CAF Confederation: DFC vs Zamalek: Mataifa ya chini ya jangwa la Sahara bado kuna safari ndefu kuwasumbua waarabu

Braza Kede

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
1,898
3,657
Hapa naangalia mechi ya CAF ya Confederation wanacheza Dream (DFC] ya naija wapo homeground wameshakula chuma 3-0 dhidi ya mafarao wa Zamalek.

Ukiangalia makosa ni yaleyale ya siku zote kama timu zetu hapa.

Papara nyingi, kimbiakimbia za hovyo kama za ndondo cup na kukosa umakini wanapokaribia goli la wapinzani kunawagharimu sana hawa DFC.

Na walivyoelemewa wanaweza kula hamsa hawa.

Hawa hawana tofauti na hawa wachezaji wetu wa hapa yaani wakikaribia goli la mpinzani wanapoteza utulivu na umakini kabisa unashangaa mtu yuko nafasi nzuri lakini icho atakachokifanya anakijua yeye na mungu wake tu.

Nadhani kuna kitu hawa waarabu wanacho na wachezaji wetu wanakikosa. wataalam wetu wana kazi ya kufanya kuweka sawa haya.
 
Waarabu wanapendelewa
 
Aisee.

Mechi ya awali akiwa ugenini walitoka sure, nyumbani kaja kufungwa.
 
Watu weusi hatuna utulivu.

Mfano nafasi aliyokosa mzize dhidi ya mamelodi ndio hiyo hiyo mshambuliaji wa esperence kafunga goli.

Mpaka nikajiuliza kwa nini watu weusi hatuna utulivu golini?
Wala Haina uhusiano na weusi mkuu ni kiwango Cha mchezaji,aliyefunga goli ya Zamaleki la pili ni mweusi na katulia sana tena kachagua angle kabisa
Kiwango ndio kinaamua hao Dream ni wepesi sana wanarukaruka tu
 
Waarabu wanapendelewa
mkuu izo zilikuwa propaganda za viongozi wetu wa mpira kuficha madhaifu.

mpira ni mchezo wa wazi sana hauwezi kuleta upendeleo hlf uachwe tu.

watu wakikushindwa kabisa basi watakusema maana hauwezi kuwazuia wasiseme.

miaka iyo viongozi wa mpira walikuwa hawaandai vizuri timu zinaenda uko zinakula hamsa icho ndo kinakuwa kichaka chao na bahati mbaya miaka iyo mpira ulikuwa hauoneshwi kwaiyo tulikuwa tunawaamini ila saivi ayo hayawezekani.

ona lile goli la aziz ki la mamelodi lilivyopigiwa kelele afrika nzima tena hata na vyombo vya habari vya ukouko sauzi wanakuambia lile lilikuwa ni goli halali
 
Wala Haina uhusiano na weusi mkuu ni kiwango Cha mchezaji,aliyefunga goli ya Zamaleki la pili ni mweusi na katulia sana tena kachagua angle kabisa
Kiwango ndio kinaamua hao Dream ni wepesi sana wanarukaruka tu
huyo mweusi wa zamalek mm nazan kinachomsaidia ni hao waarabu waliomzunguka lakin hoja ya mtu mweusi kuwa na papara na kukosa subra kwene maeneo muhim nazani iko sahihi kabisa

we waangalie wale wakongo wana timu nzuri sana lakn kukosa utuliv huwa kunawaghalimu sana licha ya kucheza ulaya lakin bado wana iyo hulka ya papara.

kwangu mimi wale mamelodi ndo kati ya timu chache sana za weusi pekee zilizoweza kuondokana na hilo tatizo la kucheza kwa kutanguliza hisia na mihemuko. mara zote utaona wanacheza kwa utulivu na akili kubwa uku wakimwangalia mpinzani nae anakujaje na wao wafanye nini.
 
Mkuu hii Haina uhusiano na rangi sema grooming namna wachezaji wanavyoandaliwa kuanzia chini hadi kufikia kiwango Cha ukubwa
Kuna mifano mingi sana ya weusi wakifanya vizuri na Kuna wazungu wengi tu na waarabu wanaokosa magoli
 
Sasa hii Mechi ya Berkanena USM Alger imeamliwa vipi maana waAlgeria hawajatokea kabisa uwanjani na sijawaona hata waamuzi pia.
 
Back
Top Bottom