CCM Inajiandaa kukabidhi nchi kwa CHADEMA-Lwaitama

Mhadhiri mwandamizi mstaafu wa chuo kikuu cha DSM Dr Azaveli Lwaitama amesema vitendo vya kinyama vinavyofanywa sasa na Jeshi la polisi dhidi ya CHADEMA vinaashiria kukaribia kuingia Ikulu kwa chama hicho.

Dr Lwaitama amelaani vitendo vya kinyama vilivyofanywa na polisi vya kupiga watu kikatili,kupiga risasi za moto na kupora mali za raia.

Dr Lwaitama kasema CCM sasa imeshindwa siasa za majukwaani na badala yake wameamua kutumia jeshi la polisi kujihami dhidi ya CHADEMA.

Dr Lwaitama amesema kiashirio tosha kwamba CCM sasa imefikia ukingoni ni matokeo ya uchaguzi wa udiwani wa kata 22 uliopita ambapo ingawa CCM ilipata viti 16 na Chadema 6 Lakini kura za Jumla zinaonyesha Chadema imeizidi CCM ambapo CCM imejikusanyia kura 17968 na CHADEMA kura 18431.Vyama vingine ikiwemo CUF vilipata Jumla ya kura chini ya 1000.

Dr Lwaitama amesema kama ingekuwa ni uchaguzi wa Urais basi CHADEMA ingekuwa imeshinda.Pia amesema haya yote yamefanyika huku maelfu ya vijana wafuasi wa Chadema wakiwa bado hawajaandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa hujuma ya CCM na ushirika wa Tume ya Uchaguzi.

Source:MAWIO UK 2

Mkuu, siku zote ukiona mtu ana act with paranoia basi juwa huyo siku zake za kusihi duniani zinayoyoma.
 
Asante sana Kyamtundu...
Mimi mwenyewe nilikuwa kilaza kwenye hizi takwimu japo nimekuwa nafuatilia sana.. Asante kwa kunifungua macho, hapa tuko sawa meen.. Bado kata za Arusha zitaongeza idadi ya kura hapo.
Hawa jamaa wa MAGAMBA kuna wakati vichwa havifanyi kazi...
Hata hivyo tunahitaji kukutana ili tujue 2014 tunajiandaaje kuchukua nchi toka kwa Manyang'au!
 
Kwani wa chadema ni watawala? Subiri 2015 watakapochukua mjengo uone watatua kwa asilimia ngapi!
 
watakupiga tuh,
namimi nasema wakupige tuh kwa sababu sasa sina namna nyingine,,

eeh,,maana sasa nimechoka sasa...

Tehe!
Amechoka kuzomewa huyo!
Amechoka kulazimisha uchumba!
Amechoka kujenga hoja!
Hata akili imechoka!
Huyu si kingine,..
ILA,KACHOKA TU!
 
Katika mazingira yaliyopo CCM IMESHAANZA kuachia nchi kwa cdm na Ukawa

Malumumba buku sabasaba njoni mbishe

KUB Safi kwa kuhakikisha nchi inarejea katika mapigo ya moyo ya kawaida
 
Kipindi hiki watanzania tumeamka,hatuchagui chama ili tusijerudia makosa.Sasa hivi tunachagua watu wenye uwezo.
 
Katika mazingira yaliyopo CCM IMESHAANZA kuachia nchi kwa cdm na Ukawa

Malumumba buku sabasaba njoni mbishe

KUB Safi kwa kuhakikisha nchi inarejea katika mapigo ya moyo ya kawaida

Wewe utakuwa umepata ugonjwa fulani. Tukabidhi nchi kwa DJ, are you serious?. Tuliuliza juzi hapa embu basi tutajieni safu ya viongozi kwa kuanzia ambao wanaweza ongoza serikali, mkashindwa. Hivi unafikiri nchi inafanyiwaga majaribio kama kichwa chako kinavyokutuma? Tafadhali bwana wananchi tumeshastuka. Hatuendekezi masiasa yenu uchwala hayo yasiyo na mbele wala nyuma. Katafuteni nchi yenu muifanyie majaribio.
 
Kipindi hiki watanzania tumeamka,hatuchagui chama ili tusijerudia makosa.Sasa hivi tunachagua watu wenye uwezo.

Well said kamanda. Watanzania nadhani wakati umefika wa kujenga utaifa sasa. Hizi siasa uchwara zitazidi kutupoteza, vyama vyenyewe vinashindwa hata kutumia ruzuku tuu, eti ndio vikabidhiwe nchi, yarabi toba. Mswalieni mtume jamani, wajameeeni tubadilike
 
Wewe utakuwa umepata ugonjwa fulani. Tukabidhi nchi kwa DJ, are you serious?. Tuliuliza juzi hapa embu basi tutajieni safu ya viongozi kwa kuanzia ambao wanaweza ongoza serikali, mkashindwa. Hivi unafikiri nchi inafanyiwaga majaribio kama kichwa chako kinavyokutuma? Tafadhali bwana wananchi tumeshastuka. Hatuendekezi masiasa yenu uchwala hayo yasiyo na mbele wala nyuma. Katafuteni nchi yenu muifanyie majaribio.

Nilikuwa nazungumza kama wewe hvohvyo kwa kukipenda chama changu ila huu upepo hatuwezi kuuzuia acha tu upinzani utakeover....
 
Naanza kuamini Mbowe ni prof.wa siasa nchini, anajua kutumia fursa hongera Kamanda wa anga.
 
Wewe utakuwa umepata ugonjwa fulani. Tukabidhi nchi kwa DJ, are you serious?. Tuliuliza juzi hapa embu basi tutajieni safu ya viongozi kwa kuanzia ambao wanaweza ongoza serikali, mkashindwa. Hivi unafikiri nchi inafanyiwaga majaribio kama kichwa chako kinavyokutuma? Tafadhali bwana wananchi tumeshastuka. Hatuendekezi masiasa yenu uchwala hayo yasiyo na mbele wala nyuma. Katafuteni nchi yenu muifanyie majaribio.

Kuna kitu ambacho nilianza kukihisi kabla na sasa naanza kuona kinajidhihirisha. Chadema ni wabinafsi sana,kila unapokuta mada ya inayozungumzia utwaaji wa madaraka utasikia chadema inajiandaa kuchukua nchi ilhali chadema wako ndani ya ukawa na ukawa bado hawajakubaliana nani atapeperusha bendera kwa niaba ya wenzao. Na kwa mwendo huu inavyoonesha endapo mgombea urais wa ukawa atatokana na chama kingine tofauti na chadema,HAKIKA UKAWA ITASAMBARATIKA
 
Back
Top Bottom