justus ndyanabo
JF-Expert Member
- Jun 2, 2015
- 444
- 378
ccm wote majizi
Lowassa hawezi kuenguliwa na ndilo hofu na tumaini la wengi. Kama ataenguliwa basi CCM itapona japo sasa hivi ipo ICU watu hawajui tu ila wao wanajua hilo. Wala sio wasiwasi ya Lowassa kukihama chama bali vichwa haswa wamejiandaa kukihama chama kama Lowassa atapita uchaguzi CCM na hiki ndicho UKAWA wanakisubiri mwaka huu 2015 - kazi kwisha... Ya Mwanakijiji yametimia.
Imekuwa kama watoto wadogo,eti Lowasa anatishia wenzie akikatwa atamleta Dr.Balali,sasa hicho ni chama ama ni genge la wavuta bangi nibangue
Hili ndilo tatizo kubwa la nchi hii na watu wake, hatuna uthubutu. The Boss, ni chama kipi kingine kimewahi kukamata madaraka ya nchi hii hadi useme hakuna replacement inayoaminika? Unatumia vigezo gani? Yaani unataka kuwaambia Watanzania waendelee kuongozwa na dead man walking kuliko kuwapa wengine ambao angalau wanajitutumua? What kind of thinking is this? Comments kama hizi huwa zinanikera kweli kweli kwani ni kama vile hivi tumelogwa, taifa limejaa dead men walking! Fikiria tunao watu wanaosema, hapana imetosha, hatuwezi kuendelea na watu wale wale, ni heri tufanye mabadiliko halafu anakuja mwingine anadai haoni mbadala, heri tuendelee na wale wale!
I understand, change can be scary. Doing anything for the first time or stepping into the unknown can at times be frightening and so requires courage and resolve, two ingredients most of us Tanzanians lack. But when one has hit rock bottom like we have, the only way out is up. It is insane to expect the same minds that led us into the pit to take us out of it hence the need for change; complete overhaul and complete about turn.
Kuvunjika kwake kumechelewa; kulipaswa kutokea tangu Kikao cha Butiama. Na labda ingevunjika hata kabla ya uchaguzi wa 2010. Ilichelewa kwa sababu bado hakukuwa na watu waliokuwa tayari kuimegua. Sasa hivi watu hao wapo, sababu zipo na inaonekana kuvunjika huku safari hii hakuepukiki - iwe kabla ya Uchaguzi au baada ya uchaguzi (itakapopoteza kiti cha Urais).
Ni vigumu kwa wote waliomo humo ndani kuweza kurithi yaliyomo ndani; wameshindwa kukaa kwa amani na sasa inaonekana wanaelekea kugongana. Wangeweza kuepusha mambo haya miaka kadhaa iliyopita ambapo wengine tulishauri mapema tu usalama wake ni kumeguka. Tofauti ambazo zimefunuliwa ndani ya chama hasa linapokuja suala la ufisadi ni kubwa mno kiasi kwamba ni vigumu kuona jinsi gani watu hawa wataweza kuwa wamoja kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Na hili limesababishwa kwa kiasi kikubwa na udhaifu wa mifumo na taratibu za chama kushughulikia watu maarufu kiasi kwamba watu hao sasa wamepata nguvu kubwa kiasi cha kutishia uwepo wa chama na tishio hilo haliondoki kwa mikwara tena. Mikwara ingekuwa inaondoa watu basi "operesheni vua gamba" ingekuwa tosha kabisa. ILishindwa ile, zilishindwa hotuba za mikwara za mwenyekiti na hata maneno ya baadhi ya wana CCM yalishindwa kuwaondoa 'mafisadi'. Nina uhakika hata hili la "tuachieni chama chetu" litafeli. Wanaodai chama ni chao watajiuta hawana chao tena isipokuwa kuondoka.
Na kama watabakia itakuwa ni sababu tosha kwa Watanzania kufikiria kama kweli watu hawa wana ukweli ndani yao au yatakuwa yale yale ya ya kujikomba tena. Wataanza kutulisha maneno tena kuwa "hawakumaanisha yule" au "hawakumaanisha wale". Walimaanisha wengine wote isipokuwa "wale". Tusije kuona wale wale ambao wanasema "wale" ni mafisadi ndio hao hao wakawa wa kwanza kuimba "tuvunje makundi". Makundi CCM hayawajahi kuvunjwa yavunjwe leo kwanini?
Wakati mwingine utaona ni vizuri kwa CCM kuvunjika hata kupoteza Urais na kukaa pembeni ili labda akili zitawarudia. Na inaweza kuchukua muda kweli akili kuwarudia. KANU ya Kenya ilibidi akae pembeni na ikavunjika kweli lakini ilirudi kwa namna nyingine kabisa na kundi lililomeguka. CCM inabidi iende njia hiyo.
Ni kwa sababu hiyo naiombea sana wang'atane, waumane, wachubuane, na hata ikibidi wavunjane. Ili hatimaye wameguke na kutawanyika huku wakibebeshana lawama wakiwa nje ya madaraka.
Siombei wapatane hata kidogo. Maana wakipatana itakuwa shida nyingine ya miaka mitano. Sioni ni nani anayeweza kuwapatanisha sasa hivi maana walijaribu hata vikao vya mashauriano na madudu gani sijui walishindwa. Sasa wananchi wa kawaida wanafikiria watapatana kwa nini, ili kiwe nini, kwa nani na kwa nini?
Meguka!
MMM
Shida sio CCM kufa kabisa
CCM now ni kama 'dead man walking'
shida ipo kwenye replacement tukishaizika CCM
je wananchi wanaiona na kuiamin replacement?
we umeiiona?
Wengi wetu bado wanaamini kuwa kwa sababu ccm haijabadili logo yake kutoka jembe na nyundo, basi ni chama kile kile chenye kauli mbiu ya "DAIMA NITASEMA KWELI, FITINA KWANGU MWIKO" wakati sasa uongo na fitina ndizo nguzo kuu za chama!vyombo vya dola vitakapoiacha ccm ijiendeshe kisiasa kama chama cha siasa, hapo hapo kitavunjika. ktk hali ilikoifikisha tanzania ni bora na nafuu sana ccm ikivunjika na kutoweka kabisa. hata kwa usalama wa taifa hili ccm haifai tena. ni bora iondoke iwe historia na tz ianze upya. naamini kama taifa tutaendelea zaidi kuliko kuwa tena chini ya utawala wa ccm