CHA KUJIFUNZA KUHUSU UONGOZI KUPITIA IMANI

SHADOWANGEL

JF-Expert Member
Sep 15, 2014
528
348
Ikumbukwe kuwa kila mwanadamu ana kile ambacho anakiamini na anaweza kuelezea jambo kwa kile ambacho anakiamini.


Katika kuelezea vile ambavyo naamini jinsi navyoelewa kuhusu uongozi kwa dini nayoamini ningependa kuanza kwa kunukuu matendo ya mitume 27:10 “Waheshimiwa, nahisi kwamba safari hii itakuwa ya shida na hasara nyingi si kwa shehena na meli tu, bali pia kwa maisha yetu. 11 Lakini yule ofisa alivutiwa zaidi na maoni ya nahodha na ya mwenye meli kuliko yale aliyosema Paulo. 12 Kwa kuwa bandari hiyo haikuwa mahali pazuri pa kukaa wakati wa baridi, wengi walipendelea kuendelea na safari, ikiwezekana mpaka Foinike. Foinike ni bandari ya Krete inayoelekea kusini-magharibi na kaskazini-magharibi; na huko wangeweza kukaa wakati wa baridi.” Mara nyingi viongozi wa dunia wamekuwa wakipenda kufanya yale wanayopenda kusikia na kusahau pasipo jamii iyo ambayo wanaiongoza akuna MTU YOYOTE KATI YAO ATAKAYEITWA KIONGOZI.


METHALI 14:20.. inasema “Fahari ya mfalme ni wingi wa watu wake,lakini bila watu mtawala huangamia.” Bado biblia katika huo mstari inaonyesha kuwa bila kuwepo watu akuna mtu ambaye anayeza kuitwa kiongozi katika jamii ya watu. Katika Kuonyesha umiumu wa watu METHALI 14:34: inasema “Uadilifu hukuza taifa,lakini dhambi ni balaa kwa taifa lolote.” Apa inaonyesha katika kuongoza taifa lolote unaitaji uadilifu wao.


Kumekuwa na kila namna ambayo watu uongoza wenzao kwa namna wanavyoona wao kila wapatapo nafasi katika jamii ya watu ila BIBLIA katika METHALI 15:22 inasema “Mipango huharibika kwa kukosa shauri, lakini kwa washauri wengi, hufaulu.” Apa pia biblia inatonyesha umuimu wa kushilikiana na wale ambao unawaongoza ili upate kufikia malengo yako katika uongozi. Ukirudi katika MITHALI 15:12 inasema “Mwenye madharau hapendi kuonywa, hatafuti kamwe maoni ya wenye busara.” Na 15:10 inasema “Adhabu kali ipo kwa wanaoacha mwenendo mwema; yeyote achukiaye kuonywa atakufa.”


Katika Samueli wa 2:17 tunaona alivyokataa kusikiliza ushauli na ilivyomgalimu katika utawala wake wote. BiBLIA katika Wafalme wa 1: 12 inasema

12 Basi, siku ya tatu Yeroboamu pamoja na watu wote wakarudi kwa Rehoboamu kama alivyokuwa amewaagiza. 13Mfalme akawajibu watu hao kwa ukali, akapuuza shauri alilopewa na wazee, 14akafuata shauri la vijana wenzake, akawaambia, “Baba yangu aliwatwika mzigo mzito, lakini mimi nitaufanya kuwa mzito zaidi. Baba yangu aliwapiga kwa mijeledi, lakini mimi nitawapiga kwa mijeledi yenye miiba.”

15 Hivyo, mfalme hakuwajali watu kwa sababu jambo hili lilisababishwa na Mwenyezi-Mungu, ili atimize neno lake alilomwambia Yeroboamu mwana wa Nebati, kwa njia ya Ahiya wa Shilo.



Biblia Pia inatuonyesha viongozi wazuri kama NEHEMIA katika mithali 16:10 inasema “Uamuzi ulioongozwa na roho unapaswa kuwa katika midomo ya mfalme;+ kinywa chake hakipasi kukosa uaminifu katika hukumu”
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom