Elections 2010 CCM kufunga mawasiliano ya simu siku ya uchaguzi

mchonga

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,233
248
Habari za uhakika toka kambi ya CCM, zimeeleza kuwa CCM kwa kutumia serikali yake iliyopo madarakani inafanya mpango wa kuzima mawasiliano ya simu hasa za mikononi ili watu wasiwasiliane kujua matokeo ya kituo na kituo.

Nasema habari ni za uhakika kwa kuwa nimezinasa kwa bahati mbaya kupitia mawasiliano ya Emails ambayo imefika kwangu kwa bahati mbaya.

Kwa wanatumia M-PESA kuwahonga wapiga kura. kiwango cha chini ni 5,000 na wenye bahati 10,000 kwa kura. tena wanawatumia watu wenye ushawishi ili kutoa hongo hiyo kwa wapigakura.

Kazi ipo kweli, kweli kwa mtaji huu hata takukuru watapata taabu sana. mimi ningeshauri kuanzia hivi sasa utumaji wa pesa ufuatiliwe kwa karibu sana.

Naliweka janvini
 
Mzee inawezekana kweli? Hapana, nadhani hukusikia vizuri.

Mwanzoni nilidhani thread yako ilikuwa inalenga ile kauli ya Makamba ya kuwanyima wagombea ubunge wa CCM kushiriki midahalo. Kama watathubutu kuzuia simu basi makubwa.

But mbona unafisha source yako
 
Wakati wenzao wamefanya upigaji kura kuwa computerise wao wanajirudisha kujichimbia kwenye zana za mawe.
WASHINDWE NA WALEGEE KAMA JK WAKATI WA UZINDUZI WA CAMPAIGN JANGWANI.
 
But mbona unafisha source yako

source siwezi kuitaja maana ilinaswa kupitia private msg, sasa nikiitoa tu nitavunja sheria na kanuni namba 4 ya JF, mimi ni third party. ww unaweza kuona ukweli wake. kwa mara ya kwanza mimi nilisikia hili kupitia ITV, kupitia kipindi chao cha kipima joto. Pia Tendwa alikuwepo live kwenye mdahalo ele na alionyesha ku-panic na kuwa un-comfortable kweli. Nikapuuza. Lakini kwa mtaji huu naanzan kuwa na wasiwasi.
 
Ni move ya kutarajiwa; kwa sababu kubwa ya mabadiliko ya utaratibu wa utangazaji wa kura za urais uliofanywa na Tume ya Uchaguzi.

Kinyume na miaka ya chaguzi nyingine huko nyuma mwaka huu kwa mara ya kwanza, matokeo ya kura za rais yatatangazwa hapo kituoni kama ilivyo kwa matokeo ya ubunge na udiwani. Hivyo ni rahisi kwa mtu yeyote kuweza kuanza kupata picha ya kura zilivyo kwa kukusanya matokeo hayo toka kituo na kituo.

Kama kutakuwa na mpango wa namna hiyo hata hivyo, unatakiwa uwekewe pingamizi mapema kabisa katika mahakama ili serikali isizuie mawasiliano ya wananchi na haki zao za faradha. Japo naamini hawatotoa sababu hiyo zaidi ya sababu za kiusalama wa taifa au another bs kama hiyo.
 
Habari za uhakika toka kambi ya CCM, zimeeleza kuwa CCM kwa kutumia serikali yake iliyopo madarakani inafanya mpango wa kuzima mawasiliano ya simu hasa za mikononi ili watu wasiwasiliane kujua matokeo ya kituo na kituo.

Nasema habari ni za uhakika kwa kuwa nimezinasa kwa bahati mbaya kupitia mawasiliano ya Emails ambayo imefika kwangu kwa bahati mbaya.

Kwa wanatumia M-PESA kuwahonga wapiga kura. kiwango cha chini ni 5,000 na wenye bahati 10,000 kwa kura. tena wanawatumia watu wenye ushawishi ili kutoa hongo hiyo kwa wapigakura.

Kazi ipo kweli, kweli kwa mtaji huu hata takukuru watapata taabu sana. mimi ningeshauri kuanzia hivi sasa utumaji wa pesa ufuatiliwe kwa karibu sana.

