Bunge hili linapaswa kuvunjwa...

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,098
144,560
Naandika haya si kwa utani bali ni kutokana na uchungu nilionao kuona jinsi watu ambao tuliwatuma waende bungeni kutetea maslahi yetu jinsi walivyogeuka wasaliti wakubwa na kutanguliza maslahi ya chama chao badala ya wale waliowatuma!Inauma sana na kusikitisha na ni bora mwenyezi Mungu achukue roho zao ili kunusuru mamilioni ya watanzania ambao sasa ni wazi wamesalitiwa kwa kiasi kikubwa.

Kilichotokea leo bungeni hakina tofauti na kile kilichomtokea mh.Mbatia.Kwa wasiofahamu ni kwamba, hoja ya mh.Mnyika nayo imepigwa chini kwa kutumia wingi wa wabunge wa ccm baada ya naibu spika kuwahoji kama wanaunga mkono hoja hiyo iondolewe.Kama kawaida ya wabunge wa ccm wao ni chama kwanza na mwananchi baadae hivyo wengi wao waliafiki hoja hiyo ya mh.Mnyika iondolewe bila hata kujali athari za kuondoa hoja hiyo muhimu.

Kwa wale wasiokuwa na taarifa ni kuwa mh.Mnyika aliwasilisha hoja yake bungeni iliolenga kuondoa tatizo sugu la maji mkoani Dar-es-salaam lakini kwa hila za ccm hoja hiyo imekuwa ikipata upinzani na hatimae leo wameiondoa kwa kutumia wingi wao bungeni.

Hili jambo ni wazi limegeuzwa la kisiasa kwa kuona kuwa kama hoja hiyo ingepita labda mh.Mnyika na chama chake wangepata sifa kwahiyo ni bora waikwamishe.

Kwa kuzingatia matendo haya ya kinyama dhidi ya watanzania wanaoteseka na shida ya maji lakini wawakilishi wao wanaona ni bora waendelee na shida hiyo na nyingine nyingi kama vile elimu isiyo na mitaala basi ni bora mwenyezi Mungu awachukue wote kwa manufaa ya taifa hili.

CCM haya ndio maisha bora mliotuahidi!
 
Aminia mkuu sioni miwaBUnge ya CCM inawakilisha nini humo ndani bora ife tu. Kwanza hujajiuliza wakati wa hoja binafsi ya Mbatia kuhusu elimu mtu anayezunguka kwenye makanisa na harambee mbalimbali kusema eti elimu kwanza kilimo baadae hakuunga mkono hoja hii. Hii si ni double standard?11111
 
Kiukweli inakera sn. hapa ndio ile kauli ya siasa mchezo mchafu inapoapply. CCM wanaona ni bora kukwamisha huduma kwa Wananchi wa Dsm kwa vile hoja imetoka upinzani. Inamaana wao hawaguswi kabisa na shida hiyo?
 
Wakifa mili yao itupwe porini hamna haja ya kuwaombea wala kuwazika.Wana roho katili sana hawa watu.
 
tatizo ni sisi wenyewe ndio tunaowachagua,2015 tuikatae CCM na mambo yake yote.
 
aisee nna hasira sana na mibunge ya ccm! Nikiwaona natamani kutapika. Yaani ipo ipo tuu! Sisi wananchi tunaona wabunge wetu wa upinzani wanavyopiga kazi. Laana zote ziwaendee wabunge wa ccm
 
kwa kikifupi, kuitetea ccm inabidi uwe na roho ya shetani.
Kilichojiri leo bungeni kimedhihirisha kuwa wabunge wa ccm wakiongozwa na ndugai ni maadui wa maendeleo ya mtanzania.
 
Mnyika,

Tunashukuru bwana mnyika kwa kuwatetea watu wa DSM. Japo humu DSM kuna wabunge wa CCM na ndio wao waliokataa hiyo hoja
isijadiliwe ikiashiria hawakwenda bungeni kuwasilisha matatizo ya majimboni kwao hususani shida kubwa ya maji ila wewe peke yako
umeamua kuwa mbunge wa DSM kuwakilisha matatizo yao na sio jimbo la ubungo tu.

Nimefarijika sana.

Heko mnyika. Mungu akubariki sana.
 
Waoneni huruma wamechanganyikiwa mbinu zote zina fail fastjet kaanza kuaga, aibu ya kukabidhi nchi inawatesa, hata kwa maombi hawaponi bora shekh yahya angekwepo angewafariji namwonea huruma mtt pori na ujana ule ataenda wap? Cck hana nafasi family haimtambui hana babu anadandia family za watu.
 
Waoneni huruma wamechanganyikiwa mbinu zote zina fail fastjet kaanza kuaga, aibu ya kukabidhi nchi inawatesa, hata kwa maombi hawaponi bora shekh yahya angekwepo angewafariji namwonea huruma mtt pori na ujana ule ataenda wap? Cck hana nafasi family haimtambui hana babu anadandia family za watu.
Aisee inaumaa,afadhali angeamka na atubu dhambi hizi....hawa masisiemu laana yao imekwiva na naunga mkono hoja ya mtoa mada hii...Hongera kamanda Mnyika daima tutakuwa nyuma yenu makamanda mpaka kieleweke!!!
 
anna makinda.
job ndugai
wiliam lukuvi
stephen wasira
mwigulu nchemba
livingstone lusinde
hamis kigwangwala
sophia simba
ana kilango
shukuru kawambwa
bernaed membe
ismail rage
suleiman jaffu
nyambari nyangwine
muhamed dewji
ahmed shabibu
stella manyanya
hasnain murji
stephen ngonyani
......
.............
................
..........................
.................................
.........................................
................................................
..........................................................
.................................................................hiki kikosi kitatupeleka pabaya.
 
Hata tusiwalaumu.....ni sisi tuliwachagua kuwa wawakilishi wetu...." change ni wewe, ni sisi twaweza"
 
Hata tusiwalaumu.....ni sisi tuliwachagua kuwa wawakilishi wetu...." change ni wewe, ni sisi twaweza"

Mkuu tangu mfumo wa vyama vingi uanze sijawahi kuchagua kiongozi yeyote wa ccm kuanzia diwani mpaka raisi.
 
Back
Top Bottom