura kwa mgonjwa. Lazima anywe tu .hivyo CHADEMA lazima wapewe dawa yao.
Kwa hiyo wanaopaswa kubugizwa dawa ni CDM tu?Kwani AFP,UDP,CHAUMA nk hawafai?Unaonesha unavyowaogopa CDM!🤔
 
Blah blah na yada yada nyingi, uchaguzi ukija mnatuma poliCCM kuiba masanduku ya kura. Idiot.
 
Kwa hiyo wanaopaswa kubugizwa dawa ni CDM tu?Kwani AFP,UDP,CHAUMA nk hawafai?Unaonesha unavyowaogopa CDM!🤔
Hapana siwezi kuwaogopa hata kidogo CHADEMA.siwezi kukiogopa chama ambacho hakina uwezo wa kuandaa hata ilani yake tu achilia mbali kukosa kwake msimamo.hapa rejea uchaguzi wa 2015 ambapo CHADEMA iliwaambia watanzania wakasome ilani yake huko mitandao,ilani ambayo hata wao wenyewe CHADEMA walishindwa kueleza inahusu nini na kuamua kumfanya mgombea kuwa ndio ilani yao,hivyo mgombe akawa anapanda majukwaani na kuzungumza kwa kutegemeana na mzuka unavyopanda au kile anachokumbuka au kumjia mdomoni mwake.
 
Blah blah na yada yada nyingi, uchaguzi ukija mnatuma poliCCM kuiba masanduku ya kura. Idiot.
CCM inapita kwa kubebwa na ubora wa sera na ajenda zake zinazogusa maisha ya watu ,wakati wao CHADEMA mtu ndio huwa ilani yao tu.
 
Kinachowanyima ushindi upinzani katika sanduku la kura siyo Tume tu bali ni ubovu wa sera zao,udhaifu wa wagombea wao,kukosa sera na ajenda zinazogusa maisha ya watu,kukosa misimamo wa kauli zao na ajenda zao na katika hili rejea kilichotokea 2015 juu ya kile walichokuwa wanahubiri majukwaani na kile walichokuja kufanya. Kukosa safu ya uongozi yenye kuleta matumaini pamoja na kutumia lugha za matusi,ubaguzi kwa misingi ya ukabila, ukanda, jinsia na Udini.

Ukija kwa CCM chini ya Rais samia unaona ni Rais mwenye maono ya mbali na anayetazama miaka mia mbele ,ndio maana unaona akitoa Elimu bure na bora ili mwisho wa siku tupate wasomi wa kada zote na kutuondolea adha ya kufauta huduma au utaalamu nje ya nchi kwa kukosa wataalamu ndani ya nchi.anataka Taifa la watu walio na Elimu bora ili waje watumie na kuziibua fursa mbalimbali zilizopo maeneo mbalimbali nchini.Ndio maana unaona akitoa nakubadili muelekeo wa kilimo ili kiwe ni kilimo cha biashara kitakachomnufaisha mkulima na kumuondolea umasikini wa kipato,lakini pia kitakachotoa ajira kwa watu wengi huwa nchi ikiwa na chakula cha kutosha na kulisha Bara zima la Afrika.
Maono kama yapii maono ni dira ya kufikisha watu miaka mingi ijayo, matatizo ya Tanzania ni ujinga umaskini na maradhi , dira yenye mipango ya kuonesha atapita wapi hadi kufika kutatua changamoto hizo iko wapii imeandikwa wapi ikajaidiliwa wapii, Israel ina maono ya kilimo since 1947 iliandikwa plan ya miaka mia na ikafatwa na ikaishi na kila waziri mkuu aliifata na mabadiliko yanaonekana nchi ni jangwa ila inajilisha kwa kilimo chake, maono ya raisi ayakai kichwani ni documentation ndio maono yanapaswa kuwekwa sio bla bla unazo sema et ana maono yapi? We ni muongeaji tu
 
Back
Top Bottom