Chadema, changamkeni mumpate Harold Sungusia!

Mwanaharakatihuru

JF-Expert Member
Mar 21, 2012
477
120
Huyu jamaa anaonekana yupo makini sana katika kujenga hoja na anajiamini, yani mtu kama huyu na Mnyika, Lisuu na Zitto wakikaa pamoja nadhani CHADEMA itakuwa unstoppable.

Kamati ya Uenezi ya Chama tukumbuke eagle does not flock you have to find one at a time.
 
Mkuu unashauri Chadema wampe cheo au nafasi ya ubunge au nini.
 
Mbona wetu huyo pamoja na kuangalia kipindi hajafunguka tu,anapingana nasi si mwenzetu ila atuungae u pamoja naye.
 
Nimewahi kumsikia huyu mtu. Hebu jaribu kumwelezea wadau.

Lakini haina haja kama mtu mwenyewe hawezi kuona fursa (0pportunities) hataweza kusaidia chama.
 
Chadema hatununui wala kubembeleza mtu kujiunga na sisi. Kuna chama kinaitwa CM ni hodari wa kufanya hivyo. Waliwanunua ze comedi na Kingwendu bila kumsahau mzee small.
 
Kwa matendo, maneno, etc anaweza akawa rafiki wa cdm kama ilivyo kwa Julius malema na anc youth league yao, au marafiki wa mahakama.
 
... Hamna haja ya kuhamia chadema. Anafaa kuendelea kutumikia watanzania mahali alipo.
 
Rejea maandiko hapo juu, "Yupo makini sana katika kujenga hoja na anajiamini yaani mtu kama huyu na Mnyika,Lissu,na Zitto wakikaa pamoja nadhani CDM itakuwa unstoppable"

Kwani viongozi wakuu wa CDM(Dr.Slaa & Mbowe) sio wajenga hoja na hawajiamini?
 
CDM hawanunui wanasiasa kama timu ya man city, wale wenye moyo wa uzalendo wa kweli na uchungu wa kuikomboa tanzania na dhamira ya dhati hujiunga wenyewe ktk muda na wakati muafaka bila kuchangamkiwa na mtu!

Point mkuu. Na pia sio lazima mtu awe mwanasiasa ndipo atoe mchango kwa taifa lake. Kama anavyoshuhudia mwenyewe mtoa mada, Sungusia anatoa mchango hapo hapo alipo and I like the way it is. Ila kura yake kwenye sanduku la kura ni muhimu sana iende CHADEMA.
 
ni mtu mzuri,ila ni uhuru wake kuwa na chama au laa na sio kumbembeleza kujiunga na cdm.
 
Kweli Sungusia ni mzalendo. Takwimu alizotoa kuhusu idadi ya wananchi wasio na hatia waliouawa na polisi ni ushuhuda kuwa anajua kutunza kumbukumbu. Hamna haja ya kumfuata, yeye mwenyewe anajua CDM ilivyo kiboko.
 
ametangaza kuwa hana chama cha siasa huenda ni wakati muafaka wa kumfuata

Sungusia ni mwanaharakati na ni vyema hawa watu wakendelea kuwepo bila kuwa na chama ili wawe huru kukosoa pindi makosa yanapofanywa na serikali ama vyama. Kuna hatari CDM ikajaza wanaharakati badala y wanasiasa kama alivyowahi kusema mzee wa ajira wa mwiha.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom