Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,519
- 9,322
Bunge limesitisha kwa muda shughuli zake za leo ili kujadili changamoto ya bei duni inayowakumba wakulima wa mahindi nchini. Wabunge wameeleza kutoridhishwa na bei ndogo ya mahindi, bei ghali ya mbolea hivyo wameitaka Serikali kuiongeza hela NFRA ili inunue mahindi kwa wakulima.
Waziri wa Kilimo, Prof. Adolph Mkenda amekiri uwepo wa tatizo la bei ndogo ya mahindi. Ameeleza kuwa Serikali inachukua hatua za haraka kushughulikia suala hilo ambapo ameahidi kuwa kabla ya Bunge kuhitimishwa hapo kesho Serikali itatoa tamko bungeni kuhusu hatua ilizochukua.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameeleza kuwa Serikali imesikia kilio na Serikali na kupitia NFRA ilianza kununua mahindi kwa wakulima lakini imegundua kuwa uzalishaji wa mwaka huu ni mkubwa na Serikali imefanya mazungumzo na mataifa jirani ili kununua mahindi hapa nchini.