CCM imekosa DIRA?

Mshiiri

JF-Expert Member
Jun 16, 2008
2,012
509
Democracy is not about voting but mainly counting! If to CCM, democracy is about voting and this shows evidently in many occasions; they are absolutely wrong since democracy is counting fairly the votes and agree to it accordingly. That is outside the box thinking and implication about democracy. Lets review is sisiemu doing fair to be granted 2010 election victory again?

My signature remains valid
 
Vyama vya upinzani havikuwahi kuwa na dira, havina dira na hakuna dalili kama vitakuwa na dira katika miaka michache ijayo.
 
Vyama vya upinzani havikuwahi kuwa na dira, havina dira na hakuna dalili kama vitakuwa na dira katika miaka michache ijayo.

But hii haimanishi kukosa kukubali mabadiliko! We must advance and change. CCM preaches the same verse "Vyama vya upinzani havikuwahi kuwa na dira, havina dira na hakuna dalili kama vitakuwa na dira katika miaka michache ijayo" wakati inaiba na kukandamiza vyama pinzani kwa kutumia vyombo vya dola. Mfano mzuri Zanzibar na hata jumuiya ya kimataifa ilishuhudia hivyo. A lot of mishaps. Kama ikiwa vyama pinzani havina dira why then allow a dictatorship multipartism. Ili tu ku-comply na wafadhili. It is a shame. Actually ni kukosa DIRA kwa kiasi kikubwa na it is a great lie kwamba vyama pinzani havina dira, CCM ni architect wa wao kuonekana walivyo.

Kwanza ni hivi majuzi tu na nampongeza sana Mheshimiwa Spika Sitta kwa kuonyesha demokrasia iliyotukuka bungeni kwa kuruhusu watu wote kusikika bila kujali itikadi tofauti kabisa na Mr. Msekwa. It is a change that we pray on every other day.
 
Je CCM ni chama cha Kibepari, Kikomunisti, Kisoshalist, kiliberali, kiislam? CCM ni chama kinyonga na kila mahali kipo (katika hizo siasa tano juu)!! Ni kweli kuwa hata upinzani huoni sera hasa, lakini ni hatari kwa chama kinachoongoza serikali kukosa dira.

Upinzani haujawahi kuwa explicit kwenye mambo kama ubinafsishaji wa mali za umma, Uendeshaji wa uchumi, mambo ya nje, n.k. Vyama vya upinzani kwenye sera nyingi vinafanana na CCM; ila vina ahidi kutekeleza vizuri zaidi kuliko CCM. Ndo huwezi kuchora mstari wa wapiga kura. Wapiga kura siku zote wako confused na pole pole wataanza kupigia kura dini, makabila, n.k.

sera hata kama zipo, hazitekelezeki au wanaozisema hawatekelezi kile wanachosema. Kwa hiyo huo ni ukweli mtupu kuwa CCM hakina dira wala mwelekeo, kinaongozwa na matukio!! Hata vyama vya upinzani vinaongozwa na matukio vile vile!
 
CCM kama chama kinayo dira,ila haitekelezwi ipasavyo[haifuatwi].
ndio maana hata wakati wa uchaguzi uliopita chama kilikuwa na ilani ya uchaguzi lakini tulishuhudia wagombea wao[akiwamo mgombea wa urais]akitangaza sera[ahadi?]ambazo hata kwenye ilani hazikuwepo.
sasa sijui linapokuja suala la utekelezaji wa wa ahadi baada ya uchaguzi kipaumbele kinakuwa kwenye ilani ya chama au ahadi binafsi za mgombea?
na hapo ndio mkanganyiko mkubwa unapoptokea mpaka kudhani kuwa chama hakina dira,dira ipo ila viongozi hawaifuati[au inawashinda kuifuata kwa kuwa labda inakinzana na malengo yao--binafsi]
hatahivyo bado CCM ina wanachama waadilifu wengi ambao kwa sababu moja au nyingine[nguvu ya mtandao?]wamekosa nafasi ya kukitumikia chama,lakini ipo siku,nayo haipo mbali,nguvu ya mafisadi haiwezi kudumu sana na inaelekea kuvunjika.
 
Chama ukiona kinaingiziwa katika ilani mahakama ya kadhi na akina "Dr" Ngasongwa mtu anatakiwa kuwa msomi na anapenyeza udini , basi ujue kinaishia kufilisika kisiasa.
Kwa wale wapenzi wa chama tulio mlengo wa kushoto, we can see the dying signs
 
CCM nakubali haina dira kwa maana kwamba si soshialisti, conservative, liberal demokrats au hata communist. Lakini ukitazama kwa makini nchi nyingine nyingi duniani utabaini kwamba nao siasa zao ni "blurred". Hakuna zenye sera ambazo ni clear-cut soshialisti au conservative.

Madhumuni ya chama cha siasa hatimaye ni kuongoza nchi ili kutatua matatizo ya kijamii na kuleta maendeleo. Hapo mwanzo CCM ilijieleza kwa ufasaha kabisa na wananchi walikubali kuipa kura wakiwa na matumaini kwa vile uongozi ulikuwa unaonyesha uadilifu na uzalendo WaTz wakitumaini kunufaika na uongozi wao. Exit Mwalimu! dira ya chama ikaanza kuelekea mifukoni na matomboni mwa viongozi.

Vyama vya siasa vya upinzani haviwezi kuwa na sera ambazo zitapinga madhumuni basic ya kuongoza nchi ili kuharakisha utatuzi wa matatizo ya maendeleo ya jamii. Hatuwezi kutegemea kwamba chama kitaibuka na kusema kinataka kuleta ubepari pure and simple au ukomunisti pure and simple. Itikadi hizo zimekwisha kuwa watered down, na siasa mamboleo ni mchanganyiko.

Kunaweza kuwa na tofauti baina ya vyama vya siasa katika msisitizo wa jinsi ya kuharakisha maendeleo na kuendeleza raslimali za nchi. Kwa mfano, chama kimoja kinaweza kusisitiza madini yamilikiwe na umma au wananchi kwa asilimia kubwa, ambapo chama kingine hakitii maanani mfumo wa umilikaji. Lakini kwa jumla vyama haviwezi kutofautiana sana.

Uchaguzi unapoandaliwa, wananchi watatakiwa kuamua ni uongozi wa chama kipi unaweza kutuletea maendeleo. Kipimo kitakuwa ni kuangalia uadilifu, uzalendo na umahiri wa kueleza misimamo vya hivyo vyama. Kwa sasa CCM imedhihirisha kuvamiwa na uongozi usiosita kupokea au kula rushwa, ama hata kuchukua hatua za kukomesha au kuizuia. Huko sio tu kukosa dira, bali ni kuchoka kutawala. Wapishe upinzani.
 
CCM haina Dira wala mwelekeo inaongozwa na hisia za mtu mmoja na busara za mtu fulani ndio maana leo tumefika hapa tulipo. Leo toka Mwalimu Nyerere afa ameondoka na CCM yake ya asili. Kuna mabaki ya CCM
 
CCM kama chama kinayo dira,ila haitekelezwi ipasavyo[haifuatwi].
ndio maana hata wakati wa uchaguzi uliopita chama kilikuwa na ilani ya uchaguzi lakini tulishuhudia wagombea wao[akiwamo mgombea wa urais]akitangaza sera[ahadi?]ambazo hata kwenye ilani hazikuwepo.
sasa sijui linapokuja suala la utekelezaji wa wa ahadi baada ya uchaguzi kipaumbele kinakuwa kwenye ilani ya chama au ahadi binafsi za mgombea?
na hapo ndio mkanganyiko mkubwa unapoptokea mpaka kudhani kuwa chama hakina dira,dira ipo ila viongozi hawaifuati[au inawashinda kuifuata kwa kuwa labda inakinzana na malengo yao--binafsi]
hatahivyo bado CCM ina wanachama waadilifu wengi ambao kwa sababu moja au nyingine[nguvu ya mtandao?]wamekosa nafasi ya kukitumikia chama,lakini ipo siku,nayo haipo mbali,nguvu ya mafisadi haiwezi kudumu sana na inaelekea kuvunjika.

Hahahaaa,

Hii ni sawa na kusema, gari hii inajua inakoenda, ila madereva ndo hawajui njia wanaipeleka gari isikotaka. I mean, chama ni uongozi na wanachama. Uongozi ndio unaotoa mwelekeo na wanachama wanauunga mkono. Sasa uongozi ukiwa hauna dira, ni vigumu kusema chama kina dira!!! Yaani gari inajua inakoenda, ila dereva mbaya?
 
Lugha yako ya picha ili isitafsirike vibaya ni kuwa wananchi wanajua uongozi bora, I mean wananchi wana standards na quality za uongozi bora na wenye adili, lakini hawa jamaa hawafuati adili baada ya kuchaguliwa. Hawa jamaa huja na hoja nzuri sana ambazo kutokana na kwamba hawana dira wala mwelekeo hawatekelezi ahadi zao. Huapa kwa unafiki na kumdanganya mola wetu na pengine hiyo ndio kubwa kuwa Mungu atuadhibu wote katika collective liability kwa kuwa na viongozi wabaya na wabovu ambao tunawaweka madarakani tena na tena.

Pili wachaguliwapo hupenda kukaa mbali na wananchi wao na kuishia Dar es Salaam kufanya ufisadi na biashara. Kama wanataka kuwa wafanya biashara na wawe wafanyabiashara na sio kuja kurubuni wananchi. Hurudi tu majimboni wakikukmbushwa kuwa term yao imeisha na itabidi ku-defend title, ukadanganye tena na kuuwa albino then back to Dar again. Ni kamchezo kao kachafu. Actually ni wapumbaf sana
 
Ni wazi kwamba CCM ilikwishapoteza dira siku nyingi. Hili halina mjadala. Mambo mengi nchini yanaenda shagala bagala (sijui shaghala baghala?) kwa sababu viongozi wa juu wanawakumbatia matajiri na kuwasahau wakulima na wafanyakazi, ambao ndio hasa mhimili wa chama. Lakini vyama vya upinzani navyo vimeshindwa kutumia udhaifu wa CCM kujijenga kwa wakulima na wafanyakazi na hivyo kuvunja nguvu za chama hiki cha mafisadi.
 
CCM ilishapoteza dira ya kuongoza Tanzania siku nyingi sana. Kwa sasa dira iliyonayo ni ile ya kuangalia ni jinsi gani itabakia katika madaraka, kuendeleza ufisadi na kutetea status quo ya watawala na vizazi vyao. Wamesahau kabisa maslahi ya mwananchi wa kawaida, na yale machache yanayofanyika ni kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wanabakia madarakani.
 
Sasa hivi ni busara za mwenyekiti, sasa hivi ndio CCM ni CHAMA CHA MWENYEWE CCM) na wewe na mimi sio mwenyewe, ni RA, MAKAMBA, EL na wengine kibao
 
Dira itoke wapi wakati ni utawala wa kambare -- kila mtu ana sharubu? Kila mtu ni msemaji, kuanzia Ikulu ambapo hadi sasa msemaji hajulikani, Ni Salva, Premy, Mkuchika, Mshana (Mkurugenzi Maelezo) au Sofia Simba?

Au ni Rostam na Manji -- na mapapa wengine ambao utawala inawaogopa na kutowagusa -- lakini iko tayari kumuandama mzalendo RM? Kweli utawala umekaa hovyo hovyo kama vile alivyosema Zitto kuhusu Waziri mmoja. Majority ya mawaziri wako hivyo hivyo -- ubabaishaji umewatawala kwa kiasi kikubwa.
 
CCM haina Dira wala mwelekeo inaongozwa na hisia za mtu mmoja na busara za mtu fulani ndio maana leo tumefika hapa tulipo. Leo toka Mwalimu Nyerere afa ameondoka na CCM yake ya asili. Kuna mabaki ya CCM

Huyo mtu kwa sasa ni nani?? Au anamaanisha kwa sasa mabo yanajiendea kivyakevyake tu. Mali haina nahodha!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Democracy is not about voting but mainly counting!

If democracy is not about voting but counting, try achieving democratic ideals by counting the stars.
 
Vyama vya upinzani havikuwahi kuwa na dira, havina dira na hakuna dalili kama vitakuwa na dira katika miaka michache ijayo.

Si kweli kama vyma vya upinzani havina dira. Angalia CHADEMA angalia CUF, unaweza kuona ni vyama ambavyo vina dira, labda useme dira yao huipendi ila unaipenda ya chama Kingine. Na dira inaweza kuwa general, ukienda kwenye specifics unaweza kuwa suprised.
 
If democracy is not about voting but counting, try achieving democratic ideals by counting the stars.

Why should he count the stars?
bs'e as per my knowledge,there must always be a meaning/reason to whatever we are doing!now,what is the point with counting the stars?
 
Back
Top Bottom