WAKATI Tanzania inajipanga upya kufufua Shirika lake la Ndege (ATCL), Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Kenya (KQ), Titus Naikuni, amesema kama Tanzania inataka shirika hilo liendelee, Serikali yake inapaswa kujitoa katika uendeshaji.
Akijibu jana maswali ya wandishi wa habari kutoka nchi nne wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, baada ya kuwasilisha ripoti ya utendaji wa KQ inayoishia Machi 2010, Naikuni alisema utafiti umeonesha kila mahali barani Afrika serikali ilipoingilia uendeshaji wa shirika la ndege, lilipata matatizo.
Alifafanua kwamba, serikali inaweza kuwekeza mtaji, lakini akasisitiza kuwa hata kama ikiwekeza mtaji, lazima iache wataalamu waendeshe bila kuingiliwa na sekta binafsi itakuja yenyewe.
Serikali ya Kenya inamiliki asilimia 23 tu ya hisa katika KQ ambayo inajipanga kuongeza safari zake katika miji zaidi ya Afrika, huku shirika la ndege la kimataifa la KLM likimiliki asilimia 26 na sehemu iliyobakia ya hisa ikimilikiwa na kampuni na watu mbalimbali duniani.
Wiki mbili zilizopita, serikali ilishauriwa kuivunja ATCL na kuanza upya kama ilivyofanyika katika Shirika la Bima la Taifa (NIC), kwa madai kuwa shirika hilo limekuwa likichukua fedha za Serikali kuliko kutoa matumaini ya kukua.
Wakati KQ inayomiliki ndege 28 kwa sasa, ikijipanga kuagiza ndege nyingine tisa ambazo ni kubwa aina ya Boing 787 na isipozipata, imeshaanza kutafuta mbadala wa kufikia lengo hilo kwa kupata ndege aina ya Airbus 330 ifikapo mwaka 2013, ili pamoja na mambo mengine, liwe shirika kubwa la ndege barani Afrika. ATCL ina ndege moja ambayo inasuasua.
Naikuni alipoulizwa iwapo KQ, ambayo imepata faida baada ya kodi licha ya soko la huduma za ndege kuathiriwa na mtikisiko wa uchumi duniani, itakuwa tayari kushirikiana na Tanzania kuifufua ATCL, alishauri ushirikiano huo uanze kwanza kati ya kampuni ya Precision kabla ya KQ.
"Sisi tuko tayari kwa ushirikiano na shirika lolote, lakini kwa nini mnawaza kushirikiana na KQ badala ya kushirikiana na Precision ambayo iko nyumbani?," alihoji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Precision, Alfonse Kioko ambayo asilimia 49 ya hisa za shirika analoliongoza zinamilikiwa na KQ, alisema wako tayari kwa mazungumzo ya kuifufua ATCL.
Hata hivyo, alitaka Watanzania waione Precision kama shirika la pili la kitaifa baada ya ATCL, kwa kuwa linamilikiwa kwa sehemu kubwa na Watanzania na limeajiri Watanzania wengi zaidi ya wageni.
Chanzo: Gazeti Habari Leo.
My take:
Katika sakata hili hapa naona wale wenye nia yao ya kuua kabisa ATCL ndo naona wanajipanga taratibu. Binafsi sikubaliani na ushauri wa huyo boss wa KQ kwamba ATCL ishirikiane na Precision air kwani hawa hawa KQ wanamiliki 49% ya precision air na kama wajinga wetu wa CCM wakiingia mkenge huu basi bora tusiwe na shirika la ndege kabisa.
Mbona kabla ya Mkapa na basil mramba shirika lilikuwa tishio ktk ukanda huu? ATC ya wakati ule ilikuwa mpaka inaruka kwenda New Delhi, SA n.k. kwa nini leo iwe hivyo? Tunajua Basil mramba na wenzake wana hisa precision air. Mimi nashauri kama ni kuvunja wavunje lakini lianzishwe shirika jipya na wafanyakazi wapya na wabia wapya na siyo kuungana na watu walioshiriki kuua ATCL.