nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa inayoongozwa na Kamati ya Hesabu za Serikali Kuu na ile ya Mashirika ya Umma, zimeibua ufisadi wa kutisha ulioligeuza taifa kuwa shamba la bibi.
Kamati hizo ambazo zinaongozwa na Augustine Mrema (TLP), John Cheyo (UDP) na Zitto Kabwe (CHADEMA), ziliwasilisha taarifa zake za mwaka wa fedha wa 2008/2009 jana bungeni.
Katika halmashauri za wilaya nchini, ufisadi mkubwa umebainika kuwepo katika ununuzi wa spea za magari kwa kuongeza bei isiyo halisi, bei ya kughushi katika ununuzi wa mafuta, matumizi makubwa kwa ajili ya posho kuliko utekelezaji halisi wa miradi kama ya (TASAF), Mazingira na miradi mingine ya maendeleo.
Akiwasilisha taarifa ya kamati yake, Mrema alisema kwa mujibu wa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka wa fedha 2008/2009, Halmashauri ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga ilitumia sh milioni 2.9 kwa ajili ya kutengeneza pikipiki ya Kichina, iliyonunuliwa kwa bei ya chini kuliko ile iliyotumika kuitengenezea.
Alisema katika Wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro, kamati yake ilibaini kuwa halmashauri ilitumia sh milioni 15 kwa ajili ya kununua spea ya gari (Injector Pump ya Land cruiser had top).
"Lakini tulipofuatilia kwa kupiga simu kwenye duka lililouza spea hiyo, tuliambiwa bei yake ni sh milioni tatu," alisema Mrema na kuwaacha wabunge wakibaki na mshangao.
Mbunge huyo wa Vunjo aliendelea kusema kuwa kuna wilaya nyingine ambayo hata hivyo hakuitaja, waligundua kuwa ilitengewa sh milioni 12 kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wa ukimwi, lakini kati ya hizo sh milioni kumi zilichakachuliwa na sh milioni mbili tu ndizo zilizowafikia walengwa.
Kwa mujibu wa Mrema, katika kipindi hicho cha mwaka wa fedha, taarifa za CAG zimebaini kuwa mali za sh milioni 111.2 zilitumika kununulia mali za halmashauri mbalimbali, lakini hazikuandikwa kwenye vitabu vya mali za halmashauri husika na sh milioni 158, zilitumika kununulia mafuta ambayo matumizi yake hayajulikani.
Akiendelea kuibua ufisadi katika halmashauri za wilaya katika kipindi cha mwaka wa fedha 2008/2009, Mrema alisema sh milioni 792.9 katika halmashauri 40 nchini, zililipwa kama mishahara hewa kwa watumishi waliokwisha kufariki dunia na wengine kustaafu.
Lakini wakati sh milioni 792.9 zikilipwa kama mishahara hewa, sh bilioni 1.7 za mishahara isiyokuwa na wenyewe haikurejeshwa hazina na kusababisha hasara kubwa kwa taifa.
Huku akisikilizwa kwa makini na wabunge, Mrema alisema kiasi hiki cha mishahara hewa kina uwezo wa kujenga madarasa 113 ya shule za msingi nchini.
"Shilingi bilioni 328.2, zilizotolewa kwa ajili ya shughuli za maendeleo katika halmashauri 132, hazikutumika, sh bilioni 1.9 zilizokusanywa kama mapato ya ndani, katika halmashauri 43, hazikurejeshwa na mawakala kwenye halmashauri husika.
"Katika mwaka huo huo, halmashauri 113, zilikuwa na jumla ya madeni yaliyofikia sh bilioni 35.6, katika mwaka huohuo, vitabu 1,341 vya makusanyo ya mapato mbalimbali, havikupatikana kwa wakaguzi katika halmashauri 50. Kutaja mifano michache tu," alisema Mrema.
Ili kukomesha tabia hiyo, Mrema alisema kamati yake imependekeza mambo kadhaa ikiwemo kamati za Bunge za usimamizi kufuatilia fedha hizo mara zinapotolewa.
Kuhusu mishahara hewa, Mrema alisema waliohusika kwanza wazirejeshe, pia Hazina iache utaratibu wa kutuma pesa kwenye akaunti ya watumishi moja kwa moja bila kupitia kwa waajiri wao.
Cheyo na Kamati ya Hesabu za Serikali
Wakati Mrema akiibua ufisadi katika halmashauri za wilaya nchini, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kuu, John Cheyo, aliishukia Wizara ya Maliasili na Utalii kwamba kuna makampuni ya kitalii ambayo yamekuwa yakifanya kazi bila leseni, hivyo kuikosesha serikali mapato.
Alisema msako uliofanywa na wizara husika, ulibaini kuwa makampuni 23 yalikuwa yakifanya kazi bila leseni, hivyo kuikosesha serikali mapato. Aliilipua pia Wizara ya Fedha na Uchumi kwamba Februari 25 mwaka 1999, ilisamehe ushuru wa makampuni ya madini kulipia ushuru wa mafuta ya dola za Marekani 200,000.
Akizungumzia deni la taifa, Cheyo alisema limefikia sh trilioni 6.4 na kwamba linaendelea kukua kwa kasi. Mbali ya deni la taifa, Cheyo pia alisema wizara kadhaa zina mzigo wa madeni, hali ambayo inaweza kuathiri bajeti ijayo.
