Buriani Mhe. Komba wa 'Joka la kufugwa'

Japo majoka bado yapo mengine yana makengeza hapa kwetu tanzania,tunahitaji viongozi watakawaowasema live na kuwaondoa hayo majoka..Buriana Capt. Komba

Tena majoka yani wa leo ni akheri wale wa Marehemu Nduli Amin Dadaa!

Tulionao leo hii ni zaidi ya joka tunalolijua.........
 
Mh Judge Warioba wengine tunamuita baba na wengine wanamuita Babu.Ni imani yangu Mzee Warioba kwa sifa zake za u Baba na U babu alikwisha msamehe RIP KOMBA,mzazi hauwi.Maandiko matakatifu yanatutaka tusameane ili iwe sababu ya ku upata ufalme wa mbinguni.
 
Kwa kuongezea tu yule Komba wa enzi za Mwl Nyerere sio Komba ambaye alikuwa hivi sasa kabla ya mauti kumpata,aligeuka na kuwa kibaraka wa mafisadi,hata utu wake aliuweka rehani,akaishiwa hata hekima na kubaki kama mwendawazimu,kinywa chake kilijaa uchafu na dharau kwa wananchi wa nchii hii,nadhani fedha zilimpofua macho,unaweza kufanya mazuri lukuki lakini jambo moja tu baya likakuondolea sifa zote,Komba atakumbukwa na mafisadi wa CCM na sio wananchi wote,alitutakia mabaya tulipodai serikali tatu,akadai ataingia msituni kabla ya kupata hizo serikali tatu,na kujiapiza maneno mambo mengi ungedhani yeye ndie Mungu.Kifo cha Komba na kiwe fundisho kwetu sisi wanaadamu,yatupasa tuwe wanyenyekevu wakati wote hata tukipata madaraka,pia yatupasa kuchunga vinywa na ndimi zetu,neno likitoka halirudi,na neno baya au lenye shari kamwe halisahauliki,maneno ya marehemu aliyokuwa anayatoa mle bungeni yalikuwa chukizo kwa watu wengi huku yakifurahiwa na wachache walioshiba.Tusijisahau sana kama hao wengine waliobaki wanaodai eti milioni 10 ni hela ya mboga,wengine eti nyoka wa makengeza,wengine wanaodai sisi ni wauza juisi tu.Dharau na jeuri ya pesa haileti heshima bali ni sifa za kijinga,na mwisho wake huwa mbaya na kuwa chukizo.

ukweli mtupu..!
 
Bunge la Katiba limemuharibia ndugu yangu wa Kusini John Damian Komba amepoteza umaarufu tu kwa kutetea Serikali mbili leo hii angekuwa shujaa wa Taifa ila kashusha thamani yake kwa kutetea Chama. kamdharau Jaji Warioba namuombea Radhi kwa Jaji kama hakufanya hivyo kabla ya mauti.
 
Wewe muongo sana, umezaliwa 1979.
Hapo hapo umekuwa kiasi cha kwamba unaweza kusikiliza nyimbo na kuzielewa.
Mkuu, ulizaliwa ukiwa unajua kuongea ama?
Kama ulikuwa unatafuta namna ya Kumsifia Komba, kuna namna nyingi sana, ungeweza kumsifia na huenda watu wangekuunga mkono ila sio kwa kutanguliza uongo.
 
Soma vizuri toka mwanzo utamuelewa.
 
Mwaka mmoja kabla ya mimi kuzaliwa 1979, ...
Consider this sentence: Woman without her man is useless.
With punctuation we have the following from he and she.

  • He: Woman, without her man, is useless...
  • She: Woman, without her, man is useless...
Sasa tuje hapa...mwaka mmoja kabla ya mimi kuzaliwa 1979. Hebu fafanua tafadhali Nyakarungu. Je ulizaliwa kabla ya, baada ya au mwaka 1979.
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli capt Komba alistahili kupewa sifa kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati huo. Lakini lazima tukumbuke kuwa mazuri mengi sana zaidi ya million utakayofanya, yanaweza kuondolewa na jambo moja baya utakalolifanya. Hata maandiko yanasema hivyo, fanyeni mema siku zote, ukikosea jambo, isifike machweo ya jua kabla hujatubu, kwa maana hilo moja ulilokosa litakuhariabia yote mema uliyofanya maishani mwako. Capt. Komba baada ya kupata sifa zote hizo aligeuka kuwa mtu asiyestahili kitu, alikuwa ni mtu ambaye hafai kwa jinsi alivoyotumia mdomo wake vibaya na sijui kama alikumbuka kutubu kabla hajafa. Aliwachulia vifo wazee wenye hekima na watumishi wenye utumishi uliotukuka kwenye taifa hili. Lakini mwenyezi Mungu mwenye rehema amemuliza Komba, je nani alikuambia kuwa wewe utaishi milele, leo nachukua roho yako. Hakuna gharama yeyote utakayotoa ukiwaheshimu na kuwasemea mema wanadamu wenzio. Komba amekwenda na iwe fundisho kwetu.

