CCM Wameishika CHADEMA PABAYA...

"The only time a politician tells the truth is when they call another one a liar."
 
it is clear that biashara ya watu kukabidhiwa kadi za CCM huwa ni mamluki yaana wenyewe kwa wenyewe na huwa local CCM leaders wanawadanganya viongozi wao wa kitaifa....hii imetokea sehemu nyingi tu.
 
Na Ghati Msamba, Bunda
Gazeti la Uhuru

Hili si tulisha li RIP? limefufuka?:pound:

Halafu hii sekretarieti ya CCM vipi? Shurti wajumbe wakajitambulishe kwao? Chiligati alikuwa Singida huyu nae Mara? Mcheza kwao nini? Walahi wangeanzia kusikokuwa kwao wangeambulia miangwi!!
 
hawa ccm humu kwenye jf wanafanya nini mi naona wanaleta kichefuchefu tu. akina nape, mwakyembe, sita wote wamedhihirika ni wasaliti kwa ccm, mafisadi mmewashindwa kuwaondoa, magamba yamewazidi halafu eti mnafiki anasema cdm imeshikwa pabaya. hivi hata uwezo wa kujipambanua hamna nyie ccm .......anguko lenu lipo karibu sana
 
Imekuwaje tena?? Nafikiri Nape alisema wanampango wa kuacha wanachama wa papo kwa papo? sasa hawa 239 wamepata mafunzo wapi? isije ikawa ni mamluki kama alivo waita? Kweli sasa hivi CCM wamebanwa pabaya sana. CDM kaza buti CCM wamechanganyikiwa.
 
Mwili mkubwa akili kidogo. Nilidhani dr. Slaa. Kashikwa na mabilioni ya EPA. Kumbe umbeya!! Kazi kweli kweli!!
 
Niliposoma chanzo tu kuwa ni gazeti la uhuru sijaendelea zaidi maana ndani kilichoandikwa nnajua ni prop....,,
 
Nimekuwa nifukifuatuatilia hoja zinazotolewa na wapenzi wa Chama cha Magamba juu ya ufisadi wa Dr Slaa,Mbowe na Ndesa pesa nikagundua kuwa kweli mtu anapoishiwa hoja ni sawa na gari bovu linapokosa break linakwenda popote. Kwani hata kutunga uwongo unaofanana na ukweli ni tatizo kwa sababu breki hamna. Fikiria Ndesamburo jinsi anavyojitoa kuwasaidia watu wa jimbo lake na jinsi alivyosaidia CHADEMA kwa hali na mali tena kwa uwazi na biashara zake ni za uwazi, Angalia Mbowe jinsi anavyojitoa kwa hali na mali kukisaidia chama chake na wananchi kwa ujumla na biashara zake zote ni za uwazi tofauti na wafanyabiashara wa chama cha magamba wanaotoa michango kwa kificho na hata hiyo wanayosema ameuzia chama magari yaliotumika ni kitu kimejadiliwa kwenye vikao na kuwekwa wazi. Tazama mtu kama Dr Slaa alivyojitoa kwa hali na mali kuwapa watanzania elimu ya uraiya na hata kuahatarisha maisha yake, mtazame Zitto kazi aliyoifanya juzi juzi hapa eti hawa ni mafisadi kama ndiyo hivyo basi mimi natangaza ufisadi wa CHADEMA tunauhitaji kabisa na waendelee kuwa na ufisadi huo.

Watanzania sii wapumbavu kiasi hicho cha watu kufikiri kuwa uanaweza kuwadanganya kama kuwa hawaoni wala hawatambui kinachofanyika. Ni dhambi kubwa chama CCM kinafanya kuwaona wa TZ hawawezi kutambua ni nani fisadi na nani mzalendo. Hivi ninyi ndugu zangu hamumuogopi hata Mungu kwa uovu mnaowafanyia wa TZ waliopewa nchi yenye utajiri mkubwa kiasi hicho mkawafanya masikini kiasi hicho. Jamani maisha yetu ya kuishi hapa Dunia ni mafupi ni miaka sabini ukiwa na nguvu miaka 80 sasa yanini kuhangaikia mambo ya rushwa, wizi na kupenda madaraka nasema malipo ya mwovu huanzia hapa hapa Duniani na wengine wenu mmeshaanza kulipwa. Hivi kunaraha gani ya wewe kusomesha nje mtoto wako kwa fedha za rushwa ili hali kuna mtoto wa masikini licha ya kwenda shule hana uhakiaka wa kula.Mshahara wa Dhambi ni mauti wanyonge wanalia na Kitabu cha Mungu kinasema kilio cha mnyonge kinamfikia Mungu moja kwa moja na washauri mbadilike na kuacha uongozi wa nchi hii kwa wengine bila hivyo huko tuendako mtakuja ona hasira ya Mungu.
 
Monday, 16 May 2011

* Akomba wanachama wake 239
* Chiligati: Mamluki CCM kudhibitiwa


Na Ghati Msamba, Bunda
Gazeti la Uhuru


KIMBUNGA cha Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, kimeitikisa CHADEMA, ambapo ngome yake imepata nyufa. Ngome ya CHADEMA imepata nyufa baada ya wanachama 239 kuihama na kujiunga na CCM, huku wakiponda kauli za kejeli na kuvuruga amani zinazotolewa na viongozi wa chama hicho.


