wazo lako ni zuri, ila kwa upande mwingine ukirudi kwa hawa madiwani ni kwamba wao wanajiamini kuwa wana support kubwa ya wananchi na ndio maana wakakomaa mpaka wamefukuzwa uanachama.kuwaacha bila kuwapa a second chance iwe CDM au chama kingine itakuwa siyo kuwatendea haki. ni vizuri wakawaeleze wananchi ni nini walichokuwa wanapigania na waombe nafasi ya kuchaguliwa tena ili wakakamilishe kazi walioianza ya kupambana na ufisadi.Utaratibu huu ni angamizo la Demokrasia na ni Jeneza la CDM. Sipenda CDM kuruhusu tena Mateja kama Shibuda. Naamini CDM ina watu wengi wazuri wakuchukua nafasi hizo na Ukatumika utaratibu mzuri wa kuwapata wagombea wasio kuwa na tabia za PANYA, Baba mwizi, mama mwizi, mtoto mwizi, Panya wote wezi, achaneni na tabia hii mbovu ya kuokota MAKOMBO ya ccm. Sipendi kuona CDM ikichukuwa viongozi toka ccm. HAKUNA KIONGOZI ccm alie SALAMA wote wameathirika na VIRUSI vya UFISADI
I don't really care about this CCM hata kama watachinjana, mazishi yao siendi ng'oooHiyo ni adhabu au ni ukombozi!?
Nimeangalia taarifa ya habari kutoka kituo cha itv usiku huu,nimesikitishwa na kushangazwa sana na taarifa ya kufuzwa kwa madiwani 8 huko Bukoba.kinachoonekana ni kwa kwamba kila anayechukizwa na wizi wa pesa za inchi hii ni adui mkubwa wa CCM,wametetea kuliwa kwa mamilioni ya pesa za wananchi badala ya kuungwa mkono na kusaidiwa wanaishia kufukuzwa?hii ni aibu kubwa kwa chama hiki.hakina huruma hata kidogo na watanzania,hii ni ishara ya wazi kuwa CCM ni wezi,ni majambazi wa mali za umma.Nawasihi wa TZ wenzangu tusikubali kufanywa wajinga na CCM tuikatae katakata,ujinga si ugonjwa hauhitaji dawa yoyote wala kwenda hosp,ni jambo la maamuzi tu.huitaji degree kutetea rasilimali za inchi hii.
Kweli kabisa, wengi hatutaliangalia hili katika mtazamo wa kiuchumi.Tutaishia kwenye nyuzi za kisiasa tu.Chaguzi zetu zinatumia nguvu nyingi mno,kazi za maana zote huwa zinasimama, watendaji karibu wote wataelekeza akili na macho yao huko.Madiwani 8 ni mtaji tosha!!!
Lakini tuache utani kufukuza madiwani 8 si jambo dogo!! Kwa mara nyingine siasa zinaenda kutuingiza katika gharama za kijinga kabisa!!
Mbona sasa Hawaii inasemekana wanatetea uamuzi aw wanna hi? Sasa hizi ni me hi nyingi. Waenda CDMA, Hawaii wanafaa katika nguvu ya umma.Kwa ufupi
· Msimamo wa madiwani waliotimuliwa ilikuwa ni kumtaka Meya wa Manispaa ya Bukoba kungoka.
· Bukoba: Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kagera kimewafukuza uanachama wa chama hicho, madiwani wake wanane kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kukaidi maelekezo mbalimbali ya chama hicho, pia kushirikiana na upinzani kukihujumu.
· Madiwani waliotimuliwa ni wale Manispaa ya Bukoba ambao wamekuwa wakitajwa kumuunga mkono Mbunge wa Bukoba Mjini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki ambaye amekuwa akivutana vikali na Meya wa Manispaa hiyo, Anatory Amani.
· Miongoni mwa waliotimuliwa ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba na Diwani wa Kashai, Yusuph Ngaiza, aliyepata kuwa mbunge wa muda mrefu wa Bukoba Mjini na baadaye Meya wa Manispaa hiyo, Samuel Ruhangisa ambaye ni Diwani wa Kitendagulo na Diwani wa Buhembe, Alexander Ngalinda ambaye pia alikuwa Naibu Meya.
· Katibu wa CCM wa Mkoa wa Kagera, Averin Mushi alisema uamuzi wa kuwatimua madiwani hao umefikiwa jana na halmashauri ya CCM ya Mkoa kwa kile alichosema ni kwa ajili ya kulinda masilahi ya chama na wananchi wa Bukoba.
· Ibara ya 93 (15) ya Katiba ya CCM inataja moja ya kazi za halmashauri ya chama hicho ngazi ya mkoa kuwa ni: Kumwachisha au kumfukuza uongozi kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake wa mwisho unafanywa na Halmashauri ya CCM ya Mkoa.
· Hata hivyo kipengele cha 14 cha ibara hiyo ya 93 kinasema hatua kumwachisha au kumfukuza mtu uanachama itachukuliwa endapo halmashauri itaridhika kwamba tabia na mwenendo wake vinamwondolea sifa za uanachama.
· Hatua ya kuwafukuza uanachama madiwani hao ambao pia watakuwa wamepoteza nafasi zao za udiwani, imekuja siku chache tangu Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alipozitaka pande zinazohusika katika mgogoro huo kumaliza kwa njia ya mazungumzo.
· Madiwani wote wa CCM walioendelea na mgomo hata baada ya maelekezo ya Mheshimiwa Rais kwa kusaini barua ya kutaka Mkurugenzi aitishe kikao cha kumwondoa Meya tumefikia uamuzi mgumu wa kuwafukuza uanachama kwa masilahi ya chama na wananchi wa Bukoba, alisema Mushi.
· Mushi aliwataja madiwani wengine waliofukuzwa ni Robert Katunzi (Hamugembe), Deus Mutakyahwa (Nyanga), Richard Gasper (Miembeni), Mulungi Kichwabuta (Viti Maalumu) na Dauda Kalumuna aliyekuwa Diwani wa Ijuganyondo.
· Katibu huyo alisema Balozi Kagasheki na Meya Amani ambao mamlaka yao ya uteuzi ni ya kitaifa na wanatakiwa kumaliza tofauti zao kama walivyoelekezwa na Rais.
· Mgogoro uliosababisha madiwani hao kutimuliwa uliibuka baada ya Kagasheki kumtuhumu Meya Amani kwamba ameingiza Manispaa katika miradi ya ufisadi hali ilioibua makundi na kukwamisha kufanyika hata vikao vya Baraza la Madiwani.
Chanzo: MWANANCHI