CEO wa HITS-Tanzania abwaga manyanga!

Oloronyo

Member
Mar 29, 2009
80
9
Habari za uhakika nilizozipata ni kuwa yule aliyekuwa Mkurugenzi mtendaji wa HITS-TANZANIA Bw.Gerhard May (Pichani)ame-resign siku ya Alhamisi,Wakati huo kukiwa na tetesi kampuni ya Huawei Technologies iliyopewa tenda ya kujenga miundo mbinu ya Hits kusimamishwa kazi hiyo huku kukiwa kuna kila dalili ya kampuni hiyo ya simu kuchukuliwa na Orange ambayo imeshachukua mtandao wa Hits wa nchini Uganda.

Chanzo hicho cha habari kilidai kuwa kuna kila dalili ya yale yaliyotokea enzi za TRITEL kujirudia, kwani kabla ya ya kampuni ya TRITEL kutangaza kufilisika uongozi wa juu wa TRITEL ulihama nyumba walizokuwa wanapanga na kuhamia hotelini kabla ya kutokomea! Kwa sasa Bw.Chris Keeping Mkuu wa kitengo cha biashara cha kampuni hiyo ndiye anayekaimu nafasi yake kiliongezea chanzo hicho.

4050d1238339796-ceo-wa-hits-tanzania-abwaga-manyanga-gerhard-may.jpg
 

Attachments

  • Gerhard May.jpg
    Gerhard May.jpg
    6.6 KB · Views: 418
Mbona wameshaanza kutest mitambo yao kwa kutumia Code 074...?????? Nadhani mambo yao yapo Mswano! Vipi wadau wa Hits ya kweli haya???
 
Yah,

hata mimi habari za kilabuni zilisema kwamba jamaa wako fit na wanaanza mambos very soon

Tanzania ni zaidi ya uijuavyo; kila siku na mambo mapya.
 
:mad:
Yah,

hata mimi habari za kilabuni zilisema kwamba jamaa wako fit na wanaanza mambos very soon

Tanzania ni zaidi ya uijuavyo; kila siku na mambo mapya.

MTM, Ni kweli jamaa wanatest mitambo lakini uzoefu wetu wa Kampuni ya GREENLAND,TRITEL,KIBO BREWERIES na sasa GTV. Wafanyakazi wa Hits wawe tayari kwa kilichowakuta wafanyakazi wa kampuni nilizozitaja awali na na tetesi ni kuwa Bw.Chris Keeping akienda kula Easter kwao ndio wakati kutakuwa na mabadiliko hayo. SHIME wafanyakazi wa Hits jiandaeni kabla ya hatari hebu wasilianeni na mtu wa legal wa TCRA muulize kabla ya kugeuka mbuzi wa kafara.
Ndimi
Oloronyo Saiguran.
 
Orange wachukue haraka ili wa tz wenzetu wasipoteze hakina ajira zao maana msala mkubwa jamaa wamechukua toka sehem mbl mbl kwa ahadi mshaara 70% zaidi unachopata....wamepata watu wazuri sana kibaoooo....
 
Ni Kweli Orange imeshanunua HITS huko Uganda na hivi sasa wale wa Bongo wako katika majadiliano na wawekezaji wa kuwaongeza nguvu. Tusubiri kuona matokeo. Pia ni kweli kwamba Chris Keeping amekuwa akicheza nafasi kubwa sana katika hili.
 
Hii habari ya lini, kwani nna jamaa kibao wanaofanya kazi hapo wana mtandao wa HITS unaoanzia na namba 0742?
 
Hii habari ya lini, kwani nna jamaa kibao wanaofanya kazi hapo wana mtandao wa HITS unaoanzia na namba 0742?

Mundu, hawa jamaa kupewa namba sio guarantee kwamba HITS is here to stay; all the experience from other companies inaonyesha otherwise. Cha maana ni kuanza kujipanga na kuombea mema... NI HERI UAMINI MUNGU YUPO USIMKUTE KULIKO KUAMINI HAYUPO HALAFU UKAMKUTA
 
Mundu, hawa jamaa kupewa namba sio guarantee kwamba HITS is here to stay; all the experience from other companies inaonyesha otherwise. Cha maana ni kuanza kujipanga na kuombea mema... NI HERI UAMINI MUNGU YUPO USIMKUTE KULIKO KUAMINI HAYUPO HALAFU UKAMKUTA

MTM nakuunga mkono!! Hali kama hii ilishawahi kutokea pia katika mahoteli yetu mfano Sheraton Dar es Salaam... mwaka 2001, Shareholders waliwaondoa ITT Sheraton na kuleta kampuni nyingine. iliyokuwa inaitwa ROYAL PALM... Wafanyakazi wazalendo walibaki na vyeo/wajibu/vibarua vyao!! Lakini ile cream ya experts wa ITT Sheraton iliondoka...
 
Erooo Wana JF,Mustakabali wa wafanyakazi wa HiTS ni leo tarehe 16.06.2009. Kuna tetesi kuna Bwana mmoja aliyekuwa ughaibuni amekuja na siri moyoni kama alivyokuja Kawawa enzi za msiba wa Mwl. JK Nyerere. Maombi na sala vielekezwe kwa wafanyakazi wote wa HiTS.

Duru za habari zilizokuwa Airport zinadai jamaa huyo hajatinga Dar na kupelekea wasiwasi kuwa jamaa huyo nae amekula kona kama wenzake kina Gerhard May na Chris Keeping!
 
Oloronyo,

Kuna tetesi kuwa family ya Mzee Mwinyi ipo katika umiliki wa HiTS Tanzania, ni kweli mkuu?
 
Vyote ni kazi ya tume kujua kuwa hizi kampani haziwezi kufa hata siku moja maana huwa zinarudhisha nyuma sana
 
Wazee waJF DT DOBIE wapo HiTS wakichukua magari aina ya Nissan Patrol pamoja na Hardbody yaliyochukuliwa kwa mkopo nitawajuza zaidi.
 
Barua za kusitisha mikataba ya ajira zimesambazwa jioni hii. Hali kwa ujumla inasikitisha sana.
 
Duru zinazidi kutujuza kuwa mkuu wa uendeshaji Bw.Theuns ameanza likizo huku akiwa na uso wa mbuzi, Theuns ndiye alikuwa kiongozi wa ngazi Juu aliyebakia HiTS na inawezekana akawa amekata mbuga kama wenzake wa awali. nitawajuza.
 
Back
Top Bottom