CCM yamfukuza mwanachama wake

Tina

JF-Expert Member
Jul 9, 2007
572
579
Mjumbe wa kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Unyamikumbi, katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida amefukuzwa uanachama kwa madai kwamba alikuwa akifanya kampeni za kuvisaidia vyama vya siasa kambi ya upinzani kupata ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Okt, 25, mwaka huu.

Hatua ya mjumbe huyo wa kamati ya siasa, Zakaria Mkuki kufukuzwa imekuja siku chache tu baada ya kugombea kwake nafasi mbili ikiwemo nafasi yaw mwenyekiti wa Kijiji cha Kisaki pamoja na ujumbe,nafasi ambazo hakufanikiwa kuzipata.

Hata hivyo inasemekana kuwa baada yaw mwanachama huyo kukosa nafasi hizo kwenye kura za maoni za uchaguzi huo ndipo Mkuki alipoanza kufanya kampeni za chini chini za kutaka wagombea wa vyama vya upinzani katika nafasi mbalimbali walizoomba wanakibwaga chama cha mapinduzi.

Habari za uhakika kutoka katika Kijiji cha Kisaki,kilicho umbali wa takribani kilomita kumi kutoka mjini singida zinasema kwamba mjumbe huyo alifukuzwa na mwenyekiti wa CCM wa Kata ya Unyamikumbi, Jakobo Lamba kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Ng’aida wakati wa kampeni za chama hicho.

Kwa mujibu wa habari hizo ambazo zimethibitishwa pia na mjumbe mmoja kutoka katika Kata hiyo ambaye si msemaji wa chama zinasema kuwa baada ya Mwenyekiti kubaini mchezo huo mchafu wa mjumbe wake dhidi ya vyama vya upinzani, ndipo aliamua kumfukuza uanachama kwenye mkutano huo wa hadhara.

Kwa mujibu wa mtoa habari huyo katika majibizano baina ya mwenyekiti na mjumbe huyo,huku mwenyekiti akitaka mjumbe kurudisha kadi ya CCM, lakini mjumbe Mkuki alikataa kata kata mbele ya mkutano huo kwa madai kuwa kadi aliyonayo ni mali yake kwani aliinunua kwa fedha zake mwenyewe.

Hata hivyo kutokana na sakata hilo uongozi wa ngazi ya juu katika kata hiyo unatarajia kukutana kabla ya uchaguzi huo wa serikali za mitaa ili kutoa tamko rasmi kuhusu sakata hilo .

Habari zaidi kutoka katika Kijiji hicho cha Kisaki zinasema kuwa huenda viongozi wa chama watakaokutana wakaamua kumfuta uanachama mjumbe huyo ili kujenge nidhamu ndani ya chama hicho kabla ya kuelekea katika uchaguzi mkuu wa viongozi hapo baadae mwakani.

Sakata hilo limekuja siku chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini kote siku ya Oktoba 25 mwaka huu, kwa kuchaguliwa viongozi katika ngazi za mitaa, vitongoji na vijiji.

Hivi karibuni Katibu wa CCM Mkoa wa Singida,Bi Naomi Kapambala alidai kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Singida tayari kimeibuka na ushindi kwa zaidi ya asilimia 62 kati ya vijiji 415 vya mkoa wa Singida wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kupitia tiketi ya CCM wamepita bila kupingwa kwenye jumla ya vijiji 261.
 
teh teh huyu naye kwa nini hakuomba msamaha kama spika 6?wangemsamehe tu si mwenzao wametoka naye mbali
 
Je ni kikao gani kilifanyika na kumvua uanachama? Je mwenyekiti wa chama wa kijiji au wilaya anaweza kumvua mtu uanachama bila kufanyika kikao cha chama mtuhumiwa ajieleze?
 
Je ni kikao gani kilifanyika na kumvua uanachama? Je mwenyekiti wa chama wa kijiji au wilaya anaweza kumvua mtu uanachama bila kufanyika kikao cha chama mtuhumiwa ajieleze?
Rev.
Kwa CCM ya leo lolote linawezekana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom