CCM Mpeni Ukweli Magufuli, Ajiandae Kisaikolojia

tuache utani ccm please hii ya kwenda na wasanii si nzuri maana tunashindwa kujua wangapi wana muitikio.Tumeshuhudia baadhi ya video wanadai walienda kuona wasanii
 
mimi kuna swala moja najiuliza,hivi ccm bila wasanii mikutano yao wangemhutubia nani?

Hivi ccm hawaoni kuwa uhalali wao wa kuitawala hii nchi umefika ukingoni?

Maana kama unataka kuwa rais wa nchi"kama magufuli"na ukiitisha mkutano kuongea na wananchi hawaji kukusikiliza na hustuki tu kuwa hawakupendi ni upofu kibri au laana?

Mi nadhani ni vema wapambe wa magufuli wamweleze ukweli kuhusu ile mikutano yake,asije juwa anapendwa kumbe watu wamefuata burudani ya bure na kubebwa na mafuso.

Asipoelezwa ukweli upo uwezekano akashindwa uchaguzi na kung'ang'ania ushindi kwa upotoshwaji anaofanyiwa na wapape wake.na nchi ikaingia kwenye mtafaruku.

Ni bora mumweleze ukweli ajiandae kisaikolojia.

ni kweli,.....
 
Kibo 10 jina lako linajieleza kuwa wewe ni wa wapi?watu wa mkoa huo tabia zenu tunazijua,tukiwakabidhi nchi sijui kama mtabakisha raslimali hata moja

Hii ndio hoja sasa? Jionee aibu hata kiduchu kabla hujaandika.
 
Ukawa hawaweki wasanii kwenye mikutano? Kuna kipi cha ajabu kwenye mikutano ya Ukawa? Kama mnaona mna mvuto sana, kwanini msiache kuita wasanii kutumbuiza? Thread nyingine sijui kwanini zinawekwa hapa?
 
Kibo 10 jina lako linajieleza kuwa wewe ni wa wapi?watu wa mkoa huo tabia zenu tunazijua,tukiwakabidhi nchi sijui kama mtabakisha raslimali hata moja

Wanaweka mbele sana ukabila,ukanda na udini hata kwenye mambo ya msingi kabisa. Sijui wakipewa nchi watu wengine wataishi vipi? Mmakonde, Mngindo, Mpogoro au Mzaramu asije akategemea kupewa ajira katika kitengo cha shirika ambalo lina boss wa kutoka huo ukanda hata kama ana vigezo.
Ukisema haya, watajitetea kuwa wao tu ndio waliosoma zaidi kwa hiyo ni automatic wao kupewa ajira kabla ya wengine kutokana na wengi wao kuwa na vigezo zaidi kuliko watu kutoka maeneo mengine.
Ndio maana wavivu wengi, mabwanyenye, watoto wa mama kutoka familia fulani zilizo na uwezo fulani, matajiri waliofilisika au ambao biashara zao zinapumulia gesi, kundi la watu wanaotumainia vyeo na madaraka makubwa na watu wenye character kama hizo kutoka ukanda huo wako nyuma ya Lowassa kwa matarajio kuwa watapata nafasi ya kupiga dili zaidi na kuwa marais wadogo na kudumisha mfumo wao wa kubebana.
 
Msibaki na historia, lowasa moto wa mabua, hayo mabomu ya udini yanayoibuliwa yanambomoa kwa kiwango kikubwa. Inabidi mmwambie ukweli akiendelea kujipa matumaini hewa atarest in peace sababu ya mshtuko wa kushindwa

Hakuna mtu anaedanganyika kirahisi kwa politics za Lowassa,eti ni maarufu. Lowassa ni maarufu?
 
Wanaweka mbele sana ukabila,ukanda na udini hata kwenye mambo ya msingi kabisa. Sijui wakipewa nchi watu wengine wataishi vipi? Mmakonde, Mngindo, Mpogoro au Mzaramu asije akategemea kupewa ajira katika kitengo cha shirika ambalo lina boss wa kutoka huo ukanda hata kama ana vigezo.
Ukisema haya, watajitetea kuwa wao tu ndio waliosoma zaidi kwa hiyo ni automatic wao kupewa ajira kabla ya wengine kutokana na wengi wao kuwa na vigezo zaidi kuliko watu kutoka maeneo mengine.
Ndio maana wavivu wengi, mabwanyenye, watoto wa mama kutoka familia fulani zilizo na uwezo fulani, matajiri waliofilisika au ambao biashara zao zinapumulia gesi, kundi la watu wanaotumainia vyeo na madaraka makubwa na watu wenye character kama hizo kutoka ukanda huo wako nyuma ya Lowassa kwa matarajio kuwa watapata nafasi ya kupiga dili zaidi na kuwa marais wadogo na kudumisha mfumo wao wa kubebana.

Mkuu mimi ni Mzaramo na ni mwana mageuzi kwahiyo hoja yako hii baki nayo kichwani mwako. Habari za Ukanda, udini na ukabila ni habari zenu ambazo hazita badilisha vuguvugu la kuleta mabadiliko ya kimaendeleo ndani ya nchi hii. Mmezoa kuwa mabwenyenye mkifikiri kila mtanzania ni mwenye kuhitaji kuishi katika hali hiyo. Kuwa tayari kutokuamini kinachokuja kutokea. Then utakuja na hizo hoja zako kama Rais atakuwa kachaguliwa na kanda moja tu au lah.
 
Umewapa ushauri mzuri na lazima wajitahidi kuufuata.
Hebu angalia siku ambayo Dr. Slaa aliongea, magazeti yao yote yaliweka front page na kukoleza maandishi. Hebu angalia jana Gwajima alipoongea, nimeangalia Jambo Leo, Uhuru, Habari Leo wote hakuna aliyeandika hiyo habari front page.
Ni vizuri wakajifunz kutofautisha propaganda na ukweli kwa maana ukweli una nguvu zaidi
 
Mkuu mimi ni Mzaramo na ni mwana mageuzi kwahiyo hoja yako hii baki nayo kichwani mwako. Habari za Ukanda, udini na ukabila ni habari zenu ambazo hazita badilisha vuguvugu la kuleta mabadiliko ya kimaendeleo ndani ya nchi hii. Mmezoa kuwa mabwenyenye mkifikiri kila mtanzania ni mwenye kuhitaji kuishi katika hali hiyo. Kuwa tayari kutokuamini kinachokuja kutokea. Then utakuja na hizo hoja zako kama Rais atakuwa kachaguliwa na kanda moja tu au lah.

Huo ni mtazamo wako na hoja kuwa wewe ni mzaramo pia haina uthibitisho pia kwa kuwa uko nyuma ya keyboard na tunachokijua kuhusu wewe ni kile unachochagua kutujulisha. Hata hivyo hiyo haibadilishi ukweli kuwa wengi wanaelewa kuhusu ubaguzi kwa kuwa wako kwenye mfumo wa ajira tofauti na wewe ambae unaweza kuwa uko kwenye kijiwe au hata mfumo wa ajira binafsi.
Na kwa kukusaidia tu, Mimi si bwanyenye na wala silishwi na CCM ila Nimefaidika na mazingira bora yaliyowekwa na chama hicho katika mfumo wa elimu ulioniwezesha mimi kufaidika na hata kuwasaidia wengine.
Kinachonitia moyo ni kuwa, kuna wengi tu ambao wanaelewa nachokizungumza ingawa hawatasema hapa kwa kuwa hili lipo wazi. Huwezi kupeleka kampeni kanisani halafu usiitwe mdini, halafu unatumia kabisa kauli kuwa uchaguliwe kwa kuwa wewe ni dhehebu fulani, ina maana unapigania uongozi au utawala wa dini yako? Huwezi kuzungukwa na mashabiki wanaoamini kuwa wakiwa wakuu wa vitengo basi ni lazima waajiri watu wa kutoka kanda yao, wamepindisha mpaka katiba ili wewe upewe nafasi ya kugombea urais. Wanataka uwafanyie nini? Kwanini wanakulinda sana? Halafu mnatoka wote kanda moja. Wanataka kufaidika nini na uwepo wako madarakani kama sio muendelezo wa ukanda?
Chadema kinataka kutawala Ukawa, vyama vingine vinasindikiza tu. Na kinachofurahisha zaidi ni kuwa hicho ni chama chenye misingi ya kifamilia zaidi kuliko kitaifa. Lakini wengi mnaburuzwa tu.
 
Mimi kuna swala moja najiuliza,Hivi Ccm bila wasanii mikutano yao wangemhutubia nani?

Hivi Ccm hawaoni kuwa uhalali wao wa kuitawala hii nchi umefika ukingoni?

Maana kama unataka kuwa rais wa nchi"Kama Magufuli"na ukiitisha mkutano kuongea na wananchi hawaji kukusikiliza na hustuki tu kuwa hawakupendi ni upofu kibri au laana?

Mi nadhani ni vema wapambe wa Magufuli wamweleze ukweli kuhusu ile mikutano yake,Asije juwa anapendwa kumbe watu wamefuata burudani ya bure na kubebwa na mafuso.

Asipoelezwa ukweli upo uwezekano akashindwa uchaguzi na kung'ang'ania ushindi kwa upotoshwaji anaofanyiwa na wapape wake.Na nchi ikaingia kwenye mtafaruku.

Ni bora mumweleze ukweli ajiandae kisaikolojia.

Bila ya kusahau mbinu hii;
 
Kweli nimeamini ule msemo kila kitu kinamwisho wake na huu ndomwisho wa cc dar mpaka inatia huruma jamani pole cna kufuli
 
Nimehudhuria mikutano miwili ya Pombe Magufuli Arusha Mjini na Moshi.

Wengi wanazombewa na takrima,wengi ni ccm mchana,picha zinazotumiwa na vyombo vya habari zinaunga ungwa na mikutano mingine.

Ukweli usio na itikadi ni kuwa mgombea wa ccm hali yake ni ngumu huku akikatishwa tamaa zaidi na wilaya ya ARUMERU na Monduli ambayo hakufanikiwa kufanya mkutano wowote ktk eneo hilo analotoka Lowassa.
 
Back
Top Bottom