Wanachama hao wapya wa CCM wamesema wameridhishwa na kasi ya maendeleo na utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kuondoa kero za wananchi. Mukama akiwa katika siku ya kwanza ya ziara wilayani Bunda, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kata ya Kibara, wananchi hao walitangaza kujiengua CHADEMA na kujiunga na CCM. Katika mkutano huo, Mukama alisema CCM ndicho Chama pekee kinachoweza kusimamia rasilimali na kubadilisha maisha ya wananchi. Aliwaasa Watanzania kutokubali kurubuniwa na kuwasikiliza watu wanaopotosha ukweli kuhusu dhana ya CCM kujivua gamba kwa kuwatosa watuhumiwa wa ufisadi.

Katibu Mkuu alisema CCM ni taasisi kubwa, hivyo haiwezi kufa kirahisi kama wanavyoota wapinzani, hususan CHADEMA kwa kuwa ina viongozi wenye maadili ya uongozi. “Miaka 34 ya CCM ni mingi, hivyo ni lazima viongozi wabadilike na ndiyo dhana ya kujivua gamba ili kuleta mageuzi, kwani kwa kufanya hivyo ni kuonyesha ukomavu na umakini,” alisema.

Alitumia fursa hiyo kuwataka wakuu wa wilaya mkoani Mara kusimamia kikamilifu fedha za miradi ya maendeleo ya wananchi zinazotengwa na serikali kwa halmashauri.

Katika mkutano huo, wazee wa Bunda wakiwakilishwa na Raphael Gurinja, walimuomba Mukama kurudi wilayani humo ili kusafisha siasa chafu na sumu iliyoenezwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa. Alisema Dk. Slaa amekuwa akieneza siasa chafu zenye mwelekeo wa kuvuruga amani nchini, hivyo kumuomba Mukama amfundishe siasa.

“Dk. Slaa anaeneza chuki wakati wenzake wanamwaga sera, sasa inabidi afundishwe jinsi ya kuhubiri sera na si siasa chafu,” alisema Gurinja. Akikabidhi kadi kwa wanachama wapya, Mukama alisema wamechukua uamuzi sahihi kurejea CCM, kwani vyama vya upinzani havina sera. “Nawapongeza kwa uamuzi wa kujiunga na CCM. Kitendo hiki kimewaziba midomo wale wanaodai eti Chama hiki kinakufa, karibuni nyumbani,” alisema.


Mukama pia alikabidhi kadi kwa wanachama wapya 175 wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na kuwataka kuimarisha jumuia hiyo kikamilifu.

Katibu Mkuu Mukama yuko katika ziara ya siku nane mkoani Mara, ambapo pamoja na mambo mengine atahimiza uhai wa Chama. Mamluki CCM kudhibitiwa CCM imesema itahifadhi majina na kumbukumbu za wanachama wake nchini kwa kutumia mfumo wa kompyuta.

Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mageuzi ndani ya Chama, ambapo imewaagiza makatibu kukusanya kumbukumbu kutoka kwenye matawi na kuzipeleka makao makuu ya CCM, mjini Dodoma, ambako zitahifadhiwa. Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), John Chiligati, alisema hayo wakati akihitimisha ziara ya wajumbe wa sekretarieti mpya ya CCM.

Alisema utaratibu huo unatakiwa kukamilika kabla ya uchaguzi mkuu wa CCM na jumuia zake utakaofanyika mwakani. Chiligati ametoa miezi mitatu kwa makatibu kuwa wamewasilisha kumbukumbu na majina ya wanachama makao makuu kwenye Kitengo cha Oganaizesheni kinachosimamia uratibu wa masuala ya uchaguzi, uhai wa Chama na jumuia zake.

Alisema makatibu watapeleka wanachama hai kwa kulipa ada na wale ambao hawajalipa watatakiwa kutuma makao makuu kila yanapotokea mabadiliko, yakiwemo ya wanachama wapya, wanaoacha uanachama au kufariki dunia. Chiligati alisema utaratibu huo unalenga kukomesha uwepo wa wanachama mamluki na wa msimu wa uchaguzi, ambao hawana faida kwa uhai wa Chama.


Ziara ya wajumbe wa sekretarieti ya CCM iliyofanyika kwa siku sita katika maeneo mbalimbali mkoani Singida, iliwahusisha Chiligati, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Mwingulu Nchemba na Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Asha Juma Abdallah.


Source gazeti la uhuru.Mnatoa nakala ngapi kwa siku?coverage yenu ya mauzo ikoje?

Tumeshawazoea wasanii, ninyi any way watu wa leo hawaambiwi tazama.
 
Niliposoma Title nilipata picha tofauti na kille kilchoma. Hebu rekebisha Mkuu
 
mkuu nilianza kutishika na tittle yako,kumbe tupo pamoja sana. usijali,kuna watu huwa wanatoa comments zao bila kusoma ujumbe so kuna uwezekano ukakutana na makombora. mana hawa wandugu si mafisadi kivile,title umeikosea.
 
Mtaongea mengi ila nawaambieni ccm imekufa siku nyingi ila inasindikizwa na nguvu za dola tu hamna kipya hapo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom