Bunge butu linaloingiliwa na kunyamaza, linapojikomba na kujipendekeza kwa Rais, linaweza kweli kuisimamia Serikali?!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,506
113,625

Wanabodi.

Naendelea na zile Makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa na Pascal Mayalla, zinazotoka kila siku za Jumatatu kweye gazeti la Raia Mwema.

Mada kuu ya udikiteta Tanzania itaendelea baada ya kumpata Prof. Kabudi, lakini kwa vile vikao vya Bunge vimeanza, kwanza nampa pole Mhe. Spika, get well soon, pia pole kwa Mhe. Tundu Lissu, tunakusubiria urudi, maana kutokuwepo kwako kumelifanya Bunge lipooze sana!. Naomba kuuliza swali dogo kuhusu Bunge letu, Jee linajipendekeza kwa serikali?. Kuna wakati enzi za Spika Sitta, Bunge la Tanzania lilipata meno, lakini sasa, ni mimi tuu naliona kama kwa kadri siku zinavyokwenda, Bunge linazidi kuwa Bunge Butu, Bunge Kibogoyo, Bunge linaloingiliwa na likanyamaza, Bunge ambalo serikali inafanya matumizi ya fedha za umma, bila kuidhinishwa na Bunge, lakini haliulizi, jee hili Bunge, ni ama linalijikomba komba kwa rais?, na linalojipendekeza kwa serikali?, Jee Bunge la namna hii, litaweza kweli kuisimamia serikali?.

Pongezi Msemaji wa Serikali Kuhusu Ukosoaji
Naomba kuanza mada yangu ya leo, kwa kutoa pongezi zangu za dhati kwa Msemaji Mkuu wa serikali, Dr. Hassan Abasi kwa kuzungumzia kuhusu ukosoaji wa serikali. Ukosoaji wowote, utaofanywa kwa kinachofanywa na serikali yetu, na mihimili yake ya dola, kama unatolewa kwa nia njema (in good faith), kwa nia ya kujenga na sio kubomoa, na ukosoaji huo ukatoa ushauri wa kitu sahihi cha kufanyika, huitwa " a constructive criticism" ambao ni ukosoaji mzuri, wenye afya katika ujenzi wa taifa lolote la kidemokrasia linaloheshimu uhuru wa kujieleza, (freedom of expression) na kuheshimu haki za binaadamu (human rights) kwa kuheshimu katiba na kufuata utawala wa sheria (the rule of law), taratibu na kanuni.

Serikali yoyote yenye nia ya dhati ujenzi wa taifa lake kwa kufuata misingi ya katiba nzuri na kuheshimu misingi ya haki binaadamu na utawala wa sheria!, inatakiwa kuheshimu sana katiba, uhuru, sheria, taratibu na kanuni, hivyo inakuwa makini sana na hoja zozote zinazohusu ukiukwaji wa katiba, sheria, taratibu na kanuni. Zikitokea kelele zozote zinazohusu ukiukwaji wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, au uminywaji wa demokrasia, serikali makini zote, huzichukulia hoja hizi very serious kwa uzito unaostahili, serikali yoyote inayopuuzia hoja za ukiukwaji wa haki zilizotolewa na katiba, then serikali hiyo sio serikali sikivu, ni serikali ya ki imla, na kama ni kweli katiba inakiukwa, then serikali hiyo ni serikali ya kidikiteta!, japo sio lazima uwe ni udikiteta mbaya!, na rais yoyote anayekiuka katiba aliyoapa kuilinda, huyo ni rais dikiteta japo pia sio lazima awe ni dikiteta katili au dikiteta mbaya, kuna madikiteta wema, madikiteta wazalendo, wanaoitwa bennovelent dictators . Vivyo hivyo Bunge linalokiuka kanuni zake, na kushindwa kuisimamia serikali, hilo ni Bunge Butu!. Jee Bunge letu ni Bunge Butu?, Linajipendekeza kwa serikali?.
Mihimili Mitatu ya Dola, Serikali, Bunge na Mahakama
Serikali nyingi za mataifa, zinazo heshimu katiba, na kufuata mfumo wa kidemokrasia na utawala wa sheria, zina mihimili mitatu ya dola ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama. Mihimili hii inatakiwa kuwa sawa kwa kufanya kazi kwa uhuru na kujitegemea bila kuingiliwa na Mhimili mwingine (independent) na wakati huo huo kila mhimili ukiwa ni mlinzi na mdhibiti wa mhimili mwenzake, (check and balance) ili mihimili mmoja usizidishe mamlaka yake na kuingilia mihimili mengine.

Kazi, Majukumu na Wajibu wa Mihimili ya Dola
Kwa wasiojua kuhusu kazi, wajibu na majukumu ya mihimili mitatu ya dola, watakipongeza kitendo cha taarifa ya kamati teule ya bunge kuwasilishwa kwa rais, badala ya kuwasilishwa bungeni, wabunge wakatoa mawazo yao, kisha bunge likatoa azimio la bunge ambalo ndilo lingewasilishwa serikalini na Waziri Mkuu, kisha Waziri Mkuu, akamkabidhi rais, azimio la Bunge, na sio mapendekezo ya Kamati Teule ya Bunge!.

Bunge Letu ni Bunge la Ajabu!, Wabunge Wetu ni Wabunge wa Ajabu
Kiukweli kabisa, wengi wa wabunge wetu, au baadhi ya wabunge wetu ni wabunge wa ajabu sana na wasiojielewa majukumu yao kama wabunge wamekwenda kufanya nini kule bungeni!. Hawa ni wabunge wa posho, ulaji, na wengine wako kule bungeni kutoa tuu huduma za kibinaadamu na sio kufanya kazi za kibunge za kuwawakilisha wananchi na kuisimamia serikali.

Wabunge wetu wanaojua majumu ya Bunge, wamewezaje kumuacha Spika, tena akiwa na Naibu Spika nguli na mbobezi wa sheria, kuliacha Bunge letu tukufu, kwenda kujipendekeza kwa rais wa JMT ambaye ni mhimili wa the executive?!. Kama moja ya majukumu ya bunge ni kuisimamia serikali, halafu Mkuu wa mhimili wa Bunge anakwenda kujipendekeza kwa Mkuu wa Mhimili wa serikali ambaye ni rais rais wa JMT, inapotokea serikali inakosea, au rais wa Jamhuri ya Muungano akatenda kinyume cha Katiba, kwa Bunge la kujipendekeza kama hili, litakuwa na uwezo kweli wa kuisimamia serikali, na kuiambia hapa mmekosea, au itakapotokea rais ni kweli amevunja katiba, bunge la aina hii, litakuwa na uwezo wa kumdhibiti rais wa JMT?!, au kumuondosha madarakani?.

Jee Ni Kweli Bunge Linajipendekeza Kwa Rais na Kwa Serikali?.
Naomba hili swali nisilijibu mimi, nisije kuitwa mbele ya kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge na kuambiwa nimelikashifu Bunge, bali nakuwekea tuu tukio lilitokea hivi karibuni, halafu majibu utayapata mwenyewe kama Bunge linajipendekeza kwa rais wa JMT, au linajipendekeza kwa serikali au la!.

Tukio la Spika Kuwasilisha Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge Kwa Rais wa JMT badala ya Bungeni, Tunaweza Kukiita Kitendo hiki ni Kunini?.
Kila Kitu Spika wa Bunge anachokifanya, kwa mamlaka yake kama Spika, kitu hicho kinakuwa kimefanywa na Bunge, kwa kanuni ya uwajibikaji wa pamoja, (a collective resiponsibilities) kama ilivyo kwa Rais ambaye ndiye Mkuu wa mhimili wa serikali, kila kitu ambacho rais atakisema au atakifanya kama rais wa JMT, kitu hicho kinakuwa kimefanywa na serikali. Spika anapounda Kamati Teule ya Bunge, kamati hiyo inakuwa imeundwa na Bunge. Taarifa ya Kamati hiyo Teule, ni taarifa ya Bunge na inatakiwa kuwasilishwa Bungeni, inajadiliwa na Wabunge, wanatoa michango yao, maoni yao na mawazo yao na mapendekezo yao, yanajumishwa na kutolewa azimio la Bunge ambalo sasa ndilo linawasilishwa serikalini kwa utekelezaji. Lakini hivi karibuni, Spika wa Bunge, amempelekea rais taarifa ya Kamati Teule ya Bunge, bila taarifa hiyo kuwasilishwa bungeni na kujadiliwa na wabunge!. Badala ya rais kupelekewa Azimio la Bunge, rais amepelekewa mapendekezo ya Kamati Teule!, wakati hayo yakifanyika, wabunge wetu makini na mahiri, na miongoni mwao ni wazoefu, wabobezi hadi manguli wa sheria, wapo wanaangalia tuu!, ukiwaita wabunge kama hawa ni watu wa ajabu, utakuwa umewaonea au umewakosea?. Hii kama sio ajabu ya mwaka ni nini?!.

Rais Magufuli Anapokea Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge Kama Nani?.
Kwa mujibu wa Katiba yetu, japo rais wa JMT ni sehemu ya Bunge kwa kuliunda, kulivunja, kulihutubia na kuteua Mtendaji Mkuu (Katibu wa Bunge), lakini rais sii mbunge na hahusiki na utendaji wa shughuli za kila siku za Bunge, hivyo alivyopelekewa ripoti ya Kamati Teule ya Bunge, kabla haijadadiliwa bungeni na kujumuisha maoni ya wabunge, rais amepelekewa ripoti ile kama nani?!.

Tena tumshukuru sana Mhe. Rais Magufuli kwa kutamka hadharani kuwa ameyapokea mapendekezo yote ya kamati teule ile na atayatekeleza kwa asilimia 100% kwa mia, utekelezaji huu ni kupitia mamlaka yake ya urais (discretionary powers) za rais wa JMT alizopewa na katiba yetu kuwa anaweza kupokea ushauri wowote na ana uhuru wa kuamua kuutekeleza ushauri wowote anaopewa, au kuamua kutotekeleza ushauri wowote anaopewa na yoyote kwa ridhaa yake, (at his discretion), na hata angeamua hawezi kutekeleza jambo lolote katika mapekezo hayo, hakuna mtu mwenye uwezo wa kumuuliza kitu rais.

Rais Anauwezo Wa Kuunda Tume, ni Tume ya Rais. Ana Uhuru Nayo.
Rais wa JMT anauwezo wa kuunda tume kuchunguza jambo lolote, hii ni tume ya rais. Matokeo ya tume hiyo, yanawasilshwa kwake. Kwenye Tume ya Rais, rais ndie mwenye uhuru atangaze matokeo ya tume hiyo, au asitangaze, na kwenye mapendekezo ya tume hiyo, rais yuko huru kuyapokea mapendekezo ya tume hiyo, kuyakubali yote au baadhi, kuyakataa yote au baadhi na hakuna mtu wa kumuuliza kwa sababu hiyo ni tume yake!. Tena katiba imempata rais wetu mamlaka ya kuteua wasaidizi, na inaelekeza kwenye baadhi ya maamuzi, rais atashauriana na wasaidizi wake, lakini katika kufikia maamuzi, rais hufikia maamuzi yeye kama yeye, ama kwa kufuata ushauri, au bila kufuata ushauri wa yeyote!.

Kamati Teule ya Bunge Sio Kamati ya Rais, Ushauri wa Kamati Teule Sio Ushauri ni Amri!.
Kamati ya Bunge inapofanya uchunguzi, kamati hiyo inakuwa na nguvu za kisheria na hadhi ya kimahakama, Quasi Judicial Committee, kama ilivyo mahakama inaposikiliza kesi au shauri, ikimaliza kusikiliza kesi, inatolewa hukumu, hukumu ikiishatoka inafuatiwa na utekelezaji, hivyo taarifa ya Kamati Teule ya Bunge, na mapendekezo yake, ni kama kuendeshwa kwa kesi, taarifa hiyo ilipaswa iwasilishwe bungeni ili mapendekezo hayo yajadiliwe na kutolewa hukumu kupitia Azimio la Bunge, azimio hili likitoka, linakuwa ni hukumu kwa serikali kulazimishwa kulitekekeza au kulipinga, kama ilivyo amri ya mahakama, utekelezaji wa maazimio ya Bunge, ndipo angepelekewa rais hapa sasa rais hapelekewi kama ushauri, au sio kuombwa bali hupelekewa kama azimio la Bunge, hii ni amri, sio kama ule ushauri wa rais kuwa huru kuufuata au kuupuuza, azimio la bunge ni amri kwa rais kuitekeleza kama amri ya mahakama!. Hapo ndipo Bunge linapoidhibiti serikali kwa kuiamrisha kutekeleza maazimio ya Bunge kwa amri na sio kwa ridhaa tuu! yaani sio at Presidents pleasures, but it is a must, na asipotekeleza, bunge linaweza kukutana na kuhitaji maelezo na ikibidi kumtimua!.

The Doctrine of Separation of Powers, Checks And Balance
Hii ni kanuni ya mgawanyo wa madaraka, kuangazia na kuzuia mhimili mmoja usivuke mamlaka yake. Kwa muda mrefu sana hapa nchini kwetu, tumekuwa na tatizo kwenye kitu kinachoitwa "The Doctrine of "Separation of Powers" and "Checks and Balances" kati ya mihimili hii mitatu ya dola, "The Legislature, The Executive and The Judiciary, ambavyo vyombo hivi vyote vitatu vinapaswa kuwa "huru bila kuingiliwa" "independence of its decisions" ili kila kimoja kiwe na nguvu zake chenyewe " powers" ambazo zimetenganishwa na kingine, "separations" ila pia vimepewa mamlaka ya kitu kinachoitwa "checks and balances" kama a watchdog of one another. Yaani mwangalizi wa mwenzake ili mihimili hii isivuke mamlaka yake, au ikitaka kuleta madhara, izuiliwe na one another!.

Mamlaka za vyombo hivi vitatu, "Powers" za Bunge, Serikali na Mahakama, hazipaswi kuingiliwa na chombo kingine chochote, kumaanisha maamuzi ya serikali ni ya serikali yanatakiwa kuheshimiwa na Bunge na Mahakama, maamuzi ya Bunge yanapaswa kuheshimiwa na Serikali na Mahakama na Maamuzi ya Mahakama, yanapaswa kuheshimiwa na Bunge na Serikali, lakini kila siku, tunashuhudia jinsi maamuzi ya vyombo hivi, yanavyoingiliwa na vyombo vingine na hata katika yale majukumu yake ya msingi ya kila muhimili!, yaani Bunge kazi yake ni kutunga sheria, Mahakama kazi yake ni Kutafsiri sheria, na Serikali kazi ni ketekeleza sheria!.

Kuingiliana kwa Majukumu ya Bunge, Serikali na Mahakama
Kumekuwepo kuingiliana katika majukumu haya ya msingi, hali inayoleta migangano ya kuingiliana kwa muda mrefu, mfano kazi ya kutunga sheria ni kazi ya Bunge, lakini Mahakama katika baadhi ya maamuzi yake, hujikuta imetunga sheria kupitia maamuzi au hukumu zake mbalimbali ambazo huleta kitu kinachoitwa "precedents" na serikali katika utekelezaji wa majukumu yake, hujikuta imetunga sheria kupitia "executive orders" mbalimbali zinazotolewa kupitia "waraka" na kutangazwa kwenye gazeti la serikali, "Government Gazette" hivyo kuwa sheria!, ambako huku ni kuingilia majukumu ya kibunge kutunga sheria, serikali nayo inatunga sheria, mahakama nayo ni mtunga sheria, na serikali za mitaa nazo ni mtunga sheria ndogo, "by laws"!. Hivyo kila chombo ni mtunga sheria na sii bunge pekee!.

Kazi ya mahakama ni kutafsiri sheria na dispensing of justice, yaani kutoa haki, lakini kuna vyombo kibao vya kiserikali, vinatoa hukumu na adhabu mfano baadhi ya Mabaraza, (Quasi Judicial Bodies) na baadhi ya Wakala za serikali, TCRA, Sumatra, Ewura, SSRA, etc, zimepewa mamlaka ya kimahakama, au mabaraza, hutoa maamuzi na hukumu, mfano Ewura aliwahi kuvifungia na kuvipiga fine vituo vya mafuta kwa kisingizio cha kuuza mafuta machafu, wamiliki wakaenda mahakamani, kwa hoja kuwa mwenye mafuta machafu ni supplier na sio wao, mahakama ikatupilia mbali uamuzi wa Ewura, na kuvifungulia, Bunge la Samuel Sitta likaingilia kati kuwa mahakama inaingilia uhuru wa Ewura na kuidhalilisha mbele ya jamii.

Kwenye jukumu la kutafsiri sheria, Mahakama ilitamka wazi baadhi ya sheria zinazotungwa na bunge ni "bad laws" na kutoa amri zifutwe kwenye vitabu vya sheria, "scraped out from the books of law" mfano haki ya mgombea huru, serikali ikangilia kati, na kufanya mabadiliko ya katiba na kukichomeka kipengele cha "mgombea lazima adhaminiwe na chama cha siasa", hivyo kuingilia uhuru wa mahakama, mahakama bado ikatamka kipengele hicho ni "unconstitutional" wanasheria nguli wakaitwa kama marafiki wa mahakama "amicus curiae" kuishauri mahakama kama ina uwezo wa kufuta kipengele cha katiba, wakakubaliana kuwa Mahakama, haina uwezo huo bali ni Bunge ndilo pekee lenye uwezo wa kubadili kipengele cha katiba!, hii issue iliwasha moto mkubwa sana wa majadiliano kuhusu uhuru wa mahakama na haki kinga na madaraka ya Bunge!.

Checks and Balance
Pamoja na kuwekwa kwa mipaka yote ya kutoingiliana, mihimili hii ya dola, imepewa mamlaka ya "checks and balance" kuingilia na kuuzuia mhimili mmoja usivuke mipaka ya mamlaka na madaraka yake kuleta madhara kwa taifa, hivyo vimepewa mamlaka ya kuingilia kati "intervention" pale inapoona mhimili fulani unajipa madaraka kuliko hata uwezo wake!. Mfano mzuri ni hali iliyopo Tanzania kwa sasa, Mkuu wa Mhimili wa serikali amejiinua mno kuliko hata katiba alyoapa kuilinda, na sasa sio tuu anajiinua katika utawala, bali pia anataka kujiinua hadi kuwadharau wakuu wa taasisi za kiimani kama Maaskofu. Hakuna kitu chenye nguvu kama imani, Dini ni imani, wakuu wa vyombo vya dini, wakikuandikia waraka, hata kama wamekukosea, jishushe kwa heshima na unyenyekevu kuwaeleza umewasikia, lakini sio kuwabeza. Kama hawa viongozi wa dini, ni viongozi wa dini za Mungu wa kweli na sio viongozi wa mungu tuu, na hoja kwenye waraka zao ni hoja za kweli, binadamu hawezi kubeza hoja za Mungu wa kweli kwa kuwabeza watumishi wa Mungu na akabaki hivi hivi!, hili ni jambo la wote wenye mapenzi mema na taifa hili, kuliombea heri taifa hili na kumuomba Mungu Baba, wasamehe tuu kwa maana hawajui watendalo. Mungu asamehe na kupishilia mbali!.

Uwezo wa Bunge na Kamati Zake
Bunge limepewa mamlaka na uwezo wa kutunga sheria yoyote, ila bunge kabla halijaitunga hiyo sheria, sheria hiyo inayopaswa kutungwa lazima kwanza ianzie kwenye "the Executive" na Bunge likiisha itunga hiyo sheria, sheria hiyo haiwi sheria hadi Mkuu wa "the executive" yaani rais, aridhie!, na kuisaini, "accent" asiposaini haiwi sheria!. Hivyo kwenye uwezo wa Bunge kutunga sheria, bunge ni kikaragosi tuu, the real powers lies with the Executive!. Bunge linaelezwa linayo mamlaka ya kumuondoa rais madarakani, "impeachment" na rais anaelezwa kuwa ni sehemu ya Bunge!, ila huyu rais amepewa mamlaka ya kuliunda bunge, kulivunja bunge wakati wowote!. Hivyo hata ikitokea tukampata rais dikiteta wa ukweli, akavunja Katiba na Bunge likaamua kumuondosha madarakani kwa impeachment, rais atalivunjilia mbali Bunge kabla halijamuondoa!.

Ingawa Mkuu wa Mhimili wa Bunge ni Spika, ambaye anachaguliwa na wabunge, Mtendaji Mkuu wa `Bunge ni Katibu wa Bunge, rais ndie anayemteua mtendaji Mkuu wa Bunge, kuna kitu kinaitwa nguvu, mamlaka na madaraka, kati ya spika na katibu wa Bunge, Spika kama mkuu wa mhimili wa Bunge, ana Mamlaka makubwa tuu ya kupiga kelele bungeni, lakini nguvu na madaraka ya kuendesha bunge kiuwezeshaji, ni Katibu wa Bunge, Spika lazima anyenyekee na kumpigia magoti katibu kumuomba fedha za uendeshaji, kama walivyo mawaziri lazima amnyenyekee Katibu Mkuu wake, where money lies, its where the real powers lies!.

Bunge Linapaswa Kuwa Independent
Bunge lilipaswa kuwa independent kuisimamia serikali, ikiwemo wabunge wasiwe mawaziri ili kuisimamia kikamilifu kabisa serikali kiukweli kweli haswa kama alivyopendekeza Warioba!, lakini wabunge wetu ambao tuliwachagua wakaisimamie serikali, ndio hao wamepewa uwaziri, "ulaji!", kuna cha usimamizi tena hapo?!, unaweza kumlinganisha Mwakyembe yule wa Kamati ya Richmond na Mwakyembe huyu waziri?!, au umlinganishe Prof. Kabudi wa Tume ya Warioba na Prof. Kabudi waziri?. Msimamizi unapopewa ulaji, unategemea utasimamia nini?!, hivyo hiyo independence of the parliament is also nothing!, just a myth!.

Mahakama ni Huru?.
Mahakama nayo is said to be independent!, uamuzi wake ni wa mwisho!, Mkuu wa Mahakama anateuliwa na rais!, ile tuu kuteuliwa na mkuu wa nchi, tayari ume compromise uhuru wa mahakama dhidi ya serikali, Jaji Mkuu, lazima awe ni mtu wa shukrani kwa rais kumpatia ulaji!. Mahakama haina vote yake separate kwenye budget, bajeti ya mahakama iko chini ya wizara ya sheria!, ili mahakama itekeleze majukumu yake, kila wakati, Jaji Mkuu lazima awe mdogo, kwenda kunyenyekea kwa The Executives kuomba hela za kutoa haki, inapotekea serikali haijatenda haki, kweli unaitegemea mahakama hii as beggars as it is inaweza kuihoji serikali?!. Mahakama ikitoa hukumu ya capital punishment , hukumu hiyo haiwezi kutekelezwa hadi mkuu wa the executive asaini!. Kitu kikubwa na kibaya kuliko vyote kwenye uhuru wa mahakama ni jamaa mmoja kwenye the executive anaitwa DPP!, huyu ana mamlaka ya kuingilia kesi yoyote, mahakama yoyote, na ikiwa katika hatua yoyote kabla hukumu na kuifuta!, "nolle" bila kutoa maelezo yoyote wala sababu zozote, na uamuzi wa DPP ni wa mwisho, hauwezi kuhojiwa na mamlaka yoyote!. Hivyo kitu kinachoitwa uhuru wa mahakama is nothing but a myth!.

The Myth of "The Doctrine of Separation of Powers and Checks and Balances",
Kiukweli hii doctrine "The Doctrine of Separation of Powers and Checks and Balances", ilikuwa iko supposed kuwepo kiukweli ukweli, ila kiuhalisia, hakuna kitu kama hiki, its just a myth, serikali ndio kila kitu!, hakuna mahali popote bunge na mahakama zina total independence!, serikali ndio mambo yote, hivyo hili bunge letu, ni bunge zuga tuu mbele ya serikali, na hizi mahakama zetu, ni mahakama zuga tuu mbele ya serikali, serikali ndio mambo yote!, sasa inapotokea hivyo vyombo viwili ambavyo vyote ni zuga tuu vinata kupimana ubavu kwa jambo ambalo mtuhumiwa mkuu ni serikali, unategemea nini?.

Hili la Bunge Kujipendekeza Kwa Serikali ni Kubwa Kuliko!.
Wengi Kati ya yote niliyowahi kuyashuhudia katika hoja hii ya the separation of powers, na Checks and Balance, kubwa kuliko ni hili la Bunge kujipendekeza kwa serikali, ni kuwa Bunge linawajibu wa kuisimamia serikali, kamati teule za Bunge huundwa pale serikali inapofanya madudu, taarifa ya kamati teule ya Bunge ni taarifa ya mhimili wa Bunge na sio taarifa ya yule yule aliyefanya madudu, yaani serikali, na inapaswa kuwasilishwa Bungeni, na mapendekezo yake, kisha waheshimiwa wabunge waijadili na kuyakubali mapendekezo, kuyapunguza, au kuyaboresha, kisha linatolewa Azimio la Bunge ambalo sasa ndilo linalopaswa kuwasilishwa serikalini kwa utekelezaji wa lazima. Kitendo cha taarifa ya Kamati Teule ya Bunge kuwasilishwa kwa rais Magufuli, sio jambo la kawaida ndio maana nimeuliza, huku sio kujipendekeza?.

Kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge, Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge inapaswa kuwasilishwa Bungeni na kujadiliwa

122.-(1) Kamati Teule itatoa taarifa Bungeni kuhusu maoni na uchunguzi wake pamoja na kumbukumbu za ushahidi uliopokelewa na vilevile inaweza kutoa taarifa maalumu juu ya mambo yoyote ambayo itaona yanafaa kuwasilishwa Bungeni. (2) Taarifa ya Kamati Teule itawasilishwa Bungeni na Mwenyekiti. (3) Iwapo baada ya hoja kutolewa, Bunge litaamua kujadili taarifa hiyo, hoja itakayotolewa Bungeni itakuwa ni kwa madhumuni ya kuliomba Bunge likubali mapendekezo yaliyomo katika taarifa hiyo. (4) Bunge linaweza kuamua vinginevyo kwa kutumia utaratibu wa kubadilisha hoja ambao umeelezwa katika Kanuni ya 57 ya Kanuni hizi. (5) Katibu wa Kamati Teule ataweka kumbukumbu zinazoonesha majina ya Wajumbe waliohudhuria mikutano ya Kamati na maamuzi yaliyofanyika.

Kwa kumbukumbu zangu, please correct me if I'm wrong, Taarifa iliwasilishwa kwa mujibu wa kanuni 122 (2), baada ya kuwasilishwa, ilibidi kanuni 122 (3) ifuatwe kwa Bunge kujadili, hapa linazungumzwa Bunge ndilo lililopaswa kuamua kujadili au la na sio spika kuamua!, kumbukeni Spika ni Spika na Bunge ni Bunge, Spika hawezi kujigeuza yeye ndio Bunge na kuzuia taarifa ya kamati teule isijadiliwe Bungeni!. Spika alipaswa kuliuliza Bunge lijadili, na kama kama kuna hoja kuwa taarifa hiyo isijadiliwe, then ingetumika kanuni ya 122(4) ambayo inaliruhusu Bunge kutojadili na kuibadilisha hoja.

Kama Spika ametumia kanuni 122 (4) ya Bunge lisijadili, then uamuzi huu ungefuata kanuni ya 57 ya kubadilisha hoja kwa kuibadili jina isiitwe tena kuwa Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge, bali ibadilishwe hoja iitwe Taarifa ya Kamati ya Rais, na itawasilishwa kwa rais, na sio tena Taarifa ya aKamati Teule ya Bunge, kwa sababu taarifa ya Kamati Teule inawasilishwa na kujadiliwa na Bunge, taarifa ya rais ndio inakabidhiwa kwa rais.

Ili hili liweze kufanyika, ingebidi kanuni hii ifuatwe

57.-(1) Hoja ikishatolewa ili iamuliwe inaweza kubadilishwa kwa:- (a) kuondoa maneno fulani kwa ajili ya kuingiza maneno mengine; (b) kuondoa maneno fulani bila kuongeza mengine; au (c) kuingiza au kuongeza maneno mapya.

Sina kumbukumbu ya hili kufanyika na sikusikia likiripotiwa na media yoyote!. Kwa vileBunge letu linafanya baadhi ya mambo kwa kujifungia, kama hili lilifanyika lakini halikuripotiwa, then taarifa iliyowasilishwa kwa rais, ilipaswa iwe na jina jingine!, Tangulini rais ambaye sio mbunge akapokea taarifa ya Kamati Teule ya Bunge badala ya kupelekewa Azimio la Bunge?.

