CCM itaendelea kutawala Tanzania hadi 2015

acha kashfa wewe!.. Kubali tu watanzania walio wengi! Bado wana mapenzi na ccm!!

Wale Wale

Because hypocrisy stinks in the nostrils one is likely to rate it as a more powerful agent for destruction than it is.
 
Heading yako inaonyesha ni jinsi gani CCM walivyo ma-JUHA wanajua KUTAWALA na si KUONGOZA
 
eu: Ccm imebebwa na vyombo vya dola

elias msuya
mwangalizi mkuu wa wa uchaguzi kutoka jumuiya ya ulaya, david martin amesema chama cha mapinduzi (ccm) kimepata ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu baada ya kubebwa na vyombo vya dola, ikiwemo tume ya taifa ya uchaguzi (nec).

Akitoa taarifa ya awali ya waangalizi hao jana jijini dar es salaam, martin alisema uchaguzi huo, uligubikwa na kasoro nyingi licha kuendeshwa kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa.

Alipoulizwa na mwandishi wa habari wa gazeti hili kuhusu muundo wa tume ya taifa ya uchaguzi kama inatenda haki, martin alisema hilo ameshaligusia katika taarifa yake.

"hilo nimelisema kama umesoma kipengele cha nne cha taarifa yetu utaona kinasema, chama tawala kilinufaishwa na muundo wa utawala thabiti wa vyombo vya serikali ambao kiliurithi kutoka kwenye mfumo wa chama cha ccm enzi za chama kimoja ambao wakati mwingine ulikuwa hautambuliki vizuri," alisema.

Alisema kimsingi idadi kubwa ya viongozi wanaoteuliwa katika vyombo hivyo, wamekuwa wakiteuliwa na rais wa jamhuri ya muungano ambaye pia ni mgombea katika uchaguzi, jambo ambalo linazua maswali kuhusu uhuru wa vyombo vya dola kukisaidia chama tawala.

Alisema ccm kilisaidiwa na vyombo vya dola katika kuendesha kampeni ikilinganishwa na vyama vingine vya siasa.

Kuhusu uhuru wa vyombo vya habari wakati wa uchaguzi, alitaja kitendo cha kutishiwa kufungiwa kwa gazeti la mwananchi kutokana na kutoa taarifa hasi za serikali, alisema ilikwenda kinyume na uhuru wa kujieleza.

"ujumbe wa ulaya wa kufuatilia kwa kina uchaguzi mkuu nchini unadhania kwamba vitisho kama hivyo dhidi ya vyombo vya habari ni jaribio la kuuwekea mipaka uhuru wa kujieleza" alisema martins.

Mapungufu mengine kwa mujibu wa martin ni kuwalazimisha watu kugombea kupitia vyama bila kutumia chama ni kinyume na kanuni za kimataifa.

"sharti hilo, linawanyima watu haki na fursa ya kusimama kugombea hasa wale ambao wangependa kushiriki katika uchaguzi kama wagombea binafsi. Matokeo yake linaiwekea mipaka ridhaa ya wapiga kura,"alisema.
Alisema tume hiyo, imesikitishwa na tabia yake ya kuchelewesha matokeo huku akitilia shaka uwazi katika kazi ya kukokotoa matokeo ya uchaguzi.

"ucheleweshwaji wa kutangaza matokeo ni jambo lililotusikitisha kwasababu jambo hilo, limesabisha mashaka miongoni mwa wapiga kura na wagombea. Pia tuna mashaka na uwazi katika shughuli ya kukokotoa matokeo ya uchaguzi," alisema.

Naye kiongozi wa ujumbe kutoka bunge la ulaya, maria ndelcheva alishangazwa na kutojitokeza kwa wanawake kugombea urais licha ya wanawake hao kujitokeza kwa wingi kupiga kura.

"japo tunaikaribisha hatua ya idadi ya viti vilivyotengwa katika bunge la taifa na katika baraza la mapinduzi, bado tunasikitishwa kutoona wanawake katika vyombo vya kusimia kazi nzima ya uchaguzi wala mgombea urais," alisema ndelcheva.​

tunawajua
 
Kibunango naona kajichimbia mafichoni anaibuka kutoa Thanx na kuondoka ..kaka uko busy sana?:smile:
 
nnawapongeza sana wale wote walioshinda kuanzia wa chama changu na hata wapinzani

bado ccm itaendelea kutawala bara na zanzibar

sasa tupunguze siasa tushirikiane kujenga nchi
Kwa mara ya kwanza mzee wa pumba umetoa point

Nawapongeza sana CCM kwa kulinda na kukwapua kura za urais kwa namna yoyote ile.... pamoja na hayo tutajenga nchi yetu, tusiumize masikini na tuhakikishe kila mtanzania maskini aliyepiga kura bila uelewa wa nguvu na thamani ya uraia wake anapata elimu hiyo ndani ya miaka mitano
 
TAHADHARi

Ndugu zangu wote wa Chadema nataka mjue mimi ni mwanachama wa chadema,na ni mpenda mabadiliko na maendeleo kwa sababu hiyo naomba wale mliozoea kuchallenge kila post kwa kudai umetumwa au unatumia masaburi muache kwenye hii post!

ccm itatawala tanzania mpaka 2020,hiyo imeshafanyiwa kazi na wana ccm nguli na imepitishwa
ccm inamwogopa Dr Slaa kuliko kitu chochote kile,ccm haiogopi chadema kwa lolote lile bali inamwogopa mtu ndani ya chadema,

kazi iliyokwisha fanywa na wana ccm nguli kwa kusaidiana na baadhi ya wapinzani na wanaharakati wanafiki:
tume ya uchaguzi iliyoteuliwa na mwenyekiti wa ccm na kuchagua wana ccm wenzake iliwapa shida sana wana ccm wakiamini wapinzani na wanaharakati watapinga na kuzua migogoro kutaka iundwe tume huru ya uchaguzi,lakini hiyo imepita na ccm ni washindi kwenye hilo,
hakuna katiba mpya mpaka 2017,kwa sababu hiyo ccm watachukua madaraka 2015 na ndio maana unaona wanagombania nafasi ya urais,walishajua kinachoendelea,
kesi ya katiba iliyofunguliwa imewafurahisha sana wana ccm kwani walitegemea hilo na ndio sababu kubwa ya kikwete kuwa jeuri na kusaini muswada wa katiba kwa mbwembwe huku akijua una kasoro,
Dr Slaa ambaye ni tishio kwa ccm atashindwa uchaguzi 2015 kwa sababu ya tume ya uchaguzi na katiba mbovu,kwa hilo ccm wamepatia ,
mara baada ya uchaguzi wa 2015 wana ccm wengi wanaoshutumia hawatapita kama wabunge,kwa sababu hiyo watawekwa pembeni kiaina na wana ccm wenzao bila kuwadhalilisha,,,isue ya rostam azizi kujiuzulu ni haraka zake na imekula kwake!
baada ya 2015 tishio la ccm ambaye ni Dr Slaa hataweza tena kugombea 2020 kwa sababu ya umri,
wamemwona zito kabwe hawezi kabisa kuwa tishio kwa ccm kwa sababu ni kigeugeu na ni rahisi sana wananchi kupoteza imani naye,
lema amekuja juu wamedai ni moto wa kifuu utazimwa na watu hawataamini,
baada ya 2015 ccm itahakikisha imejisafisha na kuhakikisha imenyoosha mapito yake yanayopigiwa kelele na wengi,
kwa kufanya vile wanaamini mambo yao yote yatakuwa safi na watatawala milele!!!!!!!!

hiyo imetoka jikoni na bado ni ya moto,kazi kwenu wapenda mabadiliko!!
 
hata chadema wakitawala kutakua na sura nyingi za wana ccm wa sasa.ni kwamba watabadilisha chama watu watakua walewale.kumbuka dr slaa alikua ccm,maalim seif n.k.
KANU ilipigwa chini lkn viongozi wengi kenya ni walokua kanu na si kanu inatawala
 
nnawapongeza sana wale wote walioshinda kuanzia wa chama changu na hata wapinzani

bado ccm itaendelea kutawala bara na zanzibar
sasa tupunguze siasa tushirikiane kujenga nchi

Yeah,inawezekana hilo likatokea lakini lazima ifanyike kazi kubwa sana kuyafanya maneno hayo yakamilike,la sivyo chochote chaweza tokea
 
We mleta mada usifikirie kirahisi rahisi hivyo,tulioichoka ccm ni wananchi sio chadema,kwa maana hiyo basi tutakuwa tayari kwa lolote full stop.
 
TAHADHARi

Ndugu zangu wote wa Chadema nataka mjue mimi ni mwanachama wa chadema,na ni mpenda mabadiliko na maendeleo kwa sababu hiyo naomba wale mliozoea kuchallenge kila post kwa kudai umetumwa au unatumia masaburi muache kwenye hii post!

ccm itatawala tanzania mpaka 2020,hiyo imeshafanyiwa kazi na wana ccm nguli na imepitishwa
ccm inamwogopa Dr Slaa kuliko kitu chochote kile,ccm haiogopi chadema kwa lolote lile bali inamwogopa mtu ndani ya chadema,

kazi iliyokwisha fanywa na wana ccm nguli kwa kusaidiana na baadhi ya wapinzani na wanaharakati wanafiki:
tume ya uchaguzi iliyoteuliwa na mwenyekiti wa ccm na kuchagua wana ccm wenzake iliwapa shida sana wana ccm wakiamini wapinzani na wanaharakati watapinga na kuzua migogoro kutaka iundwe tume huru ya uchaguzi,lakini hiyo imepita na ccm ni washindi kwenye hilo,
hakuna katiba mpya mpaka 2017,kwa sababu hiyo ccm watachukua madaraka 2015 na ndio maana unaona wanagombania nafasi ya urais,walishajua kinachoendelea,
kesi ya katiba iliyofunguliwa imewafurahisha sana wana ccm kwani walitegemea hilo na ndio sababu kubwa ya kikwete kuwa jeuri na kusaini muswada wa katiba kwa mbwembwe huku akijua una kasoro,
Dr Slaa ambaye ni tishio kwa ccm atashindwa uchaguzi 2015 kwa sababu ya tume ya uchaguzi na katiba mbovu,kwa hilo ccm wamepatia ,
mara baada ya uchaguzi wa 2015 wana ccm wengi wanaoshutumia hawatapita kama wabunge,kwa sababu hiyo watawekwa pembeni kiaina na wana ccm wenzao bila kuwadhalilisha,,,isue ya rostam azizi kujiuzulu ni haraka zake na imekula kwake!
baada ya 2015 tishio la ccm ambaye ni Dr Slaa hataweza tena kugombea 2020 kwa sababu ya umri,
wamemwona zito kabwe hawezi kabisa kuwa tishio kwa ccm kwa sababu ni kigeugeu na ni rahisi sana wananchi kupoteza imani naye,
lema amekuja juu wamedai ni moto wa kifuu utazimwa na watu hawataamini,
baada ya 2015 ccm itahakikisha imejisafisha na kuhakikisha imenyoosha mapito yake yanayopigiwa kelele na wengi,
kwa kufanya vile wanaamini mambo yao yote yatakuwa safi na watatawala milele!!!!!!!!

hiyo imetoka jikoni na bado ni ya moto,kazi kwenu wapenda mabadiliko!!

ndio mnavyo jifariji eeh?
 
Tatizo la wana jf ni ushabiki. Kwenu ukweli hauna maan.kilicho na maana kwenu ni kuambiwa mnachopenda kusikia. Lakini ukweli chadema hawana watu makini wa kuaminiwa na watanzania mpaka wapewe nchi? Ubunge mtapata lakini Ikulu ya magogoni mtaendelea kuiona kwenye runinga.
 
Back
Top Bottom