Bosi wa TCAA Hamza Johari Kuongoza Shirikisho la Kimataifa la Huduma za Anga

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
DSC_0714.JPG

Nimeipata muda si mrefu, kwamba Bosi wa Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari, leo hii jijini Madrid, Hispania, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Kimataifa la Huduma za Anga na Uongozaji Ndege (CANSO) Kanda ya Afrika.

Naamini hii ni heshima kubwa kwa Taifa katika sekta hiyo ya anga.

Taarifa kamili ni hii hapa:

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza S. Johari amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Shirikisho la Kimataifa la Huduma za Anga na Uongozaji Ndege (CANSO)akichukua wadhifa huo kutoka kwa Thabani Mthiyane wa Afrika Kusini aliyehudumu katika nafasi hiyo kwa miaka sita.

Bwana Johari ambaye atakuwa kwenye wadhifa huo kwa miaka mitatu, amechanguliwa tarehe 5 Machi 2018 katika mkutano wa CANSO unaofanyika Madrid Hispania na anatarajiwa kuthibitishwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama wa CANSO uliopangwa kufanyika mwezi Juni Bangkok, Thailand.

Kutokana na uteuzi huo, Bwana Johari anakuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya CANSO (EXCOM) ambacho ndicho chombo cha juu cha usimamizi wa shughuli za shirikisho hilo.

Bwana Mthiyane anatarajiwa kukabidhi majukumu ya mwenyekiti wa CANSO Afrika kwa Johari baina ya mwezi Machi na Juni 2018.

Tunapenda kumpongeza Mkurugenzi Mkuu wa TCAA na kumtakia mafanikio katika majukumu haya mapya CANSO ni Shirikisho la Kimataifa la Huduma za Anga na Uongozaji Ndege za Kiraia Duniani.

Wanachama wa CANSO wanatoa huduma hizo kwa asilimia 85 kote duniani.

Wanachama wa shirikisho wanabadilishana taarifa na kuandaa sera zinazolenga kuboresha huduma za anga na uongozaji ndege.
 
Hongera yake. Kumbe hawakukosea kumchagua. Ataleta mabadiliko katika sekta ya anga barani Afrika.
 
Huyu jamaa ndo aliandika habari za kuhusu ziwa nyasa na ndo alikuwa akiongoza jopo la wataalam kutoka Tanzania waliokuwa wakishughulikia mgogolo wa ziwa nyasa kati ya tanzania na malawi
 
Back
Top Bottom