Wabunge wetu walilikubalije hili la Spika kujigeuza Bunge na kuamua kwa niaba ya Wabunge wote, huku waheshimiwa Wabunge wetu wakiwa wanaangalia tuu, like worshipers waiting for their priest, longed to hear him pray their minds away?!. Kama Spika ndiye mwenye uwezo wa kuwafahamu wabunge wote, their abilities and capabilities, halafu Spika huyo anapiga simu kwa rais Magufuli kumuuliza nimteue nani?, "Mh spika, nakumbuka ulinipigia simu ukaniuliza utachagua nani?, nikakujibu Mungu atakuongoza", then huku ni kujipendekeza gani?, huku ni zaidi ya kujipendekeza!, ni kujikomba!. (Magufuli naye huyu bana hana siri!). Sasa kama Spika anajikomba kwa rais hadi kumpelekea Ripoti ya Kamati Teule badala ya kumpelekea Azimio la Bunge!. Kiukweli nimemkumbuka Sitta (RIP). Kwa maoni Mhe. Job Ndugai ndie awe spika wetu wa mwisho asiye mwanasheria!.

Bunge la Ajabu, Wabunge wa Ajabu, Mnatupeleka Wapi?.
Tukisema Bunge letu ni Bunge la ajabu, tutakuwa tunalionea?, tukisema Wabunge wetu ni wabunge wa ajabu, tutakuwa tunawaonea?!. Nimepitia kanuni za Bunge, sikufsanikiwa kuona popote ni kanuni ipi ilitumika kuiwasilisha ripoti ya Kamati Teule ya Bunge kwa rais!.

NB. Bunge pia linayo mamlaka ya kutengua kanuni yoyote ili kufanya jambo lolote lililo inje ya kanuni, sikumbuki kama kulifanyika utenguaji wowote wa kanuni, kuruhusu ripoti ya Kamati Teule ya Bunge kuwasilishwa kwa rais bila kujadiliwa na Bunge na kutolewa Azimio la Bunge.

Mhilimili Uliojichimbia Chini Zaidi, Sio Tuu Umechichimbia Chini Tuu, Hata Juu, Umejichimbia Juu Karibu na Mungu, Maaskofu Wako Chini?.
Siku sisi waandishi tulipoalikwa Ikulu (mimi kwa mara ya kwanza na nadhani ya mwisho, kwa sababu maswali yangu hayakujibiwa), nilipopata fursa ya kumuuliza maswali rais, niliulizia baadhi ya mambo rais wetu anayo yafanya, anayafanya kwa mamlaka ipi na vifugu gani?, (hili tutamalizana vuzuri na Prof. Kabudi) ila pia niliulizia kuhusu separation of powers kati ya mihimili ya dola, ndipo rais akanijibu kuwa japo mihimili yote ni sawa, lakini upo mhimili mmoja uliojichimbia chini zaidi!, kumbe mhimili huu sio tuu umejichimbia chini zaidi, unawezekana hata kwa upande wa juu kuelekea mbinguni kwa Mungu Baba, unaweza kukuta mhimili huu pia umejichimbia juu zaidi, uko karibu zaidi na Mungu Baba, na maaskofu wako chini?.

Jee Rais Kaliingilia Bunge?. Jee Kaiingilia Mahakama?.
Rais Magufuli alipoingia tuu madarakani, kwa kuifuta ile tafrija mchapalo ya Bunge, sio kuliingilia Bunge?. Kitendo cha rais ambaye ni mkuu wa mhimili mmoja na kuamuru fedha za sherehe ya mhimili mwingine zikanunue vitanda vya wajawazito pale Hospitali ya Muhimbili, huku sio kuiingilia mhimili mwingine?. Japo hili ni jambo jema, ni jambo zuri na ni jambo la heri, lakini rais kama mkuu wa mhimili mmoja, anawezaje kuingilia mhimili mwingine kwa kumuamuru fedha za tafrija zikanunue vitanda?!, huku sio kuliingilia Bunge?!, rais sio mbunge, sio Mkuu wa mhimili wa Bunge anawezaja kuingilia mambo ya ndani ya Bunge?!.

Kuna Kitu Kinaitwa Eyes On Hands On, na Eyes On, Hands Off.
Eyes on hands on ni kanuni ya serikali kufungua jicho lake na kuingiza mikono yake ndani, na Eyes on hands off, ni kanuni ya kufungua jicho tuu kutazama kinachoendelea, lakini bila kuingiza mikono yake ndani. Kwenye Bunge na Mahakama, serikali jukumu lake eyes on, hands of, jukumu lake ni kutoa fedha lakini sio kuziingilia katika utendaji wa ndani. Hili la Bunge kuingiliwa, Independence itatoka wapi?!. Jambo kama hili lihitaji ustaarabu unaoitwa decency kwa rais kumuita Spika na kumshika sikio kuwa wabunge hamuwezi kuteketeza mahela yote haya kufanyia karamu, huku wamama wajawazito wetu wakilala chini!, aliyepaswa kutangaza uamuzi wa kuifuta sherehe ya wabunge ni Spika na sio rais!.

Jee Marufuku ya Kusafiri Nje, Inamdhalilisha Spika na Jaji Mkuu?.
Rais alipopiga marufuku kusafiri nje ya nchi kwa maofisa wote wa serikali bila kibali chake, amri hiyo sio tuu iliingilia uhuru wa mahakama, bali sio alidhalilisha hadhi ya Jaji Mkuu na hadhi ya Spika wa Bunge?!. Yaani Jaji Mkuu wa Tanzania ambaye ni Mkuu wa Mhimili wa Mahakama, anaamrishwa na rais kuwa akitaka kusafiri nje, ni lazima akapige magoti kuomba ruhusa kwa Mkuu wa mhimili mwingine!, Tena ruhusa hiyo inaanzia kumpigia magoti Katibu Mkuu Kiongozi!, anaomba kibali kwa rais kusafiri!. Hata kama nia ya rais ni njema kudhibiti safari za nje zisizo na manufaa na kubana matumizi, hapa kulihitajika respect kwa Mkuu wa Mhimili wa Mahakama, kuwa Jaji Mkuu akitaka kusafiri, hapaswi kuomba ruhusa bali kutoa tuu taarifa!, tena kistaarabu zaidi, hata kama ni kweli maombi yote lazima kibali atoe yeye rais, lakini kwa Mhimili wa mahakama, walipaswa kuomba kibali kwa Jaji Mkuu na Mhimili wa Bunge waombe kibali kwa Spika, ili majaji wamrespect Jaji Mkuu na Wabunge wamrespect Spika kuwa ndio mamlaka yao, halafu maombi hayo yanaletwa kwa rais kimya kimya!.

