Bingwa Wa Mapenzi.....

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,268
17,097
:A S-heart-2:

Hii ni moja ya sifa au tuseme ''title'' iliyokuwepo kwa kitambo sasa. Nyimbo nyingi zimetungwa juu yake na watu wengi wamehusishwa nayo.

Lakini je ni mtu wa aina gani kuwa na sifa au title hii?


  1. Je ni mtu mwenye wapenzi wengi?
  2. Je ni mtu mwenye kuyajua mapenzi?
  3. Je ni mtu anayejua ''kufanya'' mapenzi?
  4. Je ni mtu wa ''kushindana'' katika mapenzi?

Tujadili kwa staha tafadhali!

:A S-heart-2:
 
Safari ni Safari,kwa vidokezo hivyo hapo juu sidhani kama kweli kuna bingwa wa mapenzi
 
Safari ni Safari,kwa vidokezo hivyo hapo juu sidhani kama kweli kuna bingwa wa mapenzi

Basi saidia kwa vigezo vyako.........mimi nimeuliza tu mkuu.....hebu soma utenzi huu wa BIMA LEE ORCHESTRE

Milionea Wa Mapenzi - Bima

Nikuite nani weweee,
Nikuite bwana mapenzi jina hilo halikufai,
Nikuite bingwa wa mapenzi jina hilo halikufai,
Naona bora nikuite milionea wa mapenziii!

Umetuweka ndanii
Sisi wanawake watatu
Khanga na vitenge sie kwetu ni sumu
Mchele wa kitumbo kwetu ni alimasi
Nusu kilo ya sukari utaigawa vipi mara tatu ?

(chorus)
Mpenzi rejea mama aaaa
Mimi naondoka
Waondoka kwa nini mama?
Huoni nilivyokonda
Wakondeshwa na nini mama aaa?
Shida zimezidi....

Kwa heri ee, mpenzi yooyo
Narudi kwa baba na mama walionilea
Sio kama sikupendi, bali ni njaa...
Inayonifanya nikimbie nyumba yako iyele yele
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom