CCM Mko wapi? Mbona hamtokei ili kujibu mapigo? Naona banda linachakazwa na mchwa!

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
CCM mko wapi kuja kujibu mapigo ya wapinzani hasa chama kikuu cha upinzani kwenu CDM. Naona mmebaki jeshi la mtu mmoja mmoja huku mkimwacha Nape peke yake acheze nafasi zote uwanjani, goli kipa yeye! Beki yeye, kiungo mkabaji yeye, kiungo mshambuliaji yeye, refari yeye, kualika mashabiki yeye! Yote katika mechi moja tu. Pumzika kaka, au chama ndiyo mwisho wake umewadia? Manake naona pambano lenu na CDM ni sawa na kumpambanisha Tyson na Maneno Osward.
 
,,,teh!,,Labda wanakula timing ya kumchinja kobe!,,,Ila kiukweli naona kama game ni ya upande mmoja.
 
Nasikia Nape anakuja na Operesheni Vua Gamba Vaa Uzalendo ha ha ha Magamba yamewashinda kwenye Vikao sasa mnayatengezea kauli za Kwenye Kanga
 
Back
Top Bottom