Mambo ya Majaji Kuomba Vibali Kusafiri, ni Jambo Likazua Jambo!.
Haya mambo ya majaji kuomba kibali kwa rais hata cha kwenda tuu likizo!, kisha rais anawatuma "wajomba" kufuatilia amesafiri na ndege gani, amesafiria daraja gani?, amefikia hoteli gani?, ya ya kiasi gani na account yake ina kiasi gani?, kunatuma ujumbe gani kwa wajeshimiwa majaji wetu on their rights to privacy?. Kila mtu anajua serikali zote zinawachunguzaga watu wake, ikiwemo kusikiliza simu zao, na kuwafuatlia watu wote wenye mashaka!, kama hata majaji ambao ni walinzi wa amani, nao wanafuatiliwa, then nani hafuatiliwi?. Japo mambo haya yapo lakini mambo haya asemwagi hadharani!, tena of all the people majaji?!, Hawa ndio watu wenye kuweza kupokea mashitaka juu ya rais, impeachment, majaji ndio wanaosikiliza ya mashauri mazito ya kiserikali kama mtanisahe sijui Kiwahili chake, ila Mashauri haya yanaitwa prerogative orders za certiorari, habeas corpus, mandamus, prohibition,, procedendo, quo warranto, scire facias,
ambapo mahakama inamuamuru rais na serikali kufanya jambo fulani kwa lazima, au kumzuia rais na serikali asifanye jambo fulani!, kama rais Magufuli amewaweka majaji na mhimili wa mahakama katika mazingira kama haya, likija shauri kama kuhitaji tafsiri ya kisheria kama rais amevunja Katiba au laa, hata kama ni kweli atakuwa amevunja Katiba, kuna Jaji kweli wa kutoa uamuzi kuwa rais amevunja Katiba?. Hili kwa ufafanuzi, nitamtafuta Jamaa yangu mmoja, aliyekuwa Dean wangu pale Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiiitwa Dr. Ibrahim Juma Enzi hizo, au nitamtafuta supervisor wangu wa LL.B Dissertation, wakati huo Prof. Palamagamba Kabudi kulifafanua hili, au kumtafuta Nguli Prof. Shiviji.
Kupiga Marufuku Bunge Live, na “Wee Washughulikie Huko, Wakija Huku Nitawashughulikia!”.
Niliwahi kumsikia kwa masikio yangu mwenyewe rais Magufuli akisema kuhusu kusitishwa kwa Bunge Live!, Rais aliwahi kumpongeza Spika wa Bunge kwa kuwashughulikia Wabunge na kumuamuru "Wewe washughulikie huko, wakija huku mimi nitadeal nao”, hivi kuna mbunge yoyote aliwahi kutaka ufafanuzi, huko kushugulikiwa huku nje ni kushughulikiwa vipi?!. Msikilize mwenyewe


Wabunge Ndani Wanashughulikiwa Ipasavyo na Huku Nje Wanashugulikiwa Barabara!.
japo haikufafanuliwa wabunge washughulikiweje, au kivipi, lakini kinachoonekana ni kweli wabunge kule ndani ya Bunge, wamekuwa wakishunguliwa ipasavyo, na hata makazi rasmi ya waheshimiwa Wabunge ambalo ni kama eneo la Bunge, pia wanashughulikiwa!, tumeshuhudia wabunge wakikamatwa bungeni bila taarifa kwa Spika!.

Japo mimi siamini jinsi Lissu alivyoshughulikiwa ndiko kushughulikiwa kwenyewe!, Lissu yeye ameshambuliwa na watu “wasiojulikana”, ila huku nje, kiukweli kabisa, kila mwenye macho, anaona jinsi baadhi ya wabunge wanavyoshughulikiwa kikamilifu!.

Hawa Maaskofu Waliotoa Waraka, Ni Kweli Kuna Vitu Wameona au Wametumwa?.
Jee ni kweli Tanzania imefika kiwango hata wenye busara viongozi wetu wa dini, Maaskofu kuna vitu wameona haviko sawa hadi wametoa waraka, ni kweli kuna vitu wameona au wametumwa tuu?. Wanaodhani kwa kunyamazia haya, ndio utii, uaminifu na kulisaidia taifa, they are doing a terrible mistakes, na sisi tunaosema au kukosoa, msidhani ndio hatulitakii mema taifa letu na rais wetu Magufuli!. No, tunalitakia mema sana taifa letu, tena unaweza kukuta sisi tunaomkosoa rais Magufuli na serikali yake na mihimili ya Bunge na Mahakama, ndio tunamsaidia zaidi rais na kuisaidia nchi yetu, kuliko hao wanaomuimbia nyimbo za shangwe, sifa na mapambio kwa kumsifu tuu kila analofanya na kila analotenda hata kama sio!.

Wabunge Wetu, Amkeni, Timizeni Wajibu Wenu Kilichowapeleka Bungeni.
Kama Mhimili wa Bunge letu tukufu linaweza kufanya mambo kama haya na au kufanyiwa haya huku wabunge wetu wamenyamaza, Mhimili wa Mahakama ndio huo majaji wanadukuliwa maisha binafsi na kutangazwa hadharani kuwa wanadukuliwa!, Mkuu wa The Executive ndio huyu analalamikiwa kuikanyaga katiba aliyeapa kuilinda, kuitetea na kuitekeleza, jee tutegemee nini kwa Bunge Letu?, linauwezo kweli wa kuisimamia serikali?, au ni kweli kwa sasa mhimili mmoja uliojimbia chini ndio kila kitu?, Mkuu wa mhimili huo ndie Mkuu kivuli wa mhimili wa Bunge kwa sababu ndie anayetoa hela?!, ndie Mkuu kivuli wa mhimili wa Mahakama kwa sababu ndio anayeipa hela?.

Mungu Ibariki Tanzania.

Wasalaam

Paskali
 
Du, si mchezo, umenikumbusha kisa cha mti na Mfalme Nebukadreza!

"Here is my dream; interpret it for me. These are the visions I saw while lying in bed: I looked, and there before me stood a tree in the middle of the land. Its height was enormous. The tree grew large and strong and its top touched the sky....Belteshazzar answered, “My lord, if only the dream applied to your enemies and its meaning to your adversaries! The tree you saw, which grew large and strong, with its top touching the sky, visible to the whole earth, with beautiful leaves and abundant fruit, providing food for all, giving shelter to the wild animals, and having nesting places in its branches for the birds— Your Majesty, you are that tree!" - Bible Gateway passage: Daniel 4 - New International Version
 
Paskali, nimesoma headlines tu maana bado sijanywa kahawa ila kusoma vichwa naweza elewa unachotaka kusema ingawa kwa asilimia 2. You are right. Je, kuna bunge au viini macho? Wabunge wapo Lupango au wamevunjwa miguu wengine ndo mhu! Hivu Mbatia yupo au? Nauliza tu.
 
Ni bora tungelifunga bunge tuwe na mhimili mmoja Tu Serikali, Wanapoteza fedha na kodi kama wale waliokuwa wanauliza mara mambo ya Taifa mtu kavaa wigi seriosly ?

Yule mungine eti anauliza mambo ya darasa la saba kurudi kazini huku akijua walishakatwa meno zamani

Gharama tunapoteza nyingi kwenye bunge lililojaa wajinga ambao wanapitisha sheria kama Nape Nnauye halafu zikianza kuwasulubu wanahamia Tweeter ni upuuzi
 
Usitegemee lolote la maana toka kwa Wabunge wanaoongelea Mawigi kwenye Nembo ya Taifa.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
Pascal, Mkuu usiite bunge sema genge la "Wasiojielewa "waliokutana pamoja ili kufanya vichekesho

Wamekaa bungeni wakisubiri Serikali imesema nini ili na wao waanze kupaka rangi na nakshi yaliyoletwa na serikali
 
Lile ni genge la comedian wapo mjengoni hakuna kitu pale.wanafanya vitu vya hovyo hovyo mara cjui wigi la mwanamke kwenye nembo ya taifa oh sanamu ya mnazi moja yani ni full drama.ni bora ifutwe hzo pesa tununulie madawa
 
Naunga mkono hoja Bunge uchwara limepoteza kabisa umuhimu wa kuendelea kuwepo maana hakuna tena mijadala ya tija ndani ya Bunge. MACCM jiwe limewatisha kwamba litawaumiza, Wapinzani hawana RUKHSA ya kuzungumza kila wanachotaka kuzungumza ndani ya Bunge hawaruhusiwi. Yanini basi kuendelea kuwa na hili dubwasha ambalo linakula mabilioni kila mwaka lakini halina faida yoyote ile kwa Watanzania.

Ni bora tungelifunga bunge tuwe na mhimili mmoja Tu Serikali, Wanapoteza fedha na kodi kama wale waliokuwa wanauliza mara mambo ya Taifa mtu kavaa wigi seriosly ?

Yule mungine eti anauliza mambo ya darasa la saba kurudi kazini huku akijua walishakatwa meno zamani

Gharama tunapoteza nyingi kwenye bunge lililojaa wajinga ambao wanapitisha sheria kama Nape Nnauye halafu zikianza kuwasulubu wanahamia Tweeter ni upuuzi
 
Kwa miaka takribani 10 na ushehe bunge limekuwa sio chombo cha uwakilishi wa shida za wananchi bali ni jamvi la kujitafutia umaarufu wa kisiasa...Sehemu ya kupigia hela kupitia kamati au posho mbalimbali.
Wabunge wengi wameingia huko kwa kutarajia haya.

Ndio maana kwa sasa wananchi wanazipeleka shida zao direct kwa Rais au Waziri mkuu ili zishughulikiwe.
 
Kwa miaka takribani 10 na ushehe bunge limekuwa sio chombo cha uwakilishi wa shida za wananchi bali ni jamvi la kujitafutia umaarufu wa kisiasa...Sehemu ya kupigia hela kupitia kamati au posho mbalimbali.
Wabunge wengi wameingia huko kwa kutarajia haya.

Ndio maana kwa sasa wananchi wanazipeleka shida zao direct kwa Rais au Waziri mkuu ili zishughulikiwe.
Pumba nyingine bwana..
Wananchi wangapi wanaopata hiyo nafasi ya kumueleza Rais na PM shida zao direct??
Ni kwenye ile mikutano ya hadhara kama yule Mama wa Morogoro??
Mamilioni ya Watanzania wana shida lukuki wangapi wamezifikisha kwa Rais na PM.??
 
Paskali Bunge limejipoteza lenyewe kwa uzembe wa wabunge wenyewe.
Wabunge wa CCM walijioni ni wabunge wa serikali na si wabunge wa wananchi waliowapigia kura kukaa mjengoni.

Wameuza ukubwa wao kama Esau alivyomuuzia Yakobo ukubwa wake kwa sahani moja ya mchuzi rojorojo.

Waliemuuzia ameishawadhibiti na ataendelea kuwatumia kama punda pale atakapowahitaji na si vinginevyo.

Kuna siku atakuja mtu kuwaambia wananchi kuwa bunge ni mzigo wafanye kazi ya kujitolea hadi pale tu watapoingia mjengoni tu.

Upande wa wabunge wapinzani nao wamejifanya much know wakaangukia pabaya,badala ya kukaa focused on big issues wamejikuta saa zote wanaingia matatani na utawala wa Magufuli na kukosa mwelekeo.

Mimi sioni kama hili Bunge letu la awamu hii kuzaliwa mara ya pili,labda bunge lijalo likiwa na muundo mpya,mawazo mapya na labda mazingira mapya.
 
Back
Top Bottom