CCM,adui namba moja wa mzanzibar

Spav V

Member
Aug 20, 2018
11
52
Wakati tunasoma andiko hili ni vyema tufahamu kwamba historia ya taifa hili na hasa Muungano haijaandikwa itakiwavyo na kuwekwa wazi,Watanzania wamekuwa wakipewa tafsiri ya kisiasa pekee na hivyo Muungano umebaki kuwa "Fumbo la Imani" kwa kuwa ni dhambi kuu Kuhoji juu ya Muungano.

NINI KILITOKEA KATIKA KUANZISHWA MUUNGANO WENYEWE?
Mkataba wa muungano ulitiliwa saini mnamo tarehe 22 aprili 1964 kati ya Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karum.Jina la Muungano limetajwa katika Sheria namba 22 ya Muungano ya mwaka 1964.Jina sahihi la Muungano ni "Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar" hili neno Tanzania halikuwepo.

Ikumbukwe kipindi baada ya Muungano hakukuwa na katiba iliyoandaliwa ili kusimamia Muungano na ilikubaliwa kwamba katiba ya Tanganyika itumike ndani ya Mwaka mmoja kutokea Muungano.Hivyo Zanzibar haikuwa na katiba yake yapata miaka 21 hadi 1984 lakini Zanzibar ilikuwa na sheria zake zitokanazo na maagizo ya Rais (Presidential Decrees).

KATIBA YA MWAKA 1965
kwa kutambua kwamba serikali za Tanganyika na Zanzibar hazikufa baada ya Muungano iliwekwa bayana kuwa sheria za Tanganyika kutumika katika nchi hizo (soma kifungu 8 cha sheria ya Muungano na ibara ya 5 ya mkataba wa Muungano).Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ilitakiwa kuwa na katiba yake ndani ya miezi 12 kuanzia aprili 26 1965 yani kufikia tarehe 26 aprili 1965 kwa mujibu wa mkataba was Muungano lakini haikuwa hivyo.
Machi 26 mwaka huo bunge lilipitisha sheria namba 18 ya mwaka 1965 kuongeza muda wa kuitisha bunge la katiba hadi hapo Julai 10 1965 ndipo binge lilipitisha Katiba ya Muungano.

KOSA LA JUMBE NI KUASISI CHAMA CHA MAPINDUZI.
Kama kuna kosa kubwa Rais wa pili wa Zanzibar analijutia huko aliko sasa basi ni kukubali kuiua ASP na kuasisi CCM mwaka 1977.Kwanza tunatakiwa tutambua kuwa Vyama vya siasa havikuwa jambo la Muungano na wala haikuwahi kutajwa katika mambo yale kumi na moja ya Muungano.Jumbe alifanya kosa ambalo baadae lilikuja kumtafuna yeye mwenyewe

MUUNGANO UNATIKISIKA.
Hatua ya kwanza iliyoanza kuutikisa Muungano wa Tanganyika na Zanzabar ni pale wazanzibar waliporudi kudai mabadiliko ya katiba kuuhusu Muungano.
Hatua kali zilichukuliwa hasa tukio linalokumbukwa ni pale Rais Jumbe alipomrejesha bara aliyekuwa Mwanasheria mkuu wa Zanzibar Jaji Damian Lubuva na badala yake akampa kushika wadhifa huo Alhaj Bashir Swanzy aliyekuwa Mghana kuanzia hapo harakati za kudai mabadiliko makubwa ya katiba yakaanza yakichagizwa na Redio za mafichoni maarufu kama KIROBOTO TAPES.
Hatimae mwisho wa yote Jumbe aliitwa kuhojiwa Katika kikao cha Halmashauri kuu NEC Dodoma alivuliwa nyadhifa zote za uongozi na kuwekwa kifungoni Kigamboni wote tunaelewa.CCM aliyeiasisi mwenyewe ikamtafuna.

KWANINI CCM NI ADUI WA WAZANZIBAR
01.Kupitia chama cha mapinduzi Wazanzibar sasa mambo ya msingi yote yanaamuliwa pale Dodoma.Mfano Mgombea urais Zanzibar anateuliwa na NEC,je kuna uwiano sawa wa wajumbe wa bara na visiwani?

02.Rais wa Zanzibar sasa ni mjumbe katika baraza la mawaziri la Muungano lakini hana nguvu yoyote kwa maana hiyo hatuwezi kukosea tukisema hana tofauti na mkuu wa mkoa.

03.CCM imetengeneza mfumo ambao si rahisi kwa Wazanzibar kujitatulia matatizo yao wao wenyewe.

04.Kitendo cha kumpunguzia madaraka Rais wa Zanzibar kutoka Makamu wa kwanza wa Rais hadi kuwa mjumbe wa kawaida wa baraza la mawaziri kwa kiasi kikubwa cheo cha Rais wa Zanzibar hakina nguvu tena

Zanzibar imeuzwa Dodoma,Wazanzibar amkeni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom