CCM hili la Jangwani ni kosa la kiufundi

Sungurampole

JF-Expert Member
Nov 17, 2007
984
205
Jana CCM mlieenda Jangwani na nyie mkatoa yenu.

Sii siri move hii ililenga kujibu mapigo ya Chadema ambao walitinga hapo Jangwani na M4C.

Wanavyosema wajuzi wa kabumbu wanasema katika makosa timu inaweza kufanya
ni kukubali kuiga mchezo wa mwenzako ukiwa unacheza naye iwe ni pasi ndefu, fupi,
mchezo wa kasi, polepole au mipira ya juu n.k.

Sababu ni wazi kuwa wewe utajikuta mgeni katika kuutumia kikamilifu ile style.
Haya ndiyo yalityowakuta CCM jana Jangwani.

USHAURI: CCM kuweni wabunifu msiingie mtego wa kufuata kila wanachokifanya CHADEMA.
Si lazima wakisema Vua Gamba, Vaa Gwanda na wewe Useme Vua Gwanda, Vaa uzalendo
Kesho wakianza maandamano nanyi mtakaandamana?
 
ukifuatilia kwa undani utakuta wote waliohudhuria ni ndugu wa viongozi wa ccm ambao wanajua ni nini wanachofaidi kwa kuwashabikia.....ila kwa wazalendo ni vigumu kuwakuta katika mikutano ya chama kilichopoteza dira na kuchochea ugumu wa maisha ya watz.
 
Kumbe kusingekuwa na magari hata robo ya watu wasingelikwenda. Hii inatoa picha kwamba ndugu zetu CCM wanatumia pesa nyingi kuwaelimisha watu mambo yaliyoyafanya baada ya mambo kujieleza yenyewe.

Kama umejenga nyumba kuna haja gani ya kuitagaza kwa majirani na wanao ili hali nyumba ni yako lasivyo nyumba si yako ila unatafuta sifa ambazo si zako.

CCM walipaswa kufanya kazi zionekane na si kuita watu na kusema tumefanya hivi, wakati bado kuna watumishi hewa, mgao wa umeme, hakuna maji, elimu mbovu, ajira za kujuana na rushwa nje nje.

Kwanza malizeni au punguzeni hayo matatizo ndo mrudi kwa wananchi na sio kupoteza pesa zenu kwa mambo yasiyo na tija.
Pesa mliyo poteza jana mngeweza kuitumia kufanya mambo ya maendeleo.
 
Breaking news! CCM yafia 'chadema square'. ukweli ni kuwa hawaziwezi pasi na soka safi la ki-bacelona linalochezwa na chadema. wamezoea kubutua tu! watapigwa magoli meeeeeeeengi.
 
hayo magari ya green acres ni msala huo! magari ya shule ni ya shule, madereva walinogewa na pesa za magamba, wakaiba ruti.wanalo hilo!
 
Kumbe kusingekuwa na magari hata robo ya watu wasingelikwenda. Hii inatoa picha kwamba ndugu zetu CCM wanatumia pesa nyingi kuwaelimisha watu mambo yaliyoyafanya baada ya mambo kujieleza yenyewe. Kama umejenga nyumba kuna haja gani ya kuitagaza kwa majirani na wanao ili hali nyumba ni yako lasivyo nyumba si yako ila unatafuta sifa ambazo si zako.
CCM walipaswa kufanya kazi zionekane na si kuita watu na kusema tumefanya hivi, wakati bado kuna watumishi hewa, mgao wa umeme, hakuna maji, elimu mbovu, ajira za kujuana na rushwa nje nje. Kwanza malizeni au punguzeni hayo matatizo ndo mrudi kwa wananchi na sio kupoteza pesa zenu kwa mambo yasiyo na tija.
Pesa mliyo poteza jana mngeweza kuitumia kufanya mambo ya maendeleo.


Na hiyo ndiyo tofauti kati ya CDM na CCM
 
ukifuatilia kwa undani utakuta wote waliohudhuria ni ndugu wa viongozi wa ccm ambao wanajua ni nini wanachofaidi kwa kuwashabikia.....ila kwa wazalendo ni vigumu kuwakuta katika mikutano ya chama kilichopoteza dira na kuchochea ugumu wa maisha ya watz.

Hadi Mjukuu wa kitwana kondo naye aliudhuria pale,alikua na fujo sana azania enzi hizo anakuja na benzi anapakia wachumba wa jangwani na zanaki tu!
 
Tuache unafiki; ccm walichemka. Wangalikua na nafuu yao wasingalitaja cdm.
 
Litasanuka tu, wiki hii utasikia mimi sikupewa posho yangu, mimi nilipewa nusu, wenye magari nao wataanza kuvamia ofisi zao kudai pesa, vuta pumzi utasikia mimi nilifanya route 5 nimelipwa 2
 
Haya ni makosa ya nape,tafadhali apewe wazee wa kumshauri.
 
Kweli hili kosa la kiufundi hata hii ya kukodi magari na kuleta watu mhhh ni tofauti na mikkutano ile watu wanaenda Voluntarily kwa miguu yao Kova alijua ccm wanasomba watu na magari ndo maana hata hakuhangaika kuhadharisha watakamata mtu atakayeonekana anaandamana
 
Kikwete na Pinda kwa nini hawakuhudhuria Mkutano wa magamba yao? au ndiyo wamenyoosha mikono juu kwamba magamba iko ICU inasubiri kuzikwa tu.?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom