rosemarie
JF-Expert Member
- Mar 22, 2011
- 6,887
- 3,412
Iwapo Chadema itashindwa uchaguzi Mkuu 2015 maisha yataendela kama kawaida,hakuna kiongozi au Mwanachama yeyote wa Chama atakaye chukua hatua za kujiondoa uhai, Chadema tumeshakubalika na kuaminika kwamba tunaweza kusogeza nchi yetu hapa ilipo na kuipeleka mbele,nilifanya research yangu binafsi hapa Arusha,niliongea na watu 47 kwa week moja na kutaka kujua uwezo wao wa kuelewa nini maana ya Serikali na uongozi wake,niligundua watanzania wengi sasa hivi wanaelewa maana ya Serikali na wajibu wa serikali kwa wananchi wake,swali la mwisho nililowauliza utachagua chama gani iwapo uchaguzi mkuu utaitishwa leo,watu 45 kati ya 47 walisema watachagua chadema,2 walisema hawajui,hakuna hata mmoja aliyesema atachagua ccm.
Hii inaonyesha wazi ni jinsi gani Chadema ilivyofanya kazi kubwa ya kuwaelimisha watanzania kujua haki zao na uwajibikaji wa serikali yao kwa ujumla Kama mwanachama wa kawaida wa Chadema nimeona nitoe maoni yangu hapa JF kwa kuwa viongozi wa Chama na wapenda mabadiliko wenzangu mpo hapa
Nisingependa kusubiri 2015 kuona matokeo yakitangazwa na tume ya uchaguzi ambayo ipo chini ya ccm na kuitangazia ushindi ccm,nini kifanyike ili kwa vyovyote vile uchaguzi 2015 tuwe na uhakika 100% tutaondoka na ushindi wa kishindo?
Chadema ilikuja na kelele za ufisadi na wizi wa raslmali za taifa letu,kelele hizo zilifanya kazi kubwa ya kuwaamsha watanzania waliokuwa wamelala usingizi mzito na kuwafanya kuwa na hasira kali dhidi ya serikali ya ccm, tunakoelekea hizi kelele zitakosa ile nguvu yake ya asili na kubakia kama kelele za kawaida kwa sababu watanzania ni watu wa kusahau haraka na pia kwa jinsi maisha ya mtanzania yalivyo itakuwa ngumu sana kukumbuka yote haya,nini cha kufanya ili hizi kelele zibaki na nguvu yake mpaka november 2015?
Kuna haja ya Chadema kusogea another level???
yes ipo haja sasa kwa sababu tayari Chadema imeshakubalika nchi nzima,na kelele zote za ufisadi na wizi zimesikika kwa wenye nchi yao, je kuna haja ya kuendelea kupiga kelele za ufisadi tena??jibu ni noo!
nasema hivyo kwa sababu ngoma ikilia sana mwisho hupasuka,Chama kwenda another level ni kuchukua hatua na kusonga mbele kuangalia jinsi ya kushawishi wapiga kura wakichague. Chadema inatakiwa kupunguza kelele za ufisadi kwa sababu moja tu!CCM inajipanga upya,nani anajua labda watakuja na safu mpya isiyoshutumiwa??
kama ikiwa hivyo kelele za chadema zitaenda wapi??we need to go another level now! Chadema ikianza sasa hivi kupigia kelele kazi na mabadiliko watakayofanya kwa watanzania,na kuwafundisha watanzania kuhudhuria mikutano yao na kalamu na daftari ili waandike watakachofanya watakapoingia madarakani itakuwa ni another level!
watanzania wakianza kusikiliza na kuandika nini kitafanywa na serikali na sio kunyanyua vidole viwili juu itakuwa ni hatua kubwa kuelekea ukombozi, wingi wa watu kwenye mikutano sio wingi wa kura,kunyanyua vidole viwili juu kama tulivyozoea sio wingi wa kura, Chadema hakuna njia mmbadala zaidi ya kuanza kueleza sera zako na kuzipigia kelele za nguvu hadi watanzania wasikie na kuelimika kwani hiyo ndiyo nguvu pekee ya kushinda hii vita ingekuwa ni rahisi kuondoa CCM madarakani ingeondoka 2010,lakini bado ipo na wanajua walitakiwa watoke wakalazimisha,ni nani anajua kama hawatalazimisha 2015??
Kila la kheri Chadema