Elections 2010 Birthday ya Raia Mwema, siku ya uchaguzi ishara ya mageuzi

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Tarehe kama ya leo, 31-10-2007, miaka mitatu iliyopita gazeti la Raia Mwema lilianzishwa, miaka mitatu ya gazeti hili limechangia kwa kiasi kikubwa katika mchakato wa mageuzi ya kisiasa na demokrasia ya nchi hii, kwa maoni yangu kwa siku hoo ya Bithday ya Raia Mwema, kuangukia siku ya uchaguzi ni ishara ya mageuzi katika siasa za Tanzania. Kila la kheir Raia Mwema. Kila la Kheir Watanzania.

Haya ni maoni ya mwaka jana yakiakisi maoni ya siku ya kuanzishwa kwake.

Jumamosi ya wiki hii, Oktoba 31, tutatimiza miaka miwili kamili tangu tulipoanzisha gazeti hili Oktoba 31, 2007. Katika kipindi hicho cha miaka miwili tumekuwa tukiulizwa, mara kwa mara, kuhusu ‘anayelimiliki’ gazeti hili; huku baadhi wakidai kwamba ni la chama kimoja cha siasa nchini na wengine wakidai kuwa ni la mfanyabiashara mmoja tajiri jijini.

Ingawa katika toleo letu la kwanza, Oktoba 31, 2007, tulichapisha makala inayoeleza sisi ni nani hasa, tunaamini wengi hawakuisoma makala hiyo kwa sababu ya upya wa gazeti wakati huo, na pengine ndiyo hao wanaoendelea kuhoji ni nani mmiliki wa gazeti hili.

Ni kwa msingi huo tumeshawishika kurudia kuichapisha makala hiyo ya Oktoba 31, 2007 ili wasomaji wetu (wapya na wa zamani) watuelewe vyema sis

Si rahisi kueleza sisi tulioamua kuchapisha gazeti hili ni nani na kwa nini tumeamua kufanya hivyo, pasipo kutaja au kueleza, japo kidogo, tulikotokea.

Hata hivyo, tutajaribu kufanya hivyo kwa uangalifu mkubwa tukitambua unyeti wa suala lenyewe; hasa katika mazingira ya sasa ya ushindani wa magazeti nchini.

Sisi ni nani? Sisi ni sehemu ya kikundi kidogo cha waandishi wa habari ambao mwaka 1993 tulijikusanya pamoja, na tukiwa na visheni moja tulichanga vipesa kidogo, na kwa kutumia nguvu zetu wenyewe, tukaanzisha gazeti la michezo la wiki ambalo mpaka leo ni moja ya yanayoheshimika nchini.

Gazeti hilo moja la michezo likakua na kuwa chanzo cha kuanzishwa kwa kampuni ya uchapishaji iliyokuja, baadaye, kumiliki magazeti mengine matano.

Kampuni hiyo ikakua zaidi, na ikawa ni mfano pekee katika Afrika Mashariki wa kampuni ya magazeti inayomilikiwa na waandishi wenyewe wa habari.

Lakini kwenye mafanikio hakukosi matatizo. Ukubwa wa kampuni unamaanisha ukubwa wa biashara, na biashara yoyote (hasa kubwa) inahitaji ujuzi katika kuiendesha. Lakini sisi hatukuwa wafanyabiashara, tulikuwa waandishi wa habari tu.

Kwa sababu ya kasoro hiyo na nyingine ambazo si busara kuzitaja hapa, kampuni ikayumba kibiashara kiasi cha kukaribia kufa.

Kilichotokea baada ya hapo, sasa, ni historia, lakini yatosha kusema tu kwamba iliokolewa na mfanyabiashara mmoja mkubwa aliyeamua kuinunua kwa kuchukua hisa nyingi na kutuachia vihisa kidogo.

Katika dunia ya biashara, ni jambo la kawaida mtu anaponunua kampuni mpya kuipa mwelekeo mpya na visheni mpya. Na ndivyo pia mfanyabiashara huyo aliyeinunua kampuni yetu alivyofanya. Na ilikuwa haki yake kabisa kufanya hivyo.

Hata hivyo, kwa bahati mbaya, mwelekeo wake mpya na visheni yake mpya vikawa ni tofauti na mwelekeo wetu wa zamani na visheni yetu ya zamani. Sisi watano hatukuwa na kitu kingine cha kufanya zaidi ya “kujing’atua” (au kustaafu?) mapema kwenye taaluma ya uandishi wa habari.

Tukamwachia mwekezaji huyo na wenzetu wengine wawili kuendelea na mwelekeo mpya na visheni hiyo mpya.

Lakini “kujing’atua” mapema au kustaafu mapema katika taaluma unayoipenda kuna matatizo yake. Baadhi yetu tukajenga hisia mapema kabisa za kuutilia shaka usahihi wa uamuzi tulioufanya wa kustaafu mapema uandishi wa habari.

Hata tulipokutana wote, kwa mara ya kwanza, asubuhi ile ya Jumapili, Oktoba 7, 2007, nyumbani kwa mwenzetu mmoja, Mbezi Beach, Dar es salaam, gumzo lilikuwa ni hilo hilo; la jinsi gani tulikuwa tumefanya makosa kustaafu mapema uandishi wa habari.

Kulikuwa na simulizi kutoka kwa kila mmoja wetu wa shutuma kutoka kwa wasomaji wetu (wananchi) wa namna tulivyowaudhi kwa uamuzi wetu wa kustaafu mapema na kuitelekeza visheni tuliyoijenga katika magazeti yale yaliyonunuliwa na mwekezaji; visheni ambayo waliiamini, na kwayo walituunga mkono kwa kununua magazeti hayo.

Kwa hakika, wengine walifikia hata hatua ya kutuita “wasaliti”; jina ambalo halifurahishi hata kidogo kuhusishwa nalo iwe ni kwa mwandishi wa habari au mwanataaluma mwingine yeyote.

Matokeo ya mkutano ule wa Mbezi Beach wa asubuhi ya Jumapili ya Oktoba 7, 2007, ni kuzaliwa kwa gazeti hili la RAIA MWEMA.

Gazeti hili ni jibu la wale Watanzania wote waliokerwa na hatua yetu ya awali ya kustaafu mapema uandishi wa habari. Ni jibu la wale wote waliokosa gazeti makini la kununua linaloheshimu maadili ya taaluma ya uandishi wa habari, na linalotetea wanyonge.

Sisi ni nani? Sisi ni Jenerali Ulimwengu, Johnson Mbwambo, John Bwire, Francis Chirwa na Shaaban Kanuwa. Sisi ndiyo ‘tuliojing’atua’ mapema huko tulikokuwa na kuungana na mwenzetu mwingine, Mbaraka Islam kuanzisha gazeti hili la RAIA MWEMA.

Na kama ilivyokuwa mwaka 1993, gazeti hili nalo ni nguvu na jasho letu wenyewe. Hakuna pesa ya mfanyabiashara mkubwa wala ya mwanasiasa au ya chama cha siasa. Ni vipesa kidogo walivyochangishana wamiliki wake ambao ni sisi waandishi wenyewe wa habari.

Kwa maana hiyo, historia ile ya Mei 9, 1993, imejirudia. Kwa kuanzisha gazeti hili, tunataka kuendelea kuthibitisha kwamba waandishi wenyewe wanaweza kumiliki vyombo vyao wenyewe vya habari bila ya kulazimika kuajiriwa na wafanyabiashara, wanasiasa matajiri au vyama vya siasa.

Tunasita kujivuna au kutabiri kuwa gazeti hili litakuwa mahiri kwa uchambuzi wa masuala mbalimabli yanayohusu mustakabali wa taifa letu au yanayohusu kero za wananchi, kwa sababu sisi si wapya katika fani.

Kweli gazeti ni jipya, lakini sisi tunaoliendesha si wapya. Wasomaji wanaufahamu uwezo wetu kitaaluma, uadilifu wetu kimaisha na hata udhaifu wetu, kutokana na huko tulikokuwa.

Tutajitahidi kuboresha hicho kizuri tulichotoka nacho huko tulikokuwa na tutajitahidi kukwepa makosa yale tuliyoyafanya huko tulikotoka; ili gazeti hili lidumu. Angalau sasa tunajua kidogo mambo ya biashara ya magazeti kuliko tulivyokuwa mwaka 1993.

RAIA MWEMA tutalisimamia sisi, lakini ukweli ni kwamba ni gazeti la wananchi. Ni dimba la mjadala wa wananchi kuhusu masuala mbalimbali yanayowagusa, na sisi tutakuwa waratibu tu wa mjadala huo. Ni dimba la kubadilishana mawazo, kupashana na kuelemishana mambo mbalimbali yanayotugusa ndani na nje ya nchi.

Kwa kutoa fursa hiyo, matarajio yetu ni kwamba RAIA MWEMA litasaidia kuboresha (nchini) utamaduni wa kukosoana, utamaduni wa kuuchukia ufisadi na rushwa na pia utamaduni wa wananchi kusimama kidete kupinga uonevu na dhuluma.

Visheni yetu ni kwamba kama tamaduni hizi zitaboreshwa nchini, basi, pengo kati ya matajiri na masikini pia litapungua; na hivyo kuifanya Tanzania yetu kuendelea kuwa nchi salama ya kuishi.

Na kama visheni hiyo itafikiwa, basi, kila mmoja wetu katika sisi sita, atakwenda kaburini, wakati wake ukifika; huku akiwa na faraja kwamba anaicha nyuma Tanzania yenye amani na upendo.

Tunaomba wasomaji, watoa matangazo na wale wote wanaoipenda Tanzania kwa dhati, na wanaoitakia mema nchi yetu, kutuunga mkono katika kuifikia visheni hiyo ya RAIA MWEMA ambayo, kwa hakika, ni visheni ya raia wema wote.

?

www.raiamwema.co.tz/news.php
 
Happy BD Raia Mwema......
Wishing u the longest possible life!
 
Back
Top Bottom