Mandown
JF-Expert Member
- Apr 8, 2012
- 1,665
- 503
Jumamosi 29/09/2012 nilishtuka kuona mambo ya ajabu nyumbani kwangu, kubwa ni la bint yangu wa miaka 16 ambapo amepatwa na ugonjwa wa kucheka hovyo, sasa imefikia hatua ya kuanguka na kuzirai, akizinduka macho hayaoni kwa muda. Hostpitali hawajagundua ugojwa wowote, manake nilidhani anaumwa malaria. Mke wangu na watu wengine wanadai mambo ya kishirikina ambapo siamini hivo. Jana mke wangu alikuta NGUO YAKE YA NDANI chumbani kwetu, na hakuna anayejua imefikaje huko.
Wadau naomba ushauri
- Nahisi anaugonjwa haujagundulika hospitali, haiwezekani mtu uzimie halafu ukizinduka macho yakose kuona, wanapima hawaoni kitu wanampa panadol.
- Nahisi pia anajifanyisha ili asiende shule, lakini hii ni staili ya pekee kumuona hivi, saa nyingine hataki kabisa ka kaa ndani anabaki nje mpaka tumuingize kwa nguvu.
- majirani wana mshawishi mke wangu kuwa amelogwa..! Sasa amelogwa ananini???? kwanini wachawi wasimloge baharesa, ama mengi eli wamwagiwe mapesa, sie mafukara ndio tunalogana!
Wadau naomba ushauri