CCM maslahi inavyokiangamiza chama na kuhatarisha amani ya nchi

Tetty ccm ina mchango mkubwa sana kwenye woga wa watanzania, wamefanya mbinu nyingi chafu sana vikiwemo vitisho na mauaji, mateso na ulaghai kuweza kubaki madarakani
Nyuma ya ccm kuna kundi kubwa sana la kinachoitwa NCHI RAFIKI hawa wana maslahi makubwa sana, wanafaidi rasilimali zetu kupitia ccm, hawa ndio vinara wa kutoa mamilioni ya dola na support ya kila aina ili ccm ibaki madarakani wahindi na Wachina huwaambii kitu kuhusu ccm

Ni kweli hiki chama kimefanya watanzania tuwe waoga total ndio maana tunashidwa kutetea rasilimali zetu. nipo maeneo ya vijijini kusini huku yani hakuna redio inayoshika kabisa watu elimu ya uraia hakuna na hii ni plan kwa CCM kupata kura kiraisi kwa kuwapa pombe na nyama tuu
 
Last edited by a moderator:
naona pumba tu humu. hata hiyo ARV scandal wala siyo ya bulembo. try to behave as a matured.


Ndani ya CCM kuna makundi mwili, CCM asili na CCM maslahi
Hawa asili bado wana damu ya uzalendo na fikra pana kwa kiasi chake, ni wazee na hekima yao iliyopunguka sana bado wanafanya mambo kwa kutafakari sana

Shida kubwa kabisa ni hawa CCM maslahi, ni kundi kubwa la wezi mafisadi wanaoandaliwa mahakama na Magufuli, wapiga dili na rushwa zilizonona, na hiki ndio kipindi chao cha mavuno kipindi cha kutengeneza pesa ndefu isiyo na query
Ni kitengo chenye watu wenye lengo moja tu... Kupiga pesa kadiri iwezekanavyo

-ndio wanaratibu michango na misaada yote kwa chama Kwasasa
-ndio wanapanga bajeti na minimizing yote kuanzia mafuta mabango nguo vipeperushi matangazo yote nknk
-ndio wapangaji na watufutaji vijana wa propaganda mitandaoni
-ndio watufutaji na washawishi wakuu wa linings watu kutoka UKAWA na makundi mengine katika jamii

Kwa ufupi ndio wahusika wakuu kwenye chama kuhusiana na swala zima linalohusu pesa
Hawajali wanasema nini kwenye mikutano ya hadharani, kwenye vyombo vya habari, kwenye mitandao ya kijamii nk wao wanachoangalia ni kwamba wanapata bei gani kwenye nini
Matamshi yao hawapimi athari zake kwa chama chao na kwa taifa,na kwa uharaka wao na bila tafakuri wanajikuta wakiwa ni watu wa kucopy na kupaste toka UKAWA
Concern yao kubwa ni kutaka kuhalalisha matumizi ya pesa ndefu wanayopiga kila mahali na kwenye chochote
Bulembo kada wa CCM, mfanyabiashara mwenye kesi mahakamani kuhusiana na ARV'S FAKE ni mmojawapo wa CCM maslahi hakipiganii chama bali maslahi yake binafsi kwakuwa anajua UKAWA wakichukua nchi hatima yake ni Segerea
 
Username yako imenikumbusha mbali sana... Wakati ule tunasoma hekaya za abunuwasi na jinsi alivyokuwa juha
kwa hiyo hata bulembo ndo mmiliki wa kiwanda ARV kule arusha? I am sure you can do better than this.
 
Ccm ilishaoza na kufa tujadili mabadiliko pekee.viva ukawa.lowasa na tanzania mpya ndani ya ukawa.
 
Baada ya uchaguzi na ccm kuanguka tutashuhudia mengi ambayo Kwasasa hayawezi kusemwa, kuanzia tenda za kuchapisha T-shirts, kofia nk, mabilioni yaliyotengwa kuumaliza upinzani, kiasi kilichotumika na kama kilitumika kwa usahihi na impact yake
Kashfa zitakazotokea baada ya uchaguzi ndio itakuwa msumari wa mwisho kwenye jeneza la ccm kuelekea kwenye kaburi la sahau

Viongozi wa Ukawa pia wanatakiwa kutatua changamoto walizonazo na kuhakikisha wanashinda.
Nafirkiri kuwa endapo Ukawa wakishindwa katika uchaguzi huu anguko lao litakuwa kubwa na baya zaidi.
Itarudisha nyuma sana jitihada ya demokrasia ya vyama vingi.
 
Back
Top Bottom