Bunda: Mwili wa Samson Josiah, mmiliki wa mabasi ya Super Sami waokotwa mto Ndabaga kwenye Kiroba

Maskini,naimagine jinsi alivyoteseka kuchinjwa bila nganzi,Binadamu ni zaidi ya mnyama.Babu yangu aliniambia zamani ukiona Binadamu unapata moyo,siku hizi ni bora ukutane na Simba kuliko Binadamu mwenzako.
Ccta mie naogopa sana lifestyle iliyopo sasa Tanzania. Hebu angalia ujasiri walionao hao wauaji!! Najiuliza je inamaana tangu wazaliwe hawajawahia kufundishwa uwepo wa mungu!? Nimechoka kabisa heri kufa kwa Ukimwi lkn si kwa style hii. Nchi imelaaniwa
 
Labda anataka aunganishe doti,mauaji ya Diwani wa CDM Kule Moro, Mwenyekiti wa NCCR MAGEUZI kule Kasulu na hili LA huyu tajiri ili ahitimishe kuwa mauaji ya sasa yamewalenga wapinzani.
Tungoje atakuja kuyajibu maswali yako yeye mwenyewe.
Sio kila kitu mnakiweka kwenye siasa wafanyabiashara yaweza kuwa alikua na mkwaruzano na matajiri wenzake ,,,msiingize siasa kila tukio
 
Kuna mambo pia tunafanya nyuma na kusahau kabisa,, tunaacha vidonda mioyoni kwa watu ,, hujui mtu anawaza nn mwishoe ndio huwa hivyo,,,, unaweza kuta ni kisas hata cha miaka 15 iliyoisha ,,

Hatuwez jua pia,,
Kisasi gani,mambo yko wazi tusimeze maneno wasiojulikana wanafanya mambo kwa baraka za mkuu,huo mto kwa upande wa serengeti unamamba wengi sana ukipita utafikiria mijusi imejianika juani.
Wamechoma gari serengeti halafu wakaja kumtupia upande wa mto kilawira ambapo hakuna mamba angeuawa serengeti maiti isingefika hpo ilipookotwa mamba wangeshafanya yao
 
Hapo ndipo tunaona mambo ya ukweli yalivyo, kapotea mtu, mke, watoto, jamaa na marafiki wametoa taarifa marehemu kapatikana...
Sasa haya ya mitandaoni kwamba maiti zaokotwa baharini halafu ndugu kutokulalamika haingii akilini kabisa..
Mkuu kama hilo furushi lingekwama mahali huko mtoni ni dhahiri marehemu asingejulikana alipo. Nina mashaka hilo furushi ilidhamiriwa lionekane.
 
Mwili wa mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah unaodaiwa kukutwa mtoni ukiwa umefungwa kwenye mfuko.



Mwili wa Mmiliki wa mabasi ya Super Sami Samson Josiah umekutwa katika mto Ndabaka eneo la Bunda /Lamadi

Taarifa kutoka vyanzo vya habari zinasema kwamba mwili wa Samson Josiah umeokotwa na wavuvi wa samaki leo jioni Jumatano Machi 14,2018.

Watu wa karibu na marehemu wanasema mwili uliookotwa ni wa Samson Josiah.

Miongoni mwa habari zilizoteka vyombo vya habari Tanzania tangu Machi 9, 2018 hadi ni kuhusu kupotea kwa mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah kwa zaidi ya wiki mbili sasa. Soma => TANZIA: Mmiliki wa mabasi ya Super Sami akutwa amekufa na gari lake kuchomwa moto Serengeti

Mapema ilielezwa kuwa gari yake ndogo aliyokuwa akiitumia aina ya Toyota LandCruiser ilikutwa imechomwa moto katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti iliyoko mkoani Mara siku ya Machi 9, lakini yeye mwenyewe alikuwa hajapatikana.

Kwa mujibu wa familia ya Bwana Josiah, ambayo inaishi mkoani Mwanza, ilidai kuwa siku ya kupotea kwa Josiah ambayo ni February 27, majira ya usiku, Josiah alimpigia simu mkewe na kumwambia kuwa atarudi nyumbani na mgeni, na hayo yakawa mawasiliano yao ya mwisho.

