Bomoa bomoa yavaa fukwe za Mbezi Beach; Kuacha kilio kwa matajiri wavunja sheria!

Ni nani alikwambia kwamba Ikulu ilikuwa kando ya Mji? Na katikati ya Mji palikuwa wapi sasa kama Ikulu ilikuwa kando ya Mji?

Mkuu,

Elimu uliyoitoa inatosha na wengi wetu tumeielewa. Huyo mnywa viroba Laki si Pesa humu JF ma-GT wote tumempuuza na hatujibu posts au comments zake. Nakusii uungane nasi katika maazimio hayo. Maana ni wazo hoja yako ameielewa ila tu ameamua kupinga.
 
Ikulu ya magogoni nayo iko Beach bomoa bomoa ipite hapo..
Nasoma post zako mara kwa mara, Nakushauri kubali Magufuli ndipo rais wako uishi kwa amani.

Maana chuki zako kwa Magufuli ziko wazi Wazi kuliko wana JF wengi ninaowasoma humu!
 
Mkuu,

Elimu uliyoitoa inatosha na wengi wetu tumeielewa. Huyo mnywa viroba Laki si Pesa humu JF ma-GT wote tumempuuza na hatujibu posts au comments zake. Nakusii uungane nasi katika maazimio hayo. Maana ni wazo hoja yako ameielewa ila tu ameamua kupinga.

Dada Hamida we punguani wahed toka lini ukawa GT wa jf? labda Great Sinker! teh teh
 
Nasoma post zako mara kwa mara, Nakushauri kubali Magufuli ndipo rais wako uishi kwa amani.

Maana chuki zako kwa Magufuli ziko wazi Wazi kuliko wana JF wengi ninaowasoma humu!

Sijawahi kumchukia Magufuli hata siku moja. namheshimu sana na ni sawa na baba yangu mzazi ki umri nimchukie kwa lipi labda?
 
wanabomolea wanyonge tu, tuona kama watayaguza majengo haya..........jangwani sea breeze, white sands hotel, Beachcomber, Golden Tulip, Sea Cliff hotel...!!!?????..
 
Hapa lazima Mama Rwakatare ahikishwe adabu, yule Mama ana kiburi sana, ndugu zetu wamebomolewa nyumba na huyu Mama na alikataa kuwalipa kisha yeye akavunja sharia kwenda kufukia sehemu ya fukwe (mangroves) ili ajenge nyumba yake kihuni. Magufuli kamata mwizi man, na onyesha kauli mbiu yako ya #HapaKaziTu inafanya kazi kweli.
 
Chonde chonde serikali yetu sikivu,mabaa na madanguro katika makazi ya watu yanatuharibia maadili ya watoto wetu na kuleta usumbufu wa kelele katika makazi.
 
WanaJF,

Naanza kwa kauli mbiu ya Hapa Kazi tu. Kwa maana kazi ndio hiyo imeanza.

Tangazo limetolewa rasmi kwa wamiliki wote wa maghorofa ya makazi na mahoteli yote yaliyo katika fukwe ya Mbezi Beach ambayo wamiliki wake wamekiuka sheria kwa kujenga majengo hayo ya ghorofa ndani ya eneo la mita 60 kutoka kwenye fukwe za bahari.

Ikumbukwe kuwa kwa sasa hapa Dar zoezi la bomoa bomoa linaendelea na hadi sasa limepita kwenye maeneo matatu ambayo ni: Kurasini, Mwenge na Boko. Hivyo zoezi hili limeamriwa kwenda sambamba na kubomoa nyumba na mahoteli yaliyo katika fukwe za bahari ambayo wamiliki wake wamevunja sheria ya mipango miji na ile ya matumizi ya ardhi.

Matajiri waliojenga fukweni mwa bahari wameagizwa kubomoa wenyewe maghorofa hayo yaliyo ndani ya umbali wa mita 60 kutoka kwenye ufukwe la sivyo watalazimika kulipia gharama zote ambazo serikali itatumia katika kutekeleza agizo hilo la kuvunja maghorofa hayo.

My take,

Wale wa Home Shopping Centre ni wajanja sana. Walijua katika huu utawala wa awamu wa tano hakuna zile 10% walizozoea kutoa hivyo wakaamua kukunja jamvi na kukimbia. Sasa kiama kuwashukia wale matajiri waliobaki. Msumeno huu hauna huruma kwa wavunja sheria wote nchini.

Mbona wameanzia mbali wakati sinza open spaces 90% zinahodhiwa na ccm kwa mabavu
 

Hata sheria za nchi hauzi
jui masikini ya Mungu, ngoja basi nikufafanulie kwa faida ya wengine pia, kisheria ufukwe wote unapaswa kuwa wazi kwa ajili ya matumizi wa WatanZania wote kama ilivyo coco beach au gymkhana una unaruhusiwa tu kujenga Mita 60 kutoa ufukweni na mara nyingi huwa ni upande wa pili wa barabara kama vile ukipita coco beach utaona br imetenganisha ufukwe na makazi ya watu sasa kwa maelezo haya labda utaweza kujijibu kama Ikulu yetu inapaswa kuvunjwa au vipi!

Ufukwe wa bahari mpaka wake ni pale linapoishia bamvua kubwa (high water tide mark). Hivyo kuanzia hapo pima sasa hizo mita 60 kuja nje.
 
wanabomolea wanyonge tu, tuona kama watayaguza majengo haya..........jangwani sea breeze, white sands hotel, Beachcomber, Golden Tulip, Sea Cliff hotel...!!!?????..
Swala si kubomolewa tuu bali wamefata au hawajafata sheria? Si kila nyumba au hotel iliyo kwa ufukwe itabomolewa...
 
waanze na dable tree pamoja na sleepway na haya maoteli huku mbezi beach bila kusahau seacliff hotel hapo nitamuunga mkono
 
Uzauza lingine la ccm ni huyu mtu!!!! Yy akiulizwa kitu jibu lake ni lowassa!! Hahaaa mita 100 Na yupo seriaz kabisa,mwenyew anaziona na nyingiiiiiii!!! Pole may be ni pure ignorance!!!

No need to panic itafahamika tu mwisho wa siku!
 
Acha ubishi mita mia ni sawa na urefu wa kiwanja cha mpira.ikulu ipo ndani ya izo mita mia hata 60 bdo ipo
 
Back
Top Bottom