Mkuu unaposema mazuri ni vizuri tuyataje. Mara nyingi watu tunasema amefanya mazuri mengi lakini hatausema hayo mazuri mengi ni yapi. Moja na labda la pekee ninaloweza kusema ni kuwa kwenye miaka ya 70 na 80 alikuwa mburudishaji mzuri. Nyimbo zake zilihamasisha umma pia. As entertainer YES.

Lakini ukumbuke kuwa he was some how connected with drug lords. Pesa za ufadhili wa TOT zilizotoka kwa Mpakanjia zinajulikana zilikuwa na harufu gani. Na baada ya Mpakanjia kuaga dunia TOT nayo ikaaga dunia.

The man openly befriended with drug lords, tacitly embraced, supported and benefited from narcotics trade. Sasa kama mtu anakuwa hivi na unajua kabisa jinsi dawa za kulevya zinavyowafanya vijana wa Tanzania, halafu unategemea watu waseme umefanya mazuri???? Mazuri yapi? Hata ukiluliza fedha za kampeni ya ubunge wake unajua kabisa kuwa ni giza tupu. Ndio maana nashangaa kuona hata watu tunaowaheshimu kama kinja Kitila Mkumbo wanawasifu watu kama hawa. So sick.
 
Nawe una ujinga huu
1. Shikilia unaandika shikiria.
2. Umbali wa km 5 huko ofisi ya kata ilikokuwa unakuona mbali hadi unamsifia babako kuja nyumbani saa tatu usiku halafu kwa kutumia baiskeli. Au ulikusudia km 50?
 
Pole kwa umma wote wa Watanzania kwani nchi imepoteza mmoja wapo wa wasanii wakubwa . Mwenyezi Mungu akaifariji familia yake.
 
Mkuu unaposema mazuri ni vizuri tuyataje. Mara nyingi watu tunasema amefanya mazuri mengi lakini hatausema hayo mazuri mengi ni yapi. Moja na labda la pekee ninaloweza kusema ni kuwa kwenye miaka ya 70 na 80 alikuwa mburudishaji mzuri. Nyimbo zake zilihamasisha umma pia. As entertainer YES.

Lakini ukumbuke kuwa he was some how connected with drug lords. Pesa za ufadhili wa TOT zilizotoka kwa Mpakanjia zinajulikana zilikuwa na harufu gani. Na baada ya Mpakanjia kuaga dunia TOT nayo ikaaga dunia.

The man openly befriended with drug lords, tacitly embraced, supported and benefited from narcotics trade. Sasa kama mtu anakuwa hivi na unajua kabisa jinsi dawa za kulevya zinavyowafanya vijana wa Tanzania, halafu unategemea watu waseme umefanya mazuri???? Mazuri yapi? Hata ukiluliza fedha za kampeni ya ubunge wake unajua kabisa kuwa ni giza tupu. Ndio maana nashangaa kuona hata watu tunaowaheshimu kama kinja Kitila Mkumbo wanawasifu watu kama hawa. So sick.
I knew he was a singer/entertainer as you said, thinking that was financed by TPDF. Now this is new to me,thanks a lot.
 
Yaani nilipokuta 'R' mahala pa 'L' zaidi ya mara tatu nimeshindwa kuendelea kusoma. Sijui inakuwaje mtu unakuwa na uwezo wa kuandika makala ndefu namna hii halafu unashindwa kujua 'R' na 'L' ni herufi tofauti na hata matumizi yake hayajawai kuwa sawa?

Chaaaa!!
 
Rest in eternal peace Captain John Komba. Alipata B.A. kutoka Washington University kimombo haikuwa taabu kwake. :baby:
 
Back
Top Bottom