Mabasi ya Super Sami yanafanya safari zake kuanzia mkoa wa Mwanza, kwenda mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Iringa pamoja na Kagera.

Chanzo: Muafrika Halisi blog
Mgeni... sawa labda mgeni muuaji.
 
Huyu alikuwa chama gani kwani? Wanaomfahamu watueleze alikuwa anataka ubunge au nafasi ya kisiasa? Na je anahistoria gani nyuma ya utajiri wake?
hajawahi kujihusisha Na siasa, pombe hanywi. Ila hakuwa mnoko kuwakopesha fedha wahitaji.
 
Duuuh...! Na walofanya hio kitu wakifika kwa WANENE wao wanasema deal done!! Aiseeee Tanzania haiko Salama
 
Jamani acheni siasa kwenye mambo kama haya. Ni vizuri vyombo vya ulinzi na usalama vikafanya kazi yake. Tukiendelea kuilaumu serikali/watawala mwisho wetu hautakuwa salama. Tutaanza kuuana kwa ajili ya ugomvi wa mashamba, ardhi, mirathi, mapenzi, dhuluma, nk, huku tukijua kwamba tutaibebesha mzigo serikali kwamba ndiyo imehusika. Tukifika huko, ni hatari sana kwa mustakabli wa taifa letu.
 
Fanya busara kidogo kwa kuigiza kama nawewe ni mtu timamu.

Unaharibu upepelezi kwa kuingiza siasa. Au wewe ndio muhusika hapa unafanya hivi kuwapotosha wapelelezi?

Inahitaji upelelzi gani hapo mkuu?
Style yao ya mauaji ni ileile , namini huko kanda ya ziwa kutakuwa n amauaji mengi sana yakiendelea kimyakimya.
 
Kuna watu walipatikana katika mtindo huo huo tukaambiwa ni wahamiaji haramu!
sasa huyu ana jina tusubiri kuambiwa kama kajiua iki kuketa taharuki au wauaji wa ndanu wamekopi mtindo wa disposal wa wale wanaowatelekeza wahamiaji haramu waluokufa ili kuketa taharuki,ama wasiojulikana kwa ujumla wake wanaendeleza wimbi la mauaji?
Na sijui katika pelelezi zao wamepata kugundua kama kesi zote zinawatendaji wa aina moja au ni isolated na hapo tuanze mbali ,mauaji ya Mawazo yule wa morogoro ,mvungi nk na kwenye utekaji
Kibanda ,roma,nondo ,masheikh nk.
Na waliopotea kote iangaliwe kama wahusika wanahusiana.
kaka mbona unabagua umesahau polisi wetu kibiti na raia wa eneo hilo?
 
Kisasi gani,mambo yko wazi tusimeze maneno wasiojulikana wanafanya mambo kwa baraka za mkuu,huo mto kwa upande wa serengeti unamamba wengi sana ukipita utafikiria mijusi imejianika juani.
Wamechoma gari serengeti halafu wakaja kumtupia upande wa mto kilawira ambapo hakuna mamba angeuawa serengeti maiti isingefika hpo ilipookotwa mamba wangeshafanya yao
Sijameza maneno,, nimewaza upande wa pili ,, siku zote dhambi yoyote ifanyikao ni vuno la shetan" na analaumiwa sawa ila kumbuka kuna mengine shetan hukana na kusema sijamtuma ni akil zake tu,,,

Kuna kikundi cha watu wanachukulia faida ya kufanya yao kwa hali hii iliyopo sasa mpka inamfrustrate mkuu wetu wa nchi
 
Hiviii wale wanaotoaga uhai wa binadamu wenzao ikitokeaga nao wakafaa huwaa wanakutana na wale waliowakatisha uhai wao? Huwa wanajiskiajee aibu huruma au?

Usalama wetuu umezid kuwa salamaa na shwarii kabisaa aman mpaka imejaaa pomon
 
Back
Top Bottom