CCM Ifanyiwe Marekebisho?!

wakati huu si majaribio na nchi yetu hATUWEZI KUMPA MTU TUSIEMUAMINI KUTUONGOZA HATUKO TAYARI KUWA KAMA YALIOTOKEA KENYA.

NI CCM PEKEE KWA SASA NDIO INAYOWEZA KURUVUSHA

Unapopata mawazo kama haya unafikiri sasa kule vijijini ambao hawawezi wengi wao kuingia kwenye mitandao mawazo yao yatakuwaje tena hawajaweza kuona mengi LIVE kwani wanaona kwenye Luninga tu na sinema. Kweli kazi ni kubwa.
 
lako hilo, utaranda randa nalo, ss tunajiandaa kutoa somo 2010

We ndiyo uko out of touch kabisa!

Kwa taarifa kuna azimio moja la Watanzania kutoichagua CCM na hili ni serious kama huna habari!

Mi nasikiliza tu CCM watafanya nini this time!

Lakini kwasababu sipendi kuona machafuko..Kwani CCM they will fight hard!

Which to me is a wrong decision since the only thing they will rely on is the law enforcements which favors them all the time!

Pamoja na tume inayojiita "HURU" ya uchaguzi wa "CCM"

Kwasababu hiyo basi ndio maana nikaamua kuanzisha mjadala huu!

Kama madai yako CCM itapeta 2010 kama haitafanya mabadiliko yanayoendana na utangulizi wangu kwenye first post...

Then unaweza kuwa unaota ndoto za mchana saa 6
 
Hivi ni vitisho vinavyotolewa na watu waliofilisika kisiasa. Tanzania itaendelea kuwa imara hata baada ya CCM kuzikwa.

Ujumbe huu ni kwa wale wana CCM waliokerwa na ufisadi na kuukemea on the open: Dk Harrison Mwakyembe, Aloyce Kimaro, Judge Joseph Sinde Warioba, Joseph Butiku etc etc;

Msikubali kuzuiwa na maslahi ya Chama chenu inapokuja kujiunga na COALITION ya watanzania kwenye kuweka Historia kwenye Taifa letu!

Hili ni badiliko jengine CCM walizingatie otherwise maneno niliyoya highlight yatakuwa kweli!

NB: Shukrani za pekee pia ziwaendee wazalendo hawa ambao hawako kwenye siasa lakini wanashare uchungu wa taifa letu!
Methedous Kilaini

R. Mengi pamoja na Masheick wote Tanzania nzima bara na visiwani pamoja na taasisi zisizo za kiserikali!

TUNAOMBA MUENDELEE KUSIMAMA UPANDE WA WANYONGE HATA KAMA WENGINE WENU NI CCM! THIS IS A DEFINING MOMENT IN THE HISTORY OF OUR COUNTRY AND GOD WILLING YOU WILL BE VICTORIOUS HENCE GO DOWN IN THE HISTORY OF THIS NATION, INFRONT OF THE NEXT GENERATION AND ABOVE ALL INFRONT OF OUR ALMIGHTY GOD!
 
iko wazi bila ya ccm imara tanzania yetu itayumba

Tanzania tayari inayumba chini ya utawala wa CCM na ndio maana halisi ya thread hii! Kama hawatazingatia ushauri huu..Mark my words CCM ITAZIKWA! Na muda si mrefu nitaanzisha thread ya "BURIANI CCM"

Na hatuna rais madhubuti kwasababu anabanwa pamoja na mambo mengine CCM!

Na kuna Azimio la Watanzania wa kila aina kuwaondoa CCM madarakani..Kutokana na hilo naomba husiidharau hii thread kwasababu CCM wana nafasi ya kufanya something kama nilivyoelezea hapo awali?

Nani amkamate nani?
 
Jmushi
Unachekesha sana .Unasema CCM wafanyeje?Mimi naungana na wote wanaosema CCM ife au isambaratike kabisa ni Joka baya sana .
 
Jmushi
Unachekesha sana .Unasema CCM wafanyeje?Mimi naungana na wote wanaosema CCM ife au isambaratike kabisa ni Joka baya sana .

Ni kweli Lunyungu..Watanzania inaelekea wame amka!
 
lako hilo, utaranda randa nalo, ss tunajiandaa kutoa somo 2010

Talking about somo?
Cheki hapo chini then niambie somo gani unalo uchaguzi mkuu wa 2010!


…CCM yatikisika

na Salehe Mohamed



HATUA zinazochukuliwa na Chama cha Wananchi (CUF) na kauli zinazotolewa na watu kadhaa mashuhuri baada ya kukwama kwa mazungumzo ya kusaka suluhu ya mpasuko wa kisiasa visiwani Zanzibar, vimeanza kukitikisa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Ushahidi wa hilo ni jinsi chama hicho kinavyoibuka na kauli tofauti kila kukicha kuhusiana na suala hilo.
Jana, mwanasiasa na kada maarufu wa CCM, Kingunge Ngombale-Mwiru, naye aliibuka kumjibu kada mwingine wa CCM, Jaji Joseph Warioba, akimshangaa kutoa kauli inayokikosoa chama chake kuhusiana na mazungumzo wakati yeye (Warioba) ahusiki katika mazungumzo hayo.
Katika kile kinachoweza kutafsiriwa kuwa ni kijembe dhidi ya Warioba, ambaye amewahi kuwa waziri mkuu, Kingunge alidai kuwa Jaji Warioba hakijui chama hicho.
Kauli hiyo aliitoa jana mjini Dar es Salaam, alipokuwa akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kujua ni kwa nini CCM haitaki kufuata ushauri wa baadhi ya wanachama wao, akiwemo Warioba, kuhusu kuanzisha serikali ya mseto visiwani Zanzibar.
Katika swali lake mwandishi huyo, alisema Warioba amekuwa akisema suluhu ya Zanzibar itapatikana kwa kuwa na serikali ya mseto baina ya CCM na CUF, jambo ambalo linaonekana kuwa gumu zaidi kukubaliwa na CCM.
Kingunge alisema Warioba hivi sasa haingii katika vikao mbalimbali vya chama hicho, hivyo si sahihi kwake kuanza kutoa maneno ambayo hayakujadiliwa na vikao vya chama, hasa suala la mazungumzo ya Zanzibar.
“Ni kweli yeye ni mwanachama wa siku nyingi wa CCM lakini hapaswi kuanza kuzungumza mambo asiyoyajua… mbona mwenzake Kawawa amenyamaza kimya na kila anapofuatwa huwa hivyo,” alisema Kingunge.
Alisema kwa nafasi aliyonayo kwa jamii, Warioba anapozungumzia suala hilo ni sawa na kuingilia demokrasia kuhusu mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea baina ya CUF na CCM.
Alisema kama kuna mtu ambaye anaona hawezi kuwa katika chama hicho ni vema akawaacha wanachama wenye nia ya kukiendeleza chama na kusikiliza kile kinachoamriwa na viongozi wahusika.
Alisema hata kama mtu ni mwanasiasa mkongwe, haimaanishi kuwa ndiyo ana mamlaka ya kutangaza mambo bila kuuliza au kufuata taratibu zinazotakiwa, kama ambavyo baadhi ya watu walivyokuwa wakiongea na waandishi wa habari.
“Hata mimi ni mwanachama mkongwe wa mwaka 1954 na huwa siingii kwenye vikao mbalimbali vya chama na kamwe sithubutu kuanza kuzungumza mambo nisiyoyajua,” alisema Kingunge.
Alisema mambo yote kuhusu mazungumzo ya muafaka wa Zanzibar yalizungumzwa katika Halmashauri Kuu ya CCM iliyofanya kikao chake Butiama Machi mwaka huu na jibu lililotolewa ndiyo msimamo wa chama.
Alisema yeyote ambaye anatoa maneno tofauti na yalitolewa na NEC, atakuwa anafanya hivyo kwa niaba yake na si ya chama, kama baadhi ya watu wanavyotafsiri.
“Anayetoa kauli mbali na ile ya kule Butiama anafanya hivyo kama maoni binafsi na wala si kutumwa na chama,” alisisitiza Kingunge.
Hivi karibuni, Jaji Warioba alibainisha wazi kuwa suluhisho la pekee la kutatua mpasuko wa kiasiasa wa Zanzibar ni kuwa na serikali ya mseto.
Kingunge, ambaye alikuwa mwenyekiti mwenza katika kamati ya mazungumzo, alisema kuwa CCM imeridhia kuundwa kwa serikali ya pamoja visiwani Zanzibar ifikapo mwaka 2010, ili kumaliza mpasuko wa kisiasa ndani ya visiwa hivyo.
Alisema si kweli kuwa mazungumzo ya muafaka yalifikia mwisho, bali kulikuwa na ajenda moja iliyobaki, ambayo haikujadiliwa kabisa.
Aidha, alibainisha kuwa, timu zilizoundwa kufanya majadiliano hayo hazikuwa na kauli ya mwisho bali vyama ndiyo vyenye jukumu hilo.
“Kwanza mazungumzo hayajamalizika, pili tulikubaliana na wenzetu kuwa tutaunda serikali shirikishi visiwani Zanzibar lakini iwe mwaka 2010, lakini CUF hawataki kukubali hilo wanataka mabadiliko hayo yafanyike sasa,” alisema.
Aliilaumu CUF kwa kile alichodai kuwa inapotosha ukweli wa mambo kuhusu mazungumzo ya muafaka, kwani wamekuwa wakiwaeleza wananchi mambo tofauti na waliyokuwa wakiyajadili na kukubaliana.
Alisema upotoshaji huo unachafua hali ya hewa visiwani Zanzibar na unarudisha nyuma juhudi za kudumisha amani, umoja na maendeleo ya visiwa hivyo na Tanzania kwa ujumla.
Aidha, alisema iwapo CCM itakubali kuunda serikali shirikishi hivi sasa itakuwa ni kukiuka katiba na sheria ambazo zinatambua kuwa chama kilichoshinda uchaguzi ndicho chenye kuunda serikali yake.
Katika hatua nyingine, Kingunge, alisema CUF ilianzishwa kutoka Chama cha ZNP (Wahizbu) na tatizo la Zanzibar ni la kihistoria, kwani tangu zamani kulikuwa na siasa za chuki.
“Siyo siri CUF ilianzishwa na Wahizbu ambao chama chao kilikuwa ZNP na historia inatueleza wazi si watu wa kukubali kushindwa, ndiyo maana tumemua kuunda serikali shirikishi ili kutatua matatizo,” alisema Kingunge.
Naye Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba, alisema kutokana na kutokukamilika kwa mazungumzo hayo, wanawaomba CUF warejee kwenye meza ya mazungumzo, ili waweze kumalizia ajenda iliyobaki.
Alisema haoni sababu za kuitwa kwa waangalizi wa kimataifa ili kumaliza mazungumzo hayo, kwani kwa asilimia kubwa yamefanikiwa na kilichobakia ni kidogo.
Alizitaja ajenda zilizojadiliwa kuwa ni uchaguzi mkuu wa Zanzibar, usawa wa haki katika kuendesha siasa, masuala ya utawala ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na njia za kuimarisha maelewano katika uendeshaji wa uchaguzi huru na haki Zanzibar.
Alibainisha kuwa, ajenda iliyobakia ni utaratibu wa utekelezaji wa programu ya utekelezaji wa makubaliano yatakayofikiwa katika mazungumzo ya muafaka.
Alisema ni timu ya wajumbe wa CCM iliyoundwa kushiriki katika mazungumzo hayo, haikuwa na mamlaka ya kutoa uamuzi juu ya mazungumzo hayo, bali ilitakiwa kuyawasilisha katika kamati kuu ya chama ambayo iliyawasilisha halmashauri kuu ya chama iliyoketi Butiama Machi mwaka huu. Alisema NEC ilitoa mapendekezo yake na kuitaka timu ya mazungumzo irejee kwenye meza ya mazungumzo na CUF ili mapendekezo hayo yaweze kufanyiwa kazi, jambo ambalo lilipingwa vikali na CUF na kudai kuwa hakuna sababu ya kurudisha muafaka kwa wananchi. Wakati CCM wakisisitiza kuwa mazungumzo bado hayajamalizika, CUF walishatangaza kuwa hawawezi kurudi kwenye mazungumzo hayo, kwani kila kitu kilishakamilika, kilichobakia ni utiaji saini.
 
Niliwaasa wafanye mabadiliko wakakataa na sasa wanaleta propaganda za UCHAWI!
 
Ccm Bado Ni Chama Imara.hakina Matatizo Ya Kisera Wala Kanuni Za Ujenzi Wake,inaweza Kuwa Na Matatizo Madogo Madogo Ya Kimaamuzi Ambayo Hakuna Taasisi Inakosa Matatizo Kama Hayo Iwe Chadema Au USA.mfano Ni Uamuzi Wa U.S.A Kuingia Katika Vita Vya Iraq,vigezo Vilivyotumika Vilikuja Bainika Kuwa Ni Uongo Lakini Mpaka Dakika Hii Hakuna Silaha Za Kemikali Wala Bailojia Vilivyoonekana....bush Bado Yuko Madarakani.
 
Last edited:
Ccm Bado Ni Chama Imara.hakina Matatizo Ya Kisera Wala Kanuni Za Ujenzi Wake,inaweza Kuwa Na Matatizo Madogo Madogo Ya Kimaamuzi Ambayo Hakuna Taasisi Inakosa Matatizo Kama Hayo Iwe Chadema Au USA.mfano Ni Uamuzi Wa U.S.A Kuingia Katika Vita Vya Iraq,vigezo Vilivyotumika Vilikuja Bainika Kuwa Ni Uongo Lakini Mpaka Dakika Hii Hakuna Silaha Za Kemikali Wala Bailojia Vilivyoonekana....bush Bado Yuko Madarakani.

Jamani mnapoamua kujibatiza majina ya nyongeza, angalau basi mkumbuke kubadilisha staili ya kuandika. Sasa hii ni nini? Yaani mnafanya tuwaFMES (tuwagundue) kila rahisi mno. Mwee!!!
 
Hakuna haja ya kufanya mabadiliko. Muhimu ni hiki chama kupotea kabisa na wala hakuna haja ya kujua hata bango lao. Wameweza nini mpaka sasa cha msingi? Elimu yetu butu kwaani uwezo wa watanzania kufikiri, kuhoji na hata kuchambua mambo ya kitaifa na kimaendeleo hachilia mbali mambo ya Afya, ajira, uchumi na hata utawala bora na demokrasia halisi umedidimia. Wanadharau na wamelewa uongozi. Hakuna tena viongozi wachapa kazi.
 
Ama kweli kumbe CUF walikuwa kimaslahi zaidi.Yani sasa ni kweli kuwa wao ni ccm b!ccm nao mnapodai hii ni forum ya chadema ndipo mnakosea.

Mnaona tulivyokuwa tukiwasisitizia mubadilike?Mkaja na haya ya kuvuana magamba na kuimeza cuf ili waache kelele.

Wengine tulidhani muafaka ni jambo jema.
 
chama,unasema eti sijawahi kuwashauri ccm?Mkuu kama nilivyosema tulichoshwa,tulijuwa ni usanii kitambo sana,huwezi kuwasapoti hawa kama huna manufaa na ufisadi,simple.
 
Last edited by a moderator:
Ccm Bado Ni Chama Imara.hakina Matatizo Ya Kisera Wala Kanuni Za Ujenzi Wake,inaweza Kuwa Na Matatizo Madogo Madogo Ya Kimaamuzi Ambayo Hakuna Taasisi Inakosa Matatizo Kama Hayo Iwe Chadema Au USA.mfano Ni Uamuzi Wa U.S.A Kuingia Katika Vita Vya Iraq,vigezo Vilivyotumika Vilikuja Bainika Kuwa Ni Uongo Lakini Mpaka Dakika Hii Hakuna Silaha Za Kemikali Wala Bailojia Vilivyoonekana....bush Bado Yuko Madarakani.
Come again?
 
BAK,mzee Warioba naye alipiga kelelee!yeye na Butiku,wakisharikiana na Nape akiwa India wakati huo,wakapingana hadi ikaja mambo ya ccj nk.Eventually sijui nini kilimyamazisha Warioba,nadhani walimshtua na ile issue ya "Mwananchi",mzee Butiku sanasana alikuwa na bifu kuhusiana na "funding" ya mwalimu Julius Nyerere foundation.Nape kama tunavyojuwa ni katibu mwenezi na alikuwa akienda kuchua mkwanja straight from mkulu mwenyewe,lakini kumbe alipelelekwa kwenye "roller coaster ride"Sasa wote wameshakuwa kitu moja again.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom