Bunge la Tanzania si kitu kwa JK?

MAGEUZI KWELI

JF-Expert Member
Jul 16, 2011
1,947
253
:embarassed2: Ninadhani ni kila mtanzania amekuwa akisubiria Tume iliyoundwa na Bunge kuhusu sakata la wizara ya Nishati na Mlungula kwa Wabunge na Jairo mtuhumiwa number 1 na waziri wake, Kisha ikahamia kwa Katibu Mkuu kiongozi Luhanjo kumsafisha Jairo ambaye Sakata lake liliibuliwa na Mama Shelukindo Bungeni, Sasa hapa ilisemekana hata waziri mkuu alikuwa Cha Mtoto kwa Luhanjo.:embarassed2:
Tume ile iliyoundwa iliibua mengi na ya kweli kabisa na kila mtanzania mpaka na wabunge wote waliokuwa wakisikiliza LIVE wanashangaa nini kinachosubiriwa na Mkuu wa Nchi.
:embarassed2:
Je kwa namna hii Bunge lina Sauti kwa Rais wa nchii hii?????
Hebu tusaidiane kwa hili....
:embarassed2:
 
Hivi kwa wasipige ile "VOTE OF NO CONFIDENCE" huu ni usanii.Kila jambo linapita pasipo maamuzi kutolewa kwa wananchi na isitoshe hata utendaji na morale umepungua miongoni mwa watanzania
 
hawa wote ni magamba wanatumia wingi wao vibaya.Wanapaza sauti bungeni then wakifika kwenye vikao vya chama wanapigwa biti wanatulia ...
 
Fikiria, baada ya kupitishwa sheria mbovu ya mchakato wa katiba, bado JK amekaa (si mara moja) kupokea busara za CHADEMA kuhusu mswada uleule (walioupinga ndani ya bunge!) Food for thought kwa hadhi ya Bunge na wabunge (hasa wa CCM).
 
Hivi kwa wasipige ile "VOTE OF NO CONFIDENCE" huu ni usanii.Kila jambo linapita pasipo maamuzi kutolewa kwa wananchi na isitoshe hata utendaji na morale umepungua miongoni mwa watanzania

Iko njiani inakuja..Beatrice Shelukindo katoa hint kwenye kikao juzi aliposema wakiamua wanamtoa JK
 
Back
Top Bottom