Akitolea mfano, alisema Wizara ya Miundombinu ilikuwa na madeni ya sh 742,920,080.58 na mihadi iliyofikia sh 178,596,360,000.
Alisema yapo madeni mengine kadhaa ya wizara na idara za serikali kama vile elimu, Jeshi la Polisi, Magereza na Wizara ya Afya na kuongeza kwamba madeni hayo yanatokana na uzembe wa maofisa masuhuli. "Haya ni madeni ambayo wizara inaenda nayo katika mwaka wa fedha unaofuata. Wasiwasi ni kwamba madeni haya yataathiri bajeti inayofuata kwa kulipia madeni," alisema Cheyo.
Kamati ya Zitto Kabwe
Kwa upande wake, Zitto Kabwe alisema kuwa fedha nyingi za umma zimepotea katika suala la manunuzi ya mali za umma.
Akitolea mfano, Zitto alitaja manunuzi yasiyozingatia sheria ya manunuzi kama yale yaliyofanywa na Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) ambapo sh 102,285,441 zilitumika.
Pia alizungumzia Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) kwamba linapaswa kuwezeshwa kama serikali ilivyokuwa ikifanya lilipokuwa likiendeshwa kwa ubia ambapo ilikuwa ikipata sh milioni 500 kila mwezi.
Tundu Lissu amvaa tena Ngeleja
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, jana alimvaa tena Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, akimtaka ajibu kwa ufasaha majibu ya maswali ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe (CHADEMA), aliyetaka kujua Shirika la Umeme nchini (TANESCO), linapata wapi fedha za kununulia mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya IPTL.
Lissu (CHADEMA) ambaye juzi alitoa kauli bungeni kwamba Waziri Ngeleja ni muongo na kutakiwa kuthibitisha kesho, aliomba mwongozo wa Spika akitaka waziri huyo ajibu maswali ya Zitto kwa ufasaha. "Mheshimiwa Spika, kanuni zinasema waziri atakuwa na wajibu wa kujibu swali la mbunge kwa ufasaha ndani ya Bunge isipokuwa kwa swali linalohitaji takwimu na vielelezo vingi. Swali la Mbunge (Zitto), halihitaji takwimu za aina hiyo. Naomba ajibu kwa ufasaha," alisema Tundu Lissu.
Akijibu hoja hiyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alisema kuwa mwenye uwezo wa kumtaka waziri ajibu swali kwa ufasaha ni Spika na kama mbunge anaona jibu lake halijakamilika, anapaswa kufuata taratibu. Someni kanuni vizuri," alisema.
Awali akijibu swali la msingi la Zitto, Waziri Ngeleja aliliambia Bunge kuwa mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura ya Kampuni ya IPTL, hutumia sh bilioni 15.62 kwa mwezi kwa ajili ya kugharimia ununuzi wa mafuta mazito ili kuendesha mitambo hiyo.
Waziri Ngeleja, alisema kiasi cha sh bilioni 46.4 au wastani wa sh bilioni 15.62 kila mwezi huitajika kwa ajili ya kugharamia ununuzi wa tani 36,800 za mafuta mazito (HFO) kwa kipindi cha miezi mitatu.
Ngeleja alisema kuanzia Novemba 15 mwaka 2010 hadi Februari 14, 2011 sawa na tani 400 ya mafuta mazito hutumika kwa siku.
Alisema pamoja na hatua zote hizo, hivi sasa kampuni mbili za Oryx na Total ndizo pekee zinazofanya biashara ya mafuta mazito na ndizo zilizoombwa kushiriki katika mchakato wa ununuzi wa mafuta hayo.
Waziri Ngeleja alisema utaratibu unaotumika kupata kampuni za Oryx na Total ni kwa ‘Restricted Tendering' ambapo kampuni za mafuta zilitakiwa kufikisha mafuta katika maghala ya IPTL kuanzia Novemba 2010.
Aidha, alisema katika hali ngumu kama hiyo maamuzi ya serikali yalihitajika kufanyika kwa haraka ili kupunguza ukali wa mgawo wa umeme kwenye mfumo wa gridi ya taifa.
Alisema fedha za kununulia mafuta ya kuendeshea mitambo hiyo ya IPTL hutoka katika mfuko mkuu wa serikali.
Waziri Ngeleja pia alisema serikali bado ina nia ya kuibadili mitambo ya IPTL kutumia gesi, lakini inashindwa kufanya hivyo kutokana na kesi iliyopo mahakamani iliyofunguliwa na IPTL dhidi ya TANESCO.
Hata hivyo majibu hayo yalimfanya mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani kuuliza swali dogo la nyongeza ambapo alihitaji kufahamu fedha hizo za kununulia mafuta hayo mazito zinatoka katika bajeti gani.
Alisema kwa sasa TANESCO iko kwenye mvutano wa kisheria na IPTL na kila siku hulipa sh bilioni 3.6 na kuziingiza kwenye mfuko maalumu na kuna zaidi ya sh bilioni 1.6 zimehifadhiwa humo.
"Ni kweli fedha hizo haziko kwenye bajeti lakini namtaka mbunge aje pale kwenye ofisi zetu tumuonyeshe wapi fedha hizo zinatoka," alisema Ngeleja. Jibu hilo ndilo lililomfanya Lissu kuomba mwongozo wa Spika kutaka Ngeleja ajibu kwa ufasaha.