Naliweka janvini

Mkuu tunaomba uiweke hiyo e mail humu jamvini.
 
Mwanakijiji mimi nimeliona hilo, kwa hiyo wahusika kama watasoma habari hii wawe makini kuzuia mpango huu kama upo. wasiwasi wangu siyo kura za Rais, ni kura za wabunge. Kwa sababu kura zikitangazwa kituoni watu wanaweza kujua instantly na ku-tex matokeo palepale bila kuchelewa. sasa hili linawanyima usingizi wahusika watakosa kufanya madudu yao kablaa ya watu kujua chochote.
 
Mkuu tunaomba uiweke hiyo e mail humu jamvini.
Thats right aweke email tuione otherwise ni maneno ya kujitungia tu, CCM si wajinga kiasi hicho wakati simu hazitumiwi na walio ndani ya Tanzania tu itakuwa international issue kwa vile external observer watakuwepo.
 
Kama CCM wangekuwa wamiliki wa kampuni zenye mitandao hiyo ya simu za mkononi, wangejaribu - lakini wasingeweza - kuzima mitambo ili wateja wasiwasiliane siku hiyo. Njia pekee ya kusitisha mawasiliano ni kwa kutokea maafa; tetemeko la ardhi, tsunami, kimbunga, n.k.

CCM hawawezi kutengeneza maafa, kwa hiyo jambo la mawasiliano ya simu kukatwa, HAIWEZEKANI! Sema kingine.

Pia, hata kama CCM ndicho chama chenye kiti cha nchi, hawawezi kuziamrisha kampuni za simu kukata mawasiliano, kwa kuwa hili ni suala la kibiashara, na pia, wenye mitandao hii wana mkataba na wateja wao. Wateja wanalipia huduma, kwa hiyo ni LAZIMA waipate, labda yatokee maafa kama nilivyotaja hapo huu.

Hivi kuna mmiliki wa kampuni ya simu ya mkononi anaweza kukubali kuwa JUHA namna hiyo kiasi cha kukata mawasiliano ili wateja wasiwasiliane? Kama CCM wanadhani hili linawezekana, basi wao ni wapumbavu kuliko Juha Kalulu!

Hata kwa ndoto za Alinacha au hekaya za Abunuwasi, HILI HALIWEZEKANI! Hakuna atakayekubali upumbavu huu! HAKUNA!

Nimeeleweka.

-> Mwana wa Haki

P.S. Ingekuwa vema u-copy and paste hiyo email hapa. Kuwa muwazi. Unaweza tu kuficha anuani yako wewe, lakini kama unataka kuwa muwazi, anuani ya aliyetuma ujumbe huo USIIFUTE. La sivyo tutakuona mzushi! JamiiForums ni mahala pa watu makini, bro/sis!
 
labda wakate na mawasiliano yote hadi ya kwenye mtandao pia. Tena ingekuwa ni jambo la busara kuwa na website inayoweka matokea hewani kadri yanavyopatikana na kutumwa ili watanzania waone nini kinakwenda vipi. Kama matokeo yote ni papo kwa hapo basi mwaka huu uchaguzi huu ni kiboko a chaguzi zote. Hii lazima mtu uingiwe na joto hata kama hupendi.
 
Hilo la kuwaza kukata mawasiliano wanaweza kuwa wamewaza kwa sababu CCM kuna majuha wa ajabu ambao ndio 'think tank' yao. Kuna watu wanaoitwa washauri lakini akili zao ni ndogo sana. Wamezoea kutumia maguvu hata pasipohitajika. Kwani wakikata mawasiliano wao CCM watawasiliana kwa ungo?

Kinachoweza kufanyika hapa JF ni kutengeneza simple data base ambayo mod/invisible atakuwa anajaza matokeo kituo kwa kituo jinsi yanavyokuja. Nadhani sasa hivi NEC wana list ya vituo vyote. Hii ni kazi kubwa kidogo ila kwa kuwa tunataka 'kuisaidia' NEC inawezekana. Pia hii itawezesha JF kuwa kati ya eneo ambalo watu wanaweza kuja kupata taarifa na kuzichambua na kupima uchakachuaji.
 
labda wakate na mawasiliano yote hadi ya kwenye mtandao pia. Tena ingekuwa ni jambo la busara kuwa na website inayoweka matokea hewani kadri yanavyopatikana na kutumwa ili watanzania waone nini kinakwenda vipi. Kama matokeo yote ni papo kwa hapo basi mwaka huu uchaguzi huu ni kiboko a chaguzi zote. Hii lazima mtu uingiwe na joto hata kama hupendi.
Sio busara kukata mawasiliano kwani ni kutangaza hali ya hatari,lakini ikitokea kwa makusudi,basi zoezi zima la uchanguzi litakuwa batili.Wafadhili wa nchi za Magharibi watakuwa wa mwanzo kukata misaada kwa serikali itakayoingia madarakani ikiwa itakuwa ya CCM.Itawachukua muda mrefu nchi wahisani kurudisha imani kwa serikali hiyo,na serikali ya CCM haiwezi kuruhusu hilo litokee kwani bajeti yao ni tegemezi,na hilo wanalielewa.
 
Mimi nadhani lisemalo lipo. Inawezekana ni wanaCCM walikuwa wanajadili mikakati ikiwa ni pia njia hii ya kuzima mawasiliano. Ila tusiseme haiwezekani kumbukeni Kibaki alijaribu kutumia njia hii huko Kenya. Na Vodacom iko kwa Rostam, Zain ni ya wahindi ambao hawajajiamini, na pia wawekezaji wa Bongo wanapenda kujipendekeza kwa watawala hivyo wanaweza kukubali. Pia mamlaka inayosimamia mawasiliano TCRA sina uhakika kama wana ubavu wa kuikatalia CCM. Mi nadhani ni vyema kukaa macho na kuiongelea suala hii iwe kwenye consicousness ya jamii...
 
Sio busara kukata mawasiliano kwani ni kutangaza hali ya hatari,lakini ikitokea kwa makusudi,basi zoezi zima la uchanguzi litakuwa batili.Wafadhili wa nchi za Magharibi watakuwa wa mwanzo kukata misaada kwa serikali itakayoingia madarakani ikiwa itakuwa ya CCM.Itawachukua muda mrefu nchi wahisani kurudisha imani kwa serikali hiyo,na serikali ya CCM haiwezi kuruhusu hilo litokee kwani bajeti yao ni tegemezi,na hilo wanalielewa.

Mi naona kama vile haiwezekani!
Maana katika watu wanaohitaji mawasiliano zaidi siku hiyo ni hao CCM!
MAWASILIANO KAZI YAKE SI KUTOA MAJIBU YA UCHAGUZI TU JAMANI!.Yanahitajika katika logistics mbalimbali ILI KULIFANYA ZOEZI ZIMA LIWE SUCCESS!..HUH!!
 
Tusiwa-underestimate CCM, wapo desperate na wanaweza kufanya chochote ili wabakie madarakani. Ni suala la kifaa kimoja kinacho-control mawasiliano kuharibika na nchi kutokuwa na mawasiliano for 3 hours muda ambao unatosha kabisa CCM kufanya mambo yao ili by the time mawasiliano yanarudi, kila kitu wanakuwa walishamaliza.

Nadhani VYAMA washindani wa CCM inatakiwa waweke Precautionary Strategy na Plan B kama mawasiliano yatakatika.
 
Hivi ni kosa kuwapa wapiga kura hela kuchagua chama flani bila wewe kua mwana chama yeyote. Yani wewe sio affiliated na chama yeyote wala wewe sio mgombea lakini una toa hela kwa watu ili wachague chama wewe unayotaka. Hivi ni kosa?:confused2:
 
Kwani CCM wakikata alafu suala la logistics za matokea kuwa shared na watu likakwama then baadae wakaja omba msamaa kwa katizo ilo tutawafanyaje.
Watu mnatahamaki kuwa haliwezekani CCM wako desperate wanaweza fanya chochote ili mradi washinde angalau kwa 55-50% manake sioni kwa sasa wakiongelea ushindi wa Kishindo
 
Back
Top Bottom