CHADEMA bado yalia na ripoti UN

Serayamajimbo

Senior Member
Apr 15, 2009
191
38
na Esther Mbussi


amka2.gif

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ametakiwa kuwashinikiza mawaziri ambao wizara zao zimeguswa katika ripoti ya Umoja wa Mataifa (UN) kujibu au kutoa ufafanuzi kuhusu hoja na tuhuma zilizoibuliwa ndani ya ripoti hiyo.
Ripoti hiyo ni ile ya kundi la wataalam ya UN inayoitaja Tanzania kulisadia silaha kundi la waasi katika ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Taarifa ya Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, ilieleza mawaziri hao wanapaswa kufanya hivyo ili Watanzania kuelewa mjadala ulioanzishwa kuhusiana na ripoti hiyo, kwani tayari Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imeshafanya kosa la kisiasa la kuitumbukiza serikali kwenye malumbano kwa kuliibua suala hili na kuituhumu UN kabla serikali haijafafanua ama kujieleza kwenye kamati ya vikwazo.
“Kwa kuanzia ni muhimu kwa Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi na ile ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa zikatoa maelezo na vielelezo kuhusu suala hili, hivyo mawaziri wanaopaswa kufuatia kutoa kauli ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Hussein Mwinyi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha. “Hii ni kwa sababu siku chache zimebakia kwa serikali kuwasilisha ripoti yake kwa Umoja wa Mataifa wakati mpaka sasa haijawasiliana na wananchi ama walau wawakilishi wa wananchi kupata maoni yao, ili kujenga msimamo wa pamoja kama taifa kuhusu yaliyoibuliwa na ripoti hiyo,” alisema Mnyika. Aidha, alisema CHADEMA inatoa wito kwa UN pia kutafakari masuala yaliyomo kwenye taarifa yao ya awali wakati inapojiandaa kuipitia taarifa ya Serikali ya Tanzania kuhusu ripoti hiyo ambayo serikali kupitia kwa balozi wake wa kudumu kwenye Umoja wa Mataifa, Dk. Mahiga imetangaza kwamba itaiwasilisha Desemba mwaka 2009.
Alisema wanakubaliana na hoja kwamba Serikali ya Tanzania imechafuliwa katika ripoti hiyo kwa baadhi ya viongozi wake, ama raia wake kutajwa kwa namna moja au nyingine na kwamba serikali yenyewe kama taasisi imechafuliwa kwa kuonyesha kwamba haitekelezi kikamilifu maazimio ya Umoja wa Mataifa ambayo ni mwanachama.
Pamoja na mambo mengine pia alisema kosa kubwa la Wizara ya Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa katika sakata hili ni kufikiri kwamba yenyewe ndiyo inayowajibika kulitolea ufafanuzi suala hilo.
“Ikumbukwe kuwa tuhuma za Tanzania kujihusisha na vita vya DRC zilianza toka wakati taifa hili linaasisiwa, tofauti ya watawala wa sasa ni kwamba uongozi wa Nyerere ulikuwa unasema wazi kuwa unasaidia waasi, na UN inajua, Lakini wakati ule walioitwa waasi ni wazalendo waliokuwa wakipambana dhidi ya watawala wa kidikteta ambao walikuwa ni makuwadi wa ubeberu na ukoloni mamboleo katika Afrika.
“Sera ya wakati huo ya mambo ya nje ya Tanzania ilikuwa ni kuleta ukombozi Afrika nzima, serikali ya sasa ipo tofauti kwanza, haina msimamo endelevu pili, sera yake ya mambo ya nje haieleweki.
“Tatu masuala ya sasa ya usafirishaji wa silaha ama utoroshaji wa madini toka maeneo yenye vita ambao yanasemwa kuwa yanafanywa na serikali ama watanzania yanahusu zaidi miradi binafsi ya watu ambayo wanaiendesha kwa ama kuzitumia taasisi za kiserikali au kuruhusu mianya kwa kutowajibika kusimamia utawala wa sheria ikiwemo kuheshimu maazimio ya Umoja wa Mataifa (UN) ambayo nchi yetu imetia saini.” Ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
 
Back
Top Bottom