Bitegeko ni vigogo gani Bodi ya Kahawa Polisi wamewakamata Moshi?

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Polisi Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania linawashikilia watu wanne waliokuwa viongozi wa Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) kwa tuhuma za wizi wa fedha kiasi zaidi ya Sh.2 bilioni.

Akizungumzia kukamatwa kwa watuhumiwa hao leo Jumatatu Novemba 25, 2019, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni amesema vigogo hao walikamatwa juzi Jumamosi Novemba 23, 2019.

"Ni kweli Jeshi la Polisi Kilimanjaro linawashikilia watuhumiwa wanne kwa tuhuma za wizi wa fedha kiasi cha Usd 908,065.65 mali ya Tanzania Coffee Board (TCB)," amesema Hamduni
Aidha amesema fedha hizo zinadaiwa kuibiwa kwa nyakati tofauti katika msimu wa mauzo ya Kahawa mwaka 2016/2017 na 2017/18.

Hamduni amesema upelelezi wa kukamatwa kwa vigogo hao unaendelea na kwamba utakapokamilika jalada litawasilishwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na taratibu za kuandaa hati ya mashtaka ili watuhumiwa wafikishwe mahakamani.

Kamanda Hamduni ametaja majina yao kuwa ni Astery Bitegeko, aliyekuwa mkurugenzi wa Fedha, Goodluck Moshi, alikuwa mhasibu mwandamizi, Isaya Mrema, aliyekuwa mkaguzi wa ndani pamoja na Emaculate Bitegeko.

My take: Hawa Bitegeko naona wote wapo sehemu nyeti sana. Ni ndugu au majina tu?
 
Bitegeko ni majina tu bro,ni kutoka Lake Zone au BK kama wao wanavyopenda kuyaita,huyo Bitegeko wa TCB alikuwa na jeuri kubwa sana ya pesa yeye na mke wake walitengeneza Kampuni moja na kuwaibia wakulima wa Kahawa inaitwa AKIK and Familly,leo wamefikishwa mahakamani kwa mujibu wa taarifa kutokana Divisheni ya mashitaka
 
Bitegeko ni majina tu bro,ni kutoka Lake Zone au BK kama wao wanavyopenda kuyaita,huyo Bitegeko wa TCB alikuwa na jeuri kubwa sana ya pesa yeye na mke wake walitengeneza Kampuni moja na kuwaibia wakulima wa Kahawa inaitwa AKIK and Familly,leo wamefikishwa mahakamani kwa mujibu wa taarifa kutokana Divisheni ya mashitaka
Kwa hio kulikua na mgongano wa maslahi!
 
Hawa Bitegeko wana kampuni inaitwa AKIK ya maswala ya Ujenzi wa majengo na Barabara??? Huwa naona wana kazi nyingi za Barabara Moshi
 
Na hizo kazi nyingi anahonga mbaya mpaka wazabuni wenzake wanalalamika,haiwezekani kwenye halmashauri moja ukapewa kazi saba wewe peke yako kama hakuna rushwa,amesajili kampuni nyingi za ujenzi zaidi ya saba lakini tangu hili sekeseke lianze amepoa sana na hata mjini alikuwa haonekani tofauti na mwenzake Goodluck Moshi
 
Back
Top Bottom