CCM walazimisha wanafunzi Sangu Sekondari washiriki maandamano Mbeya, wao wapinga

kapotolo

JF-Expert Member
Sep 19, 2010
3,727
2,214
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wazazi ya Sangu ilyoko Mbeya wamelalamikia CCM kuwalazimisha kushiriki kwenye maandamano yao yatakayofanyika leo huko Mbeya.

Chanzo: Nipashe.

CCM nawashauri muwaache wananchi washiriki kwenye maandamano kwa hiari yao kwama kweli wanaguswa na hicho mnachotaka kuwaambia. Kama hamna jipya acheni kusumbua watu na muaache watoto wasome. wanafunzi wenyewe mmewanyima waalimu acheni watumie muda mwingi kujisomea wenyewe.

Nape usije hapa kutudanganya kwamba mnaungwa mkono wakati mnalazimisha watu kuandamana, aibu!
 
ASANTE EEH MUNGU BABA KWAKUWA UMESIKIA KILIO DHIDI YA KIFO CHAMA CHA MAGAMBA KWA KUTUMIA VIJANA WA KIZAZI WAZALENDO Amen.
 
lakini Sangu si shule ya jumuiya ya wazazi wa CCM au? Nafkiri wanahisi na wanafunzi ni mali ya ccm pia maana hawa magamba nowadays sijui wanafikiri kwa kutumia vichwa vipi, yaani ni kuforce force mambo tu cha muhimu wananchi tuwakatae waziwazi na kwa nguvu tuwambie tumechoka. Huko vijijini wananchi wanalazimishwa kuhudhuria mikutano ya ccm na kinyume chake watendaji wa vijiji huwatoza fine
 
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wazazi ya Sangu ilyoko Mbeya wamelalamikia CCM kuwalazimisha kushiriki kwenye maandamano yao yatakayofanyika leo huko Mbeya.Chanzo: Nipashe.CCM nawashauri muwaache wananchi washiriki kwenye maandamano kwa hiari yao kwama kweli wanaguswa na hicho mnachotaka kuwaambia. Kama hamna jipya acheni kusumbua watu na muaache watoto wasome. wanafunzi wenyewe mmewanyima waalimu acheni watumie muda mwingi kujisomea wenyewe. Nape usije hapa kutudanganya kwamba mnaungwa mkono wakati mnalazimisha watu kuandamana, aibu!
ni pamoja na wale wa Meta sek.
 
dah! Nimekumbuka kipindi cha kampeni za jeikei 2005 wanafunzi wote wa shule za wazazi mbeya tulilazimishwa kwenda sokoine kuujaza uwanja...
 
Hii kitu ya kulazimishwa maandamo ni vitu vilivyonifanya niichukie saaaana tena saaana CCM toka nikiwa darasa la pili. Mnachukuliwa shule nzima na bendi saa tatu mnaandama km kilomita nane hadi kumi mnaingia uwanjani saa nne labda mnapigwa na jua hadi saa nane, mnaa njaa hakuna cha kula wala maji kwenye chupa enzi zile. Na wakakti ule hakuna mzazi alikuwa anampa mtoto wake pesa mkononi so mnashida na njaa, huyo mgeni rasmi anakuja saa nane mchana anahutubia mpaka saa kumi anaondoka na gari, nyie saas ndo mnarudi home na miguu, kwa kweli ile nikama CHILD Labour! nilikuwa nayachukia sana haya mambo na kuomba mungu siku utawala wa CCM ufike kikomo, CCM mlitutesa sana!! Msikubali kataeni huo utumwa!
 
wanafunzi hao nawapongeza sana. wamefanya jambo zuri. ccm ikataliwe kuanzia na mtoto mdogo wa nursery hadi wazee mijini na vjjini
 
Majengo ndiyo mali ya ccm lakini walimu,wanafunzi na wafanyakazi ni mali ya taifa lenye kulilia ukombozi kutoka kwa magamba.amakweli nepi imechanika na haifai kabisa itupeni.hao magamba mbona hawaendi arusha na kilimanjaro?
 
Kweli CCM imekosa mvuto mbele ya jamii..hahahaaa mtaendelea kulazimisha sana watu wawapende lakini mkumbuke mtanzania wa wa sasa sio wale wa miaka ya 47 nyuma, ambao wlalikuwa wakilazimishwa kujifunza na kuitikia kwa salamu ya kidumu chama tawala bila wao kujijua nao wanajibu hivyo huku wakiwaibia...leo hii hata ukimuliza mtoto mdogo Dr Slaa ni nani atakuambia ni raisi makini ajaye siku si nyingi..wanafunzi kama vipi jitokezeni huku mkiimba peoples pooooooooowweeeeeeeeeeeerrrrr..................
 
Wamesahau yaliyotokea mwaka jana kule Kigoma, watoto waliandamana siku iliyofuata baada ya kudanganywa kwenda kushiriki sherehe za kuzima mwenge halafu wangelipwa elfu tano tano!? Ccm hawana watu wa kuandamana nao, wanachofanya ni kutafuta wakuwahonga kwa kofia, tshirt au hela ili waonekane wana watu. Sasa wana walazimisha wanafunzi! Aibu tupu!
 
lakini Sangu si shule ya jumuiya ya wazazi wa CCM au? Nafkiri wanahisi na wanafunzi ni mali ya ccm pia maana hawa magamba nowadays sijui wanafikiri kwa kutumia vichwa vipi, yaani ni kuforce force mambo tu cha muhimu wananchi tuwakatae waziwazi na kwa nguvu tuwambie tumechoka. Huko vijijini wananchi wanalazimishwa kuhudhuria mikutano ya ccm na kinyume chake watendaji wa vijiji huwatoza fine
Obsolete systems and thinkings of CCMs will never work in this era.
 
dah! Nimekumbuka kipindi cha kampeni za jeikei 2005 wanafunzi wote wa shule za wazazi mbeya tulilazimishwa kwenda sokoine kuujaza uwanja...
Historia yao magamba pamoja na matendo yao yatawahukumu! Vijana hawataki ujinga!
 
Hii kitu ya kulazimishwa maandamo ni vitu vilivyonifanya niichukie saaaana tena saaana CCM toka nikiwa darasa la pili. Mnachukuliwa shule nzima na bendi saa tatu mnaandama km kilomita nane hadi kumi mnaingia uwanjani saa nne labda mnapigwa na jua hadi saa nane, mnaa njaa hakuna cha kula wala maji kwenye chupa enzi zile. Na wakakti ule hakuna mzazi alikuwa anampa mtoto wake pesa mkononi so mnashida na njaa, huyo mgeni rasmi anakuja saa nane mchana anahutubia mpaka saa kumi anaondoka na gari, nyie saas ndo mnarudi home na miguu, kwa kweli ile nikama CHILD Labour! nilikuwa nayachukia sana haya mambo na kuomba mungu siku utawala wa CCM ufike kikomo, CCM mlitutesa sana!! Msikubali kataeni huo utumwa!

Aisee inaudhi mateso wanafunzi tuliyokuwa tunayapata. Halafu maandalizi wakati mwingine yalikuwa yanachukua hadi mwezi mzima kuandaa kwaya, ngonjera na takataka nyingine.
 
Hao wanafunzi wana options mbili; (1) wanaweza kukataa kushiriki maandamano au (2) waende kwenye maandamo lakini waimbe nyimbo za kukataa ufisadi na ccm na ikifika wakati wa kuhutubia wazomeee mwanzo mwisho. Nina uhakika wakifanya hivyo itakuwa mwisho kwa ccm kusomba watu kama wanyama. Zomeeni.
 
Zama za kikoloni hawana wanachama wa kutosha mpaka wawatumie watoto?
 
Back
Top Bottom