kukomya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2011
- 344
- 143
Mi nilishaacha kuwaita hawa jamaa "waheshimiwa" na hicho kijiwe chao "kitukufu" kuanzia nilipobaini wezi na vibaka kama kina Mramba wakitokea Mahakamani na rumande kwenda kuhudhuria vikao "vitukufu" baadae nilipata kichefuchefu cha kumwita yeyote mheshimiwa au mtukufu nilipoona hata vibaka kama kina Chenge, EL, na wengine kibao wamo! Nasikia hata yule aliyekamatwa na rushwa red handed na kesi yake iko mahakamani bado anaitwa "mheshimiwa"! Hivi watanzania tuna akili kweli? Napata kigugumizi hata kumwita mkuu wa kaya Mheshimiwa baada ya wazungu anaowahusudu kuanika madudu yake ya kuhongwa hata nguo! Majuzi ndiyo kabisaa... karibu nizimie; eti Spika amevunja kamati iliyohusika na rushwa na kuunda nyingine huku hao jamaa wakiendelea kuitwa "Waheshimiwa"! Hivi kwa nini tusiweke katika katiba yetu mpya kwamba watu wa aina hii wasimamishwe nafasi zao za ubunge na wakithibitishwa kutenda walivyotenda - inyume cha kiapo na kuaminiwa kwao wafungwe maisha (Maana wajimba wamesema tusinyonge mtu!)? Kwa kifupi Tanzania ni nc hi ambayo huna wa kumwamini, kuanzia Rais, Polisi hadi Tarishi; kaa chonjo na "Kila abiria achunge mzigo wake". Tuitane Ndugu tu lakini hili la waheshimiwa na watukufu wezi, majambazi, vibaka na malaya kuwaita "waheshimiwa na watukufu" hapana tusubiri kidogo.