Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,030
- 974
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Simiyu Shemsa Seif Mohammed amemshukia Mbunge wa Jimbo la Kisesa Luhaga Joelson Mpina kuacha siasa za Majitaka na badala yake ajikite kuwatetea wananchi waliomchagua.
Aidha, Mwenyekiti huyo amewataka Wabunge wa Mkoa wa Simiyu kufanya shughuli za kuwaletea maendeleo wananchi ili CCM isipate wakati mgumu kuomba kura kwa wananchi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 na uchaguzi Mkuu 2025.
Ameyasema hayo April 25, 2024, kwenye ziara yake ya Tarafa kwa Tarafa iliyofanyika katika Tarafa ya Kanadi, kata ya Langangabilili wilayani Itilima ikiwa ni sehemu ya kukagua na kuimarisha uhai wa Chama kwa akikutana na mabalozi, viongozi wa matawi, mashina pamoja na Madiwani.
Akitolea mfano Jimbo la Kisesa, Mwenyekiti huyo amesema wananchi wanalia kwa sababu wana changamoto nyingi na Mbunge wao (Luhaga Mpina) hajawahi kufika kuwasikiliza badala yake anahangaika na kifo cha Rais Magufuli.
"Badala ya kuhangaika na matatizo ya wananchi, anahangaika na sababu ya kifo cha Rais Magufuli…aliyetuumba ndiye anajua lini na saa ngapi atatuchukua, unasema Mawaziri hawafai, yeye alikuwa Waziri hata salamu kwa wananchi wake alikuwa hawezi kuwasalimia, alitusaidia nini Wanasimiyu alipokuwa Waziri, arudi jimboni akatatue kero za wananchi"
"Wananchi wake wana maboma hayajaisha yanahitaji fedha, wananchi wake wanateseka na Tembo akapambane na waziri wananchi waache kuteseka…asiende kupambana na mipango ya Mwenyezi Mungu anapochukuwa watu wake"
Amesema CCM inapoteuwa Wabunge kwenda Bungeni, ni kwenda kutatua matatizo ya wananchi na kuhakikisha changamoto za wananchi zinatatuliwa huku akisisitiza kuwa Mbunge akishirikiana na Mwenyekiti wa Mkoa kupambania maendeleo ya wananchi yatawafikia haraka sana.
Ameeleza kuwa wana Kisesa wanasikitika sana kuona Mbunge wao akihoji vitu ambavyo hawajamtuma badala ya kujikita kwenye siasa za kujenga jimbo kwa lengo la kuwatetea wananchi.
"Si uhame Kisesa uende huko ili wananchi wa Kisesa wachague mwingine wa kuwaletea maendeleo…nayasema haya kwa sababu nina uchungu, ulipewa Uwaziri, kipi kizuri ulichokifanya wewe kuanzia kwenye mkoa na wilaya yako husika, ni Mbunge anayeongoza hata kwa kutoshiriki vikao vya Chama, anaongoza hata kutokwenda kusikiliza wananchi wake’’ amesema Shemsa.
Ameongeza kuwa, ‘’kila siku yuko kwenye Magazeti na vyombo vya habari inasikitisha sana…unakwenda kuhoji kifo cha mtu Bungeni inasikitisha sana"
Akitolea mfano wa wabunge wazuri, Shemsa amemtaja Njalu Daud Silanga kuwa mchapakazi na anajituma kwa maslahi ya wana Itilima na anashughulikia maendeleo ya wana Itilima.
Amesema wana Mbunge anayepambana na Mawaziri na viongozi wa serikali kuleta maendeleo ya Jimbo huku akiwasisitiza kuendelea kumwombea ili awaletee maendeleo huku akiongeza kuwa ana Wabunge karibia wote wanasema shida za watu.
MWISHO.