CCM ina bahati sana Kumpata Kinana, Mwigulu

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
579
CCM ina bahati kuwapata Kinana,Mwigulu

Na Angela Kiwia

KATIKA kipindi cha mwaka mmoja sasa tumeweza kuona ni kwa jinsi gani viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walivyoweza kusimama kidete katika kumtetea Mtanzania kupatiwa haki yake ya msingi kuanzia ngazi za vijijini.

Tumeweza kumshuhudia Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana jinsi ambavyo ametumia muda mwingi tangu alipochaguliwa kushika wadhifa huo mkubwa katika chama akitembelea mikoa na hata kata mbalimbali nchini ili kusaidia kwa njia moja kutafuta ufumbuzi wa kero zinazowakabili.

Kinana ameonekana na kusikika akiwakemea watendaji katika Serikali iliyopo madarakani kwa kutotimiza majukumu yao ipasavyo hivyo kuwaagiza kufanya hivyo ili kuweza kuongeza tija kwa taifa.Kinana amekuwa ni mwanga mkubwa katika siasa za sasa kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Pamoja na juhudi hizi zinazofanywa na Kinana, pia tumeweza kushuhudia jinsi naibu wake ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba anavyopambana kwa upande mwingine kuhakikisha kila Mtanzania anapata haki yake ya msingi.

Haya katu si mambo ya kubeza katika kipindi hiki na kizazi cha dot com. Kinana na Mwigulu wameweza kudhihirisha kuwa CCM haikufanya makosa katika kuwateua kushika nyadhifa zao hizo.Katika kikao kilichofanyika mkoani Dodoma Mwigulu alionyesha msimamo wake kuhusiana na sakata la uchotwaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Mwigulu alijitokeza na kusema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ameshamaliza utata hivyo, mali zote, fedha zote za IPTL zikamatwe na wahusika wote wakamatwe.Alibainisha kuwa- haiwezekani watu wakawajibika tu kwa kujiuzulu kwa kuwa ni sawa na kutoa likizo- kwa watuhumiwa wa uchotwaji fedha hizo ili kwenda kuzitumia watakavyo.

-"CAG ameshasema pesa zile zilikuwa mali ya umma, sasa zikamatwe zote na wahusika wote wakamatwe na kufilisiwa mali zao, hizi ni fedha za umma haziwezi kupotea hivi hivi tunaangalia" alisema Mwigulu.

Pamoja na msimamo huo, alienda mbali zaidi na kubainisha kuwa katika orodha hiyo wapo watu ambao- walishastaafu na wamehusika kulihujumu taifa wakamatwe na akaunti zao zikamatwe na zifilisiwe ili kurudisha fedha kwa wananchi.

Huu ni ujasiri wa hali ya juu, kitendo chake cha kuonyesha msimamo wake katika suala hili na kutetea maslahi ya umma ni jambo la kujivunia kutoka kwa kiongozi huyu.Tunatambua ya kuwa wapo baadhi ya viongozi tulionao ambao katu hawathubutu kufungua mdomo kukemea maovu, siku zote vipaumbele vyao ni wao na familia zao.

Tunalo la kujivunia kutoka kwa Mwigulu katika kutetea kile kilicho cha Mtanzania.Katika kuhakikisha anakuwa mstari wa kwanza kutekeleza majukumu yake aliweza kumuagiza Kamishna Mkuu wa Idara ya Mapato nchini (TRA) kumchukulia hatua mtumishi wa TRA ambaye anatuhumiwa kupatiwa mgawo wa fedha kutoka IPTL.

"Naagiza- mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambaye anatuhumiwa kuchota Sh1.6 bilioni za akaunti hiyo afukuzwe kazi, akamatwe na akaunti zake za fedha zifilisiwe ili fedha irudi serikalini"

"Tazama wanafunzi, watoto wa maskini zaidi ya elfu 40 wamekosa mikopo, madawa hospitalini hakuna, maskini wanakufa, watu wasio na hatia wanafungwa kwa kukosa michango ya maabara, walimu wanadai fedha zao, wazabuni wanauziwa nyumba zao na benki huku wakiidai Serikali kwa huduma walizotoa, leo wezi tuwape adhabu ya kujiuzulu? Tuwape likizo ya kwenda kutumia fedha walizo waibia maskini?"

-"Nimemwagiza Kamishna wa Kodi amfukuze kazi yule mtumishi wa TRA iliyoko chini ya wizara yangu na afilisiwe, pia mitambo na kodi vikamatwe na wahusika wakamatwe.Hatuwezi kuendeleza mazoea ya kufunga maskini na kuwapa likizo wezi wakatumie fedha. Walio serikalini na walioko kwenye siasa wakamatwe na tuwafilisi fedha irudi serikalini," Mwigulu alisisitiza.

Mwigulu na Kinana wameweza kujitofautisha na aina ya viongozi waliokabidhiwa madaraka ambao wamevimba vichwa vyao huku wakiuvimbisha- ubongo wao na kuanza kuwatukana Watanzania kwa kuwabeza kuwa wanastahili kuuza juice na matunda huku wakipata kiburi kutokana na udalali wao kwa makaburu na wanyonyaji wa masikini wa nchi yetu.

Wamekubali kuwachefua wananchi kwa kuhongwa mabilioni ya fedha, wanakwenda kugawana kwa sandarusi na lumbesa. Viongozi wanaojifanya wasomi wamejikuta wakikubali kuwa watwana kwa wababaishaji huku wakikipaka matope chama kutokana na tamaa zao binafsi.

Waswahili husema, mtu mwongo mpe tu kamba ndefu mbele ya safari atajinyonga kwa mikono yake mwenyewe. Tumeweza kuona ni kwa jinsi gani baadhi ya wanaotuhujumu wanavyojinyonga wenyewe kutokana na kuvuna wanachokipanda.

Tunalo deni, deni kubwa la kuhakikisha tunaunga mkono msimamo wa Mwigulu kwa kudai fedha zetu walizokwapua na kuwachukulia hatua stahiki wale wote walioshiriki katika ukwapuzi huu.

Tanzania ni yetu sote, tunalo jukumu la kuilinda pamoja na raslimali zake, tusiwaachie wababaishaji na wezi kutulaghai na kuichafua nchi yetu huku wakishibisha matumbo yao yasiyoridhika kutokana na jasho letu.

Tusimame kwa pamoja kuukataa udharimu huu, tuanze sasa hata kama tumechelewa.Tunaweza wote kuokoa kilicho chema kabla jua halijazama.

Tuungane na wale wote wenye uchungu na mali zetu bila kujadi itikadi zetu, Tanzania nchi yetu haina itikadi bali sisi watu wake ndiyo wenye itikadi.Tuungane kutokomeza umwinyi na umimi, upuuzi na usomi uchwara uliojaa kauli za kifedhuri zisizo na jembe ya majuto.


Chanzo:Dira (01.12.2014)
 
jamani acheni kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa wenzenu,,,ccm wote ni mafisadi,,kama ambavyo mmeiba 320 bil,,,,mtanzania gani waliyemtetea,si tungewasikia kwenye sakata la eacrow,,
 
2005- Tembo 130000

2014-Tembo 5000

Tushukuru watu aina ya kinana yupo mmoja wangekuwa wawili tu ingekuwa historia
 
Back
Top Bottom