Bundi CHADEMA kapewa kigoda

we mtoa mada unatoka katika chating site ya The grid.

Ndugu yako Eng. Mayeye ameona hapamfai humu kaondoka.

Sasa wewe unataka kusema nini???????
 
we mtoa mada unatoka katika chating site ya The grid.

Ndugu yako Eng. Mayeye ameona hapamfai humu kaondoka.

Sasa wewe unataka kusema nini???????

Tunazungumza suala nyeti hapa mkuu, mimi na mayeye wapi na wapi tena. Lakini Muziki si unausikia. CDM Viongozi ni wasikivu na wao wameishaiona hatari licha ya yule mwendawazimu kutishia ati atamwaga mboga, ishakuwa fashion ukibanwa unatishia kumwaga mboga, lakini kama kweli hiyo mboga ipo aweke hadaharani tujue,

Nareje maneno yangu ya awali katika thread hii, UNAFIKI wa wanasiasa ni hatari sana kwa demokrasia ya kweli, tunataka wazungumze nasi lugha moja.
 
Hiyo ya ku-go out ni ndoto za Alnacha, bado CCM itaendelea kukutawala hata ukiongea kwa jazba. na Rais wa Tanzania mwaka 2015 ni Edward N. Lowasa.


Off course huu ni mtazamo wa jukwaa la kijani, hatuna pingamizi na hilo...itakuwa tu kama hadithi ya GORDON BROWN na TONY BLAIR
 
we mtoa mada unatoka katika chating site ya The grid.Ndugu yako Eng. Mayeye ameona hapamfai humu kaondoka.Sasa wewe unataka kusema nini???????
we the grid mbona mwake huko koleo unaliita koleo ni full freestyle No ban wala nini unasema kitu unachotaka it is free
 
Mkuu kuchukua hatua kwa taratibu za chama ni sahihi ila uoga wangu ni hapo anapojitokeza Mwenyekiti na Naibu Katibu Mkuu na kusema Shibuda ni Muasi na atafukuzwa. Si tusubiri vikao vikae vitoe tamko. Mimi bado naamini kuwa swala la posho ni bomu ambalo limetua CHADEMA na Shibuda hayupo peke yake hivyo ni vyema tukasubiri maamuzi ya Chama na si kauli za viongozi. Kiongozi mzuri anayejua uongozi akiulizwa swala kama hilo ni vizuri kusema tutalizungumza katika vikao vya Chama kwa kuwa Kiongozi hana madaraka ya kumfukuza mwanachama kama afanyavyo kwa mchungaji wa ng'ombe wake nyumbani.

inashangaza sana viongozi kujitapa namna hiyo inamaana hata kwenye vikao cha kukmjadili Shibuda utatumika u dikteta.
hata kauli ya Dr Slaa ya kusema madiwani wa Arusha wamekosea na wanaweza fukuzwa wakati huo huo anaunda tume ni kichekesho. hivi hiyo tume ikisema hawakukosea nini kitatokea? au wanaenda kukusanya data ambazo tayari wanamajibu yake?
 
Mleta hoja niyo anataka kutuaminisha CDM ina watu wao.....yeye akiwemo kwasababu anasema amehusika kukisimamisha...na anasema tusimuulize kivipi.Lakini mambo haya si mara ya kwanza kutokea, issue ya ZITTO ilisemwa sana na watu wakaenda mbali zaidi na kusema bwana ZITTO amepewa mlungula na mapacha watatu ili aidhoofishe CDM. yako wapi sasa?My point is, kuna taratibi za kushughulikia mambo haya, viongozi wa kambi ya upinzani (Mbowe, Zitto na Lisu) wote wamesema vizuri sana kuhusu jambo hili - Gazeti la mwananchi amabalo mtoa hoja hapa kaanzishia thread tofauti.Wasiwasi unatoka wapi? Kambi ya upinzani inatakiwa kumshughulikia kwanza, then wakiona kuna ulazima basi, Chama kitajulishwa na taratibu za kinidhamu zitafuata.
Mkuu umenena kwa weledi wa hali ya juu. Nilitaka kuacha kuchangia kwenye mjadala huu kwakuwa mtoa mada analazimisha mawazo yake tuyakubali wakati wenye akili tunaona ni upupui tu.Kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani. Na chadema imejiwekea mkakati wake wa kudeal na kenge wanaovamia msafara. Ni ujinga kusema bundi anaunguruma chdm kwa kurefer tukio la Shibuda kupinga posho.Nilitegemea tuelezwe bundi yupo ccm kwa sababu ni wazi kabisa mkakati wa kuvua gamba kama utatekelezwa kama tunavyoaminishwa lazima chama kipasuke lakini sio chadema kwa ishu za posho
 
Ni heri ya Ubundi wa Chadema kuliko unguruwe wa CCM, maana wametafuna mihogo yote, viazi vyote na wameuza kila kitu handsome hana cha kusema siku hizi kabisa. No way they can remain in 2015 they must go out to restart a fresh. Chadema is comited and hakuna njia yoyote unaweza kutudanganya na propaganda za kujivua magamba alihali no electricity, no water no madawati shuleni na unatuletea tabasamu kila siku lol tumekuchoka umeshazeeka. CCM sasa imezeekaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.

Bange mbaya sana, hasa kuvutia chooni kama huyu
 
Huyu mkuu amejiunga JF 10/6/11 yaani siku 19 tu zilizopita, anapost 184 na amejishukuru mara 40 kwenye post 23!!

Lakini kitu gani hasa kinamfanya huyu mkuu aweweseke namna hii? raia wa nchi hii wamefaidikaje na miaka 50 ya ccm madarakani?

1. Umeme
kwenye hii dunia ya karne ya 21 ya sayansi na technologia, vijiji vingapi vya nchi yetu vina umeme?

2. Afya
ni aibu kubwa hadi leo baadhi ya wake zetu kudhulika kwenye uzazi, matitizo kama ya Fistula (VVF) yalishasahauliwa kabisa kwenye nchi zilizoendelea na zinazoendelea, actually ni mojawapo ya vipimo ya nchi fukara isiyoweza kuwapatia wananchi wake huduma za afya. Hapo hujaongezea na kipindupindu, surua, malaria, TB, utapia mlo nk magonjwa ya umasikini ambayo yanaendelea kushamiri tanzania miaka 50 ya kujitawala, Hospitali mbovu, chafu, zisizo na vifaa vya kisasa? madaktari uchwara kitaaluma (daktari aliyesoma Muhimbili ni daktari UPE, yaani ni kama wale walimu wa UPE wakati wa mwalimu)

3. Elimu
tujilinganishe na majirani zetu Kenya na Uganda. Sisi tuna elimu mdundiko

4. Usafiri
reli?, ndege?, barabara za lami? viwanja vya ndege? meli? usafiri wa mijini? ustaarabu wa kupanda vyombo haba vya usafiri yaani watu wazima kupigana vikombo wakati wa kuingia kwenye madaradara au mabasi? utumiaji wa magari mitumba na uchafuzi wa hewa mijini (air pollution)? wachache wanaweza kununua magari mapya? Mkuu naomba uwambie ccm waache mara moja kukiita kiwanja cha ndege mwanza International Airport, pamoja na kwamba watanzania ni mazezeta lakini uzezeta mwingine kama huu wa kukiita hiki kiwanja cha mwanza international airport unavuka mipaka.

6. Maji
Haa haaa haaa haaaa! pamoja na kuwepo mito, maziwa, bahari na mvua zinazo sababisha mafuriko, nchi haiwezi kutoa huduma ya maji bora hata kwenye makao makuu yake? Haa Haaa Haaaaaa Haa aha!!!!!!!! achilia mbali vijijini. rafiki yangu kijijini kwao ni pembeni mwa ziwa victoria, mwezi uliopita alitumia millioni 2 kuchimba kisima nyumbani kwao???? sasa anatafua solar ya umeme na pump ya maji, jamani ile kitu inayoitwa serkali iko wapi?

5. Makazi ya watu
unplanned, mitaa ya vumbi na matope isiyo na taa? Hakuna sewage system, kila mwenye kujenga nyumba anajenga septic tanks na kuishi na mavi yake mwenyewe uani kwake

6. wafanyakazi wa serkalini
wavivu? wana elimu duni, hawajui wanachofanya? hawalipwi mishahara inayokidhi mahitaji yao ya kimaisha? kila mfanyakazi wa serkali ni potential thief?

7. viongozi wa ngazi za juu serkalini (raisi, mawaziri, makatibu wakuu nk)
elimu duni (elimu ya tanzania), uwezo mdogo, hawajui walitendalo

8. Maisha ya mwananchi wa kawaida kijijini
Ni jehanamu, hakuna anayejali, ujanja ni kukimbilia mijini na kuwa machinga wenyewe wanasema "tutabanana humu humu"?

Mkuu sababu gani hasa inakufanya uwachukie wale ambao wanajaribu kubadilisha hii hali angalau iwe nafuu kwa watu? Future ya nchi hii ipo namna hii:
1. As long as ccm wako madarakani hali na maisha ya watanzania yatabakia ama kama yalivyo au kudidimia zaidi
2. vyama vingine vikipata nafasi ya kuunda serkali vinaweza kurekebisha kasoro za ccm na kuinua maisha ya watu au vinaweza kuwa worse than ccm.

Sasa hapa ndipo panapo hitaji maarifa yaani uogope kuchukua hatua na uendelee kudumaa na kudumaa zaidi au uchukue hatua ambayo inaweza kukuinua au kukuangamiza kabisa. The future belongs to the brave and those who dare to take risk. Hata kwenye biblia bwana Yesu alitoa mfano ya taranta, yule mtumishi aliyepewa taranta moja akaogopa kuitumia na kuishia kuifukia ili mkuu wake atakaporudi amkabidhi talanta ileile alilaaniwa kwa kufanya hivyo siku mkuu wake aliporudi, alinyanganywa taranta na akapewa yule ambaye alichukua risk ya kuzifanyia biashara talanta za mkuu na kutengeneza faida.

Mzee inaonekana ww unajazba sana punguza jazba alaf inaonekana ww ni ngwin uliyesomea certificate ya politics /journalism/ hoteli management Ilala pale. Huwezi kujifananisha na Daktari wa Muhimbili ata kidogo mkuu. Changia hoja ww acha kashfa, hao madaktari unaowaita wa UPE ndio wanaowatibu dada, kaka, wajomba, shangazi, bibi, babu, mama na baba yako magonjwa ya kuharisha ambayo yamekithiri kwenye familia yenu. Maana uliotoa hapo ni uharo mtupu.
 
Huyo bundi yuko wapi ndege wa Mungu masikini, mbona mie smuoni?
Mie mniambie tu maandamano wapi!!!
 
Huyu mkuu amejiunga JF 10/6/11 yaani siku 19 tu zilizopita, anapost 184 na amejishukuru mara 40 kwenye post 23!!Lakini kitu gani hasa kinamfanya huyu mkuu aweweseke namna hii? raia wa nchi hii wamefaidikaje na miaka 50 ya ccm madarakani?1. Umeme kwenye hii dunia ya karne ya 21 ya sayansi na technologia, vijiji vingapi vya nchi yetu vina umeme?2. Afya ni aibu kubwa hadi leo baadhi ya wake zetu kudhulika kwenye uzazi, matitizo kama ya Fistula (VVF) yalishasahauliwa kabisa kwenye nchi zilizoendelea na zinazoendelea, actually ni mojawapo ya vipimo ya nchi fukara isiyoweza kuwapatia wananchi wake huduma za afya. Hapo hujaongezea na kipindupindu, surua, malaria, TB, utapia mlo nk magonjwa ya umasikini ambayo yanaendelea kushamiri tanzania miaka 50 ya kujitawala, Hospitali mbovu, chafu, zisizo na vifaa vya kisasa? madaktari uchwara kitaaluma (daktari aliyesoma Muhimbili ni daktari UPE, yaani ni kama wale walimu wa UPE wakati wa mwalimu)3. Elimu tujilinganishe na majirani zetu Kenya na Uganda. Sisi tuna elimu mdundiko4. Usafiri reli?, ndege?, barabara za lami? viwanja vya ndege? meli? usafiri wa mijini? ustaarabu wa kupanda vyombo haba vya usafiri yaani watu wazima kupigana vikombo wakati wa kuingia kwenye madaradara au mabasi? utumiaji wa magari mitumba na uchafuzi wa hewa mijini (air pollution)? wachache wanaweza kununua magari mapya? Mkuu naomba uwambie ccm waache mara moja kukiita kiwanja cha ndege mwanza International Airport, pamoja na kwamba watanzania ni mazezeta lakini uzezeta mwingine kama huu wa kukiita hiki kiwanja cha mwanza international airport unavuka mipaka.6. MajiHaa haaa haaa haaaa! pamoja na kuwepo mito, maziwa, bahari na mvua zinazo sababisha mafuriko, nchi haiwezi kutoa huduma ya maji bora hata kwenye makao makuu yake? Haa Haaa Haaaaaa Haa aha!!!!!!!! achilia mbali vijijini. rafiki yangu kijijini kwao ni pembeni mwa ziwa victoria, mwezi uliopita alitumia millioni 2 kuchimba kisima nyumbani kwao???? sasa anatafua solar ya umeme na pump ya maji, jamani ile kitu inayoitwa serkali iko wapi?5. Makazi ya watu unplanned, mitaa ya vumbi na matope isiyo na taa? Hakuna sewage system, kila mwenye kujenga nyumba anajenga septic tanks na kuishi na mavi yake mwenyewe uani kwake6. wafanyakazi wa serkaliniwavivu? wana elimu duni, hawajui wanachofanya? hawalipwi mishahara inayokidhi mahitaji yao ya kimaisha? kila mfanyakazi wa serkali ni potential thief? 7. viongozi wa ngazi za juu serkalini (raisi, mawaziri, makatibu wakuu nk)elimu duni (elimu ya tanzania), uwezo mdogo, hawajui walitendalo8. Maisha ya mwananchi wa kawaida kijijiniNi jehanamu, hakuna anayejali, ujanja ni kukimbilia mijini na kuwa machinga wenyewe wanasema "tutabanana humu humu"?Mkuu sababu gani hasa inakufanya uwachukie wale ambao wanajaribu kubadilisha hii hali angalau iwe nafuu kwa watu? Future ya nchi hii ipo namna hii:1. As long as ccm wako madarakani hali na maisha ya watanzania yatabakia ama kama yalivyo au kudidimia zaidi2. vyama vingine vikipata nafasi ya kuunda serkali vinaweza kurekebisha kasoro za ccm na kuinua maisha ya watu au vinaweza kuwa worse than ccm.Sasa hapa ndipo panapo hitaji maarifa yaani uogope kuchukua hatua na uendelee kudumaa na kudumaa zaidi au uchukue hatua ambayo inaweza kukuinua au kukuangamiza kabisa. The future belongs to the brave and those who dare to take risk. Hata kwenye biblia bwana Yesu alitoa mfano ya taranta, yule mtumishi aliyepewa taranta moja akaogopa kuitumia na kuishia kuifukia ili mkuu wake atakaporudi amkabidhi talanta ileile alilaaniwa kwa kufanya hivyo siku mkuu wake aliporudi, alinyanganywa taranta na akapewa yule ambaye alichukua risk ya kuzifanyia biashara talanta za mkuu na kutengeneza faida.
Umenena mkuu nakubaliana nawe kwa asilimia mia moja hasa kwenye makazi umenikuna yaani nimerialize kumbe naishi na mavi yangu hapa nyumbani!!! Duh haya si maendeleo wenzetu wana sewage na wanarecycle maji taka yanarudi kwa matumizi sisi tunaishi nayo wenyewe!! Kwa kuongezea na Bunge pia lililojaa mipasho kama bendi mbili za taarab enzi zile tot na muungano wabunge hasa wa CCM kusimama na kuikosoa serikali hasa bajeti hadi ukisikiliza ukadhani watakwamisha bajeti isipite na kwa mshangao wa ajabu kama kumuona mbuzi anataga mayai mbunge huyo huyo aliyetumia muda wake kuiponda bajeti anamalizia hotuba yake kwa kusema `mheshimiwa supika baada ya kusema hayo naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja' hapa unaweza kujiuliza sasa huyu alisimama kufanya nini kuuza sura!!!!! Mi nikiona mbunge wa ccm anaongea kwakweli huwa nabadili kuangalia chaneli nyingine isiyorusha bunge
 
Title ya thread yako ni nzito ukilinganisha na content. Ki msingi umeilaumu Chadema kutokana na matendo ya Shibuda. Hapo umekosea sana, umekurupuka. Tafakari yafuatayo
1. Chadema ni taasisi iliyokaa kimfumo. Ukileta upuuzi kwenye taasisi iliyokaa kimfumo mfumo utaku-phase out automatically
2. Kama chama kilichojijenga ambacho msingi wake ni watu watu kama Shibuda hukijenga chama na hakika hakitasambaratika
3. Dhamira, malengo na nia binafsi walizonazo viongozi na wanachama wa chadema haviwezi kukiteteresha chama
4. Kadiri CCM wanavyo perform poorly na chadema kubainisha mapungufu hayo kisayansi ndivyo credibility ya chadema inavyopaa
5. Ipo project inayofadhiliwa kwa nguvu zote na CCM ya kuhakikisha Chadema inakufa lakini kutokana na sababu ya 1 hapo juu yote hayo yamebainika na chama linasogea.
Yapo mapungufu katika kuipresent hoja ya posho na nadhani chadema hawakujipanga kama chama toka mwanzo na kwenye hilo wameteleza kidogo lakini huwezi ku conclude eti bundi amepewa kigoda(amekaribishwa) chamani.
Tulitoa tahadhari kwenye mchakato wa uchaguzi uliopita kuhusu akina Shibuda-type kuingia Chadema na kupewa uongozi mara moja. Lilikuwa kosa. Hawa hawakuja Chadema kwa sababu ya mapenzi ya chama bali kwa sababu walitemwa huko CCM. Wakipata mwanya watarudi tena kwa mbwembwe za 'nimerudi nyumbani'. Watarudi wakiwa na siri nyingi za chama. Hili ni fundisho kwa siku zijazo. Mamluki ni hatari.
 
Mimi nadhani mkuu amenena mema tena kwa weledi mkubwa sana tatizo lililopo humu jf ni kuwa watu hawataki kusikia habari za tahadhari kuhusu chadema huu ni upumbavu mkubwa sana aliwahi kunena Mh Benjamin Mkapa kuwa 'mtu kama hataki kuumiza mbongo yake basi ni bora angepewa uti wa mgongo kuliko ubongo.

Tatizo CHADEMA halipo kwa Shibuda tatizo lipo mbali zaidi kwa mfano Zitto Zuberi Kabwe ameshasema ya kuwa yeye ndie atakuwa mgombea Urais 2015 kupitia CHADEMA siyo mbaya but hebu fikiria ikitokea akapigwa chini kama ilivyotokea wakati alipotaka kugombea uenyekiti itakuwaje?

Ikumbukwe kuwa watanzania kwa mara ya kwanza walionyesha hamasa kubwa sana kwa Dr Slaa so kama ikipendekezwa Slaa agombee tena Zitto atafanyaje?

Coz kiukweli zitto anawafuasi wengi na mpaka sasa haeleweki vizuri ijapokuwa wajinga wamesha amini kuwa ni kiongozi bora.Lakini pia hapa arusha napo si shwari hata kidogo.

Nionavyo mimi kuwa chadema inatakiwa ijitazame upya, hawa wabunge maarufu wenye itikadi zisizo eleweka watakuja kiharibu chama chetu.
 
Mzee inaonekana ww unajazba sana punguza jazba alaf inaonekana ww ni ngwin uliyesomea certificate ya politics /journalism/ hoteli management Ilala pale. Huwezi kujifananisha na Daktari wa Muhimbili ata kidogo mkuu. Changia hoja ww acha kashfa, hao madaktari unaowaita wa UPE ndio wanaowatibu dada, kaka, wajomba, shangazi, bibi, babu, mama na baba yako magonjwa ya kuharisha ambayo yamekithiri kwenye familia yenu. Maana uliotoa hapo ni uharo mtupu.

Kwa nini nijilinganishe na madaktari wa Muhimbili? ili iweje? Sawa mimi pamoja na watanzania wengi bado tuna ugua magonjwa ya umasikini kama ya kuhara kwa sababu hakuna huduma za afya wala mikakati ya serkali kuendeleza wananchi wake. Baba yangu alifariki mikononi mwa hao madaktari wako wa muhimbili na sidhani kama ni mimi tu ambaye nimeathirika na uvundo wa muhimbili na madaktari wake. Siku watanzania tutakapo jua haki zetu na kupata serkali makini, tutaanza kuwafungulia kesi hao madaktari kwa kusababisha vifo ambavyo vingeweza kuzuilika kwa familia zetu.
Huna sababu ya kubisha fanya utafiti juu ya ubora wa huduma za afya Tanzania unaweza kupata habari hata kwenye google juu ya training na ubora wa madaktari wa Tanzania, uwiano wa madaktari na population ya tanzania, infant mortality rate, maternal mortality rate nk nk halafu linganisha na nchi zingine.

Nakushauri pia uache kukashifu fani za watu wengine, journalism, hotel management nk. Kuwa daktari hakukufanyi wewe uwe tofauti na hotel manager, sana sana kimapato hotel manager anaweza kumshinda daktari...... lol!!
 
Umenena mkuu nakubaliana nawe kwa asilimia mia moja hasa kwenye makazi umenikuna yaani nimerialize kumbe naishi na mavi yangu hapa nyumbani!!! Duh haya si maendeleo wenzetu wana sewage na wanarecycle maji taka yanarudi kwa matumizi sisi tunaishi nayo wenyewe!! Kwa kuongezea na Bunge pia lililojaa mipasho kama bendi mbili za taarab enzi zile tot na muungano wabunge hasa wa CCM kusimama na kuikosoa serikali hasa bajeti hadi ukisikiliza ukadhani watakwamisha bajeti isipite na kwa mshangao wa ajabu kama kumuona mbuzi anataga mayai mbunge huyo huyo aliyetumia muda wake kuiponda bajeti anamalizia hotuba yake kwa kusema `mheshimiwa supika baada ya kusema hayo naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja' hapa unaweza kujiuliza sasa huyu alisimama kufanya nini kuuza sura!!!!! Mi nikiona mbunge wa ccm anaongea kwakweli huwa nabadili kuangalia chaneli nyingine isiyorusha bunge

Mheshimiwa unajua jambo usilolijua ni kama usiku wa giza, kuna mambo mengi tu sisi watanzania hatuyajui na watawala wetu wanatumia ujinga wetu kama mtaji wao. Safari bado ni ndefu, God willing ipo siku watanzania finally tutafika.
 
Chadema mpka sasa unaona wamekufanyia nini? Angalia sehemu zote cdm wanazoongoza maendeleo yalivyo duni! mifano halisi unayo, angalia Karatu na Kigoma kulivyo na maendeleo duni!

Nilidhani binadamu wote vichwa vyao vinafanya kazi ..... kumbe wapi!.
Wengine vimejaa maji tupu!
 
Kama lengo la kuweka title ya hivyo ili watu wafungue waisome basi na wewe umeteleza. Ume-water down fikra zangu juu yako kuhusu dhamira yako kwa chadema. Title yako imekaa kiudaku udaku.Nikukumbushe tu kuwa wewe sio wa kwanza kutaka kuuaminisha uma kuhusu huyo Bundi. Yaliandikwa, yakaandikwa lakini hadi sasa bundi hasikiki. Lakini hilo halimanishi kuwa chadema hakukuwa na migogoro au kupishana ki mtazamo. Hi huo utaasisi ambao unaupuuza sasa uliofanikisha chadema kuvuka vigingi vizito na vikali. Ni mwehu pekee anayeweza kuignore mfumo wa kiutawala na wa kitasisi wa chadema. Nikuhakikishie, chadema inamfumo mkali wa kiintelijensia ambapo threat yoyote kwa chama huwa detected haraka na hushughulikiwa accordingly. Mifano ipo na wengine wanafahamika.Lakini njia na taratibu zinazotumiwa na chdm kutatua migogoro ya ndani ni thabiti.Pamoja na hayo yote bado chadema inagroom vijana kitaasisi kuja kuwa viongozi madhubuti wa chama na taifa baadae.Hiyo ndio taasisi, na taasisi ya namna hiyo haifi! Mtaendelea kutoa dua la kuku kila siku. Hakuna bundi chadma


MK sina la kuongeza umenisemea vyema sana .Na wakumbuke Chadema wako Duniani so haya yanatokea kwa kila aliieyko Duniani .CCM wao walidhani na bado wanadhani Dunia tofaui ndiyo maana wanaishia kukataa n kupanga mbinu chafu na hawakubali hali halisi ya karne ya 21.Thanks Mzito Kabwela
 
Kwa nini nijilinganishe na madaktari wa Muhimbili? ili iweje? Sawa mimi pamoja na watanzania wengi bado tuna ugua magonjwa ya umasikini kama ya kuhara kwa sababu hakuna huduma za afya wala mikakati ya serkali kuendeleza wananchi wake. Baba yangu alifariki mikononi mwa hao madaktari wako wa muhimbili na sidhani kama ni mimi tu ambaye nimeathirika na uvundo wa muhimbili na madaktari wake. Siku watanzania tutakapo jua haki zetu na kupata serkali makini, tutaanza kuwafungulia kesi hao madaktari kwa kusababisha vifo ambavyo vingeweza kuzuilika kwa familia zetu.
Huna sababu ya kubisha fanya utafiti juu ya ubora wa huduma za afya Tanzania unaweza kupata habari hata kwenye google juu ya training na ubora wa madaktari wa Tanzania, uwiano wa madaktari na population ya tanzania, infant mortality rate, maternal mortality rate nk nk halafu linganisha na nchi zingine.

Nakushauri pia uache kukashifu fani za watu wengine, journalism, hotel management nk. Kuwa daktari hakukufanyi wewe uwe tofauti na hotel manager, sana sana kimapato hotel manager anaweza kumshinda daktari...... lol!!

Muhimbili hakuna wataalam bwana kuna waganga tu .Mimi nina ushahidi wa yaliyo nikuta a very senior Dr na wa kuaminika Tanzania nzia hakujua ninaumwa nini .Yeye alikazana na matokeo ya MRI scanning , akasema nipelekwee Moi nipasuliwe uti wa mgongo .Nikamuuliza unataka kupasua ili iweje ? Yes disc zimesagik lakini nini chanzo ? Naumwa nini ? Hakujua hata leo.Wote mnajua hapa miliniombea sana muda huo .Kwenda ulaya wana angalia damu na dktari wa kike anasema naumwa kitu fulani na hakuna operation wala nini leo natembea nimetoka Tanzania niko kwenye wheelchair .Thanks Paka Jimmy alinisaidia hata kuingia kwenye ndege nikiwa hoi ila naukumbuka utu wake .

Leo nieongea na mtaalam mmoja amekiri kwamba pamoja na yeye kuwa doc lakini Muhimbili wanawapa watu wengi ushauri wa kijinga nakuwapeleka India wakiwa na ugonjwa tofauti na muhimbili waio usema .So nasema muhimbili bora liende kwa kweli .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom