Mpwechekule
JF-Expert Member
- Jul 8, 2012
- 221
- 55
Katika hali isiyotarajiwa mtoto mdogo umri 10 aliona mfuko wa plastik kwenye uzio wa michongoma, na kuuchunguza akakuta ni bomu na kutoa taarifa kwa majirani ambao walitoa taarifa polisi, polisi walifika na kubaini ni bomu, na kuwaarifu jwtz ambao walikuja kuliondoa, siku hiyo hiyo ya jumamosi th 3 . 11 .2012, ni siku ya jumuia, na jumuia ilifanyika hapo baada ya kumalizika jumuia ndipo bomu likaonekana, WASIWASI wangu ni kutopewa kipaumbele habari hii na vyombo vya usalama na habari, kwani ninavyo mimi kukutwa bomu mtaani ni hatari, ukizingatia halikutengenezwa kienyeji, pia hali ya usalama wa ndani ya nchi yetu si nzuri, hawa viongozi wetu wanasubiri maafa ndio wachukue hatua?.