SoC03 Chachu ya maendeleo ni Utawala Bora

Stories of Change - 2023 Competition

Joel Hamis Spea

New Member
Jul 29, 2023
1
3
Kila kukicha tunasikia neno Utawala bora, na ni ndoto ya kila taifa kutamani kuwa na utawala bora. Lakini ndoto hiyo imebakia kuwa kama ndoto ya mchana kutokana na ubadhilifu unaofanywa na viongozi walioko madarakani. Hivyo basi, wananchi hukosa imani na viongozi wanaowachagua kila iitwapo leo, mbali na kuwa huakikishiwa kuwa wataletewa utawala bora na siyo bora utawala. Swali hubaki kwa wananchi kwa kujiuliza je! Nini maana ya utawala bora?

Utawala bora
ni dhana inayoelezea namna serikali au mamlaka inayopaswa kushika hatamu na kusimamia nchi au jamii kwa njia ambayo inahakikisha uwazi, uwajibikaji, ushirikishwaji, haki za binadamu, pamoja na demokrasia. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake ya mara kwa mara ibara ya 129 (1) inatambua uwepo wa utawala bora katika jamii ili kuwezesha upatikanaji wa haki za binadamu nchini.

Katika jamii ya sasa uwepo wa utawala bora imekuwa kama ndoto ya mchana, kwani viongozi wanaoshika hatamu huingia kwa maslahi yao binafsi na siyo kwa maslahi ya wananchi. Na hivyo hugeuza dhana ya utawala bora na kuwa bora utawala. Hii ni kutokana na kushindwa kutekeleza ahadi zao kwa wananchi jambo ambalo limepelekea jamii kuwa na bora kiongozi na siyo kuchagua kiongozi bora.

Hali kadhalika, katika kuhakikisha utawala bora nchini kuna mambo kadha wa kadha ambayo yanapaswa kuzingatiwa ili kuchochea utawala bora kwa viongozi walioko madarakani hasa katika suala zima la kuitumikia jamii:

Kuwepo na uwazi na uwajibikaji wa viongozi katika jamii. Jamii inapaswa kuwa na ufahamu wa kutosha juu ya maamuzi na hatua za serikali katika masuala yote ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi ili wananchi waelewe kinachoendelea katika serikali yao.

Kwa mfano, uwazi katika mapato na matumizi ya serkali, uwazi katika upatikanaji na utolewaji wa habari. Pia, utawala bora utahimiza uwajibikaji katika kusimamia rasilimali za umma kama rasilimali watu, fedha, habari, muda, pamoja na rasimali vitu. Sanjari na hilo, pia viongozi wanapaswa kuwajibika kwa hali na mali ili kuhakikisha wananchi wanapata maslahi yao husani katika suala zima la maendeleo.

Kuwepo na ushirikishwaji wa wananchi. Sauti ya wananchi inanguvu katika kuchochea utawala bora nchini hususani katika michakato ya kidemokrasia. Kwa mfano, ibara ya 21 (1) pia inachochea kuhusu ushirikishwaji wa wananchi katika hatua mbalimbali kama mchakato wa katiba ya nchi, pamoja na mchakato wa bajeti ya serikali. Lengo na madhumuni ni kuchochea utawala bora ili kuhakikisha viongozi wanatetea maslahi ya wananchi na siyo maslahi yao binafsi.

Taifa lenye utawala bora lazima lijali haki za binadamu. Kwa mfano, haki za kisiasa na kiraia zinapaswa kuheshimiwa na kulindwa kwa hali na mali, uhuru wa kushirikiana, pamoja na uhuru wa kujieleza. Sambamba na hilo, pia, mwananchi anatakiwa kuhakikishiwa uhuru wa kujieleza, yaani kabla na baada ya kujieleza. Utawala bora ndiyo utakochochea haki za binadamu nchini, kwani kuna baadhi ya matukio yanayotokea ila hufumbiwa macho na tabaka tawala. Na hiyo yote ni kutokana na kukosekana kwa utawala bora utakaoweza kuondoa dosari zote zinazokiuka haki za msingi za wananchi.

Utawala bora husimama kidete kupambana na matukio ya rushwa, ufisadi, na upendeleo. Matukio mengi ya ufujaji wa mali za umma hutokea pale tu panapokosekana utawala bora wa kusimamia mali za umma, kwani viongozi wasiyo na maadili ya utumishi wa umma ndiyo wanaoongoza kwa kesi nyingi za ufisadi.

Kwa mfano, mwaka 2008, 2014, na 2018 kesi nyingi za ufisadi zilisikika masikioni pa watu lakini cha ajabu viongozi hao hao waliojishughulisha na vitendo vya ufisadi wala wahakuchukuliwa hatua zozote za kisheria na serikali. Hilo ni kosa la serikali kushindwa kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria za nchi. Hii ni sababu kukosa utawala bora ambao utazioenea uchungu mali za umma, na kuhimiza zitumike kwa maslahi ya wananchi wote na siyo kwa maslahi ya watu wachache.

Sambamba na hilo, pia, ripoti nyingi za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) huwa zinaonesha matendo ya ufisadi na rushwa, pamoja na ufujaji wa mali za umma, lakini hawachukuliwi hatua zozote. Hiyo inaonyesha wazi kuwa tuna bora utawala na siyo utawala bora. Hivyo, kuna ulazima wa kuwa na utawala bora utakaopambana na dalili zote zinazoashiria ufisadi.

Utawala bora huchochea maendeleo endelevu. Taifa lenye utawala bora hujali maendeleo ya muda mrefu na ustawi wa vizazi vijavyo kwa kuweka mikakati endelevu yenye tija kwa wanachi wake na siyo kwa familia zao.

Kwa mfano, suala la uchumi unaojali mazingira na jamii kiujumla, pamoja na kuboresha huduma za msingi kama miundombinu endelevu, pamoja na fursa za kiuchumi.

Kuwepo kwa utawala wa sheria. Katiba za nchi zote duniani zinatambua umuhimu wa kufuata sheria za nchi, na zote zinasisitiza kuwa hakuna mtu wa aina yeyote aliyeko juu ya sheria. Pia, inatambulika wazi kuwa sheria ni msumeno, hivyo, viongozi wanapaswa kutii sheria za nchi ili kuhakikisha kuwa wawanchi wanapata maslahi yao.

Kwa mfano, kiongozi mkubwa akifanya kosa, kosa lake litafumbiwa macho kana kwamba halionekani. Lakini kwa mtu wa tabaka la chini, hupoteza haki zake na kuozea jela. Siyo tu kuozea jela, bali kuna uwezekano mkubwa wa kupoteza haki zake za msingi zikiwemo na mali zake. Pia, kukosekana kwa utawala bora hupelekea kuwepo kwa upendeleo wa chama tawala mpaka kwenye vyombo vya dola.

Kuwepo kwa haki na usawa nchini. Utawala bora ndiyo kichocheo pekee cha kuhakikisha haki za binadamu na usawa kwa kila mwananchi hususani kuondoa ubaguzi, udhalilishaji, pamoja na ubaguzi wa kijinsia. Pia, wananchi wanapaswa kuwa na fursa sawa ya kupata huduma za msingi kama vile huduma za afya, elimu, ajira, na makazi.

Mfano mzuri, Tume ya Haki na Utawala bora sheria ya 2000 na. 3 ib 17 inafafanua haki zote za msingi ambazo mwananchi anapaswa kuzipata bila ya ubaguzi wa aina yeyote. Lengo na madhumuni ya kuanzishwa kwa sheria hiyo ni kuleta usawa katika jamii.

Hivyo basi, maendeleo ya taifa hutokana na utawala bora wenye sera bora za kulijenga taifa kwa kuimarisha uchumi wa nchi na jamii kiujumla, sambamba na kuchochea na ushirikishwaji wa vijana, uwazi na uwajibikaji wa viongozi walioko madarakani. Pia, ili kuhakikisha tunapata viongozi bora na wenye maadili ni vyema wakaandaliwa mapema kwa kufundishwa maadili ya uongozi ili kuondokana na kasumba za rushwa, ubaguzi, upendeleo, ufisadi, na utovu wa kutofuata sheria za nchi.​
 
Kalamu ni Sauti ya muandishi, maandishi kama haya ndio uponyaji kwa wasomaji. 💐
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom