Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
Sisiemu kujivua gamba kwa kulivunja baraza la mawaziri!
Inapokuja swala la kuendelea kubaki madarakani sisiemu huwa haina cha msalia mtume na huchukua hatua stahiki kwa kuwamwaga makada wake walioshindwa kusoma alama za wakati.
Ni dhahiri sera ya ubinafsishaji wa taasisi za umma siyo chagua la wananchi wa taifa hili hususani kutokana na mchango wake kiduchu kwenye maeneo yote ambayo yalitaifishwa.
Hakuna hata kiongozi mmoja ndani ya sisiemu yuko tayari kutathmini zoezi zima la ubinafsishaji tangia Mkapa aingie madarakani.
Mfano tu, sekta ya madini tu inazalisha zaidi ya dola za kimarekani bilioni 5 kwa mwaka lakini mchango wake kwenye bajeti ya serikali ni chini ya asilimia moja tu.
Wanaonufaika na sera za uwekezaji ni wachache mno huku wengi tunachoambulia ni mzigo wa kodi kuwaruzuku wawekezaji feki.
Kutokana na hii sera ya hovyo na isiyo ya tija sisiemu haina jinsi ni kujivua gamba kwa kulivunja baraza la mawaziri na kuwatupia virago vyao akina maprofesa uchwara Kitilya Mkumbo, na huyo wa uchukuzi ambao kwa pamoja wamedhihirisha hawana ujuzi wala maarifa ya kusimamia kitu kidogo kama bandari na kuongeza mapato, mitambo kusomana n.k
Waziri Mkuu pia kutemwa kwa kuwadhalilisha watanzania hawana uwezo wa kuzisimamia bandari zao miaka 61 baada